Mkuu wa wilaya ya Moshi,Musa Samizi wa pili kutoka kulia akizindua safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kama kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru,wa kwanza kulia Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza,Wa kwaza kushoto ni kiongozi wa wapanda mlima na mmtoto wa hayati baba wa taifa,Mwl Julius Nyerere,Madaraka Nyerere na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Zara Tours,Zainab Ansell.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi

MTOTO wa baba wa taifa,hayati Mwl Julius Nyerere, Madaraka Nyerere amesema kitendo cha baadhi ya viongozi kuchanganya biashara na uongozi kinachochea kushindwa kutoa maamuzi sahihi katika baadhi ya mambo ya kiutendaji.

Madaraka aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akiwa kama kiongozi wa msafara wa watu 90 kutoka ndani na nje ya nchi wanaopanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru.

Alisema miaka ya nyuma maadili ya uongozi yalikataza viongozi kujihusisha na biashara lakini sasa hali ni tofauti huku baadhi ya masuala yanayojitokeza yanachochewa na viongozi kujihusisha na biashara jambo ambalo linasababisha mgongano wa maslahi.

Katika safari hiyo iliyandaliwa na bodi ya utalii Tanzania(TTB),Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na kampuni ya usafirishaji watalii ya Zara Tours,Madaraka aliwataka watanzania kujivunia amani iliyopo kwa kuendelea kuitetea bila kuvuruga misingi imara iliyopo.

“Leo hii Tanzania ni nchi ya kihistoria tunatimiza miaka 50 tukiwa bado ni wamoja…lazima tukiri kwamba yapo mafanikio mengi yaliyojitokeza katika Nyanja mbalimbali lakini pia tujenge utamaduni wa kupanda mlima huu tusione ni wageni pekee”alisema.

Awali akizindua safari hiyo,mkuu wa Wilaya ya Moshi,Musa Samizi amewataka watanzania kuienzi amani na utulivu ikiwemo kuepuka masuala ya udini, ukabila na ubaguzi wa aina yoyote ambao ukiachwa utahatarisha umoja miongoni mwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Zara Tours, Zainab Ansell alisema kampuni yake itaendelea kuandaa safari hizo kila mwaka kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru sanjari na kuutangaza mlima Kilimanjaro kuwa upo Tanzania.

“Kampuni imeona ni vyema kuendelea kumtumia Madaraka Nyerere kama kiongozi wa safari za kupanda mlima Kilimanjaro kila mwaka,kwanza kuutangaza mlima lakini pia kuwahakikishia wageni wetu kwamba Tanzania itaendelea kuwa nchi ya amani”alisema.

Naye Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza alisema shughuli hiyo ni moja wapo ya masuala yaliyokuwa yamepangwa na TTB katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kama sehemu ya kutangaza utalii wa ndani.

Alisema suala la utalii katika baadhi ya vivutio nchini limefanywa kuwa ni la wageni pekee na kwamba ni wajibu wa watanzania kuvitembelea ili kujivunia raslimali zilizopo kuliko kuonekana ni kwa ajili ya wageni pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mama Zara nakukubali kwa kuzicghungulia deal

    ReplyDelete
  2. Sasa kipi ni kipi,,,humu kt mtandao wa jamii ndani ya blogu jana na juzi taarifa zimesema wanaopandisha bendera na mwenge wa Uhuru nu watoto wa shujaa Hayati Alexander Nyirenda,,,leo tunasikia tena ni Madaraka Nyerere,,, hivi watoto wa marehemu Nyirenda hawakutosha kufanya kitu hicho ikawa tumemamiliza?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...