Mradi wa Nyumba ya Utamaduni ambao uliibuliwa kwa njia ya kuwashirikisha wadau zaidi ya 200 na kuanza kutekelezwa mwaka 2005 hivi sasa umekamilika. Kupitia mradi huu wa Nyumba ya Utamaduni majengo mapya matatu (3) yamejengwa na mawili (2) kukarabatiwa na hivyo kuongeza 100% ya nafasi ya kuhifadhi mikusanyo, kuwa na kumbi za kisasa kwa ajili ya maonyesho ya jukwaani na maonyesho ya kudumu, studio ya watoto kujifunzia sanaa, studio ya kurekodi muziki na chumba kwa ajili ya mawasiliano ya mtandao (multi-media centre).

Mafanikio ya mradi yanadhihirishwa na tuzo mbili; mradi umekwisha kupata kutokana na kuwa mradi bora katika Ushirikishaji, Usanifu na Usimamizi iliyotolewa katika maonyesho ya Wasanifu majengo Ujerumani mwaka 2008 na Meneja Mradi Dkt. Paul J. Msemwa kwa kupata tuzo iliyotolewa na “Hans Menneby Memorial Foundation for Museum Development” ya Sweden mwaka 2009 kwa mchango wake wa kuendeleza Makumbusho Duniani.

Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ambao umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Sweden ni mkubwa kwa Sekta ya Malikale kuwahi kutekelezwa hapa nchini. Aidha, kutokana na kukamilika kwa mradi wadau wa ndani na wa kutoka nje watatumia huduma za mradi katika kutangaza kazi zao na kujiongezea kipato kutokana na vipaji vyao.

Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 3 Desemba, 2011 atazindua rasmi miundombinu ya Mradi wa Nyumba ya Utamaduni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...