Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho(kushoto ) akitoa cheti na cheki ya shilingi laki saba kwa mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Renatus Mutabuzi wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho(kushoto ) akiongea na waandisha wa habari jana jijini Dar es salaam wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za UKIMWI nchini (AJAAT) Simon Kivamo na kulia ni Afisa Uraghibishi (Advocacy Officer) wa TACAIDS Simon John.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za UKIMWI nchini (AJAAT) Simon Kivamo(kulia) akiongea na waandisha wa habari jana jijini Dar es salaam wakati wa tafrija fupi ya utoaji wa zawadi na vyeti kwa washindi wa shindano la waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za UKIMWI kwa makundi ya watu wenye fursa chache . Kushoto ni Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...