Jiji la Wuhan

Hii ni tahadhari iliyotolewa na watu wanaoishi maeneo ya Wuhan kuwataka Watanzania popote walipo nchini China hasa kwenye mji wa Wuhan kuchukua hadhari za lazima ili kuepuka hatari.  

Shukran kwa "Mzalendo" aliyeona vyema kusambaza ujumbe huu muhimu.
------------------------------------------------------------------------------

Wakuu kipindi tunaelekea mwisho wa mwaka kuna matukio mengi mno yanatokea hapa Uchina hususan Wuhan, ingawa kwa wengi wetu tunaweza kudhani kuwa Uchina hakuna uporaji, maharamia n.k.;  Si kweli ila ni kutokana na mazingira ambayo tunaishi hatujawa "exposed" sana kuweza kujua haya mambo, ila ukweli ni kuwa China kuna kila ushenzi kama mahali popote pale duniani. 

Katika siku hizi za karibuni kwa wale wafuatiliaji mtakuwa mmejionea matukio kadhaa, mfano:
  1. Utekaji wa watu na kutoa viungo vya ndani (this happened in many Chinese Cities, Wuhan is one of them)
  2. Upigaji wa bomu kwenye benki ya Communication iliyo karibu na Zhongshan Middle School ili kupora fedha. Tukio lililopelekea watu kadhaa kujeruhiwa na mmoja kupoteza maisha palepale.
  3. Jana mchana, benki nyingine Mishen Bank Donghu Branch ilivamiwa kwa mtindo huo huo.
  4. Wiki mbili zilizopita jamaa walifunga mtaa shuleni kwetu mitaa ya saa sita usiku na kusabababisha kizaazaa.
  5. Binafsi niliibiwa kadi ya benki nikiwa nalipia dawa. Ilikuwa hospitalini. Kitendo kilikuwa kama mazingaombwe kwani ndani ya sekunde kadhaa (ninamaanisha SEKUNDE kweli) kadi niliyotumia kulipia dawa sikuiona wakati Hospitali hakukuwa na watu wengi (was one of the private Hospital.)

Hayo ni yale ambayo tumeyasikia au kuyashuhudia, kwa wale wanaojichanganya na Wachina watakuwa tayari washataarifiwa hilo kwani siku hizi hii ni mada moto. 

Sasa binafsi ninakushauri yafuatayo:
  1. Punguza nyendo za usiku zisizo na tija, haswa kwa wale wenzetu ambao kila wakati wapo "tilalila". Watu WANATAKA VIUNGO jamani. Inapobidi omba "kampani" ya watu wengine.
  2. Usiende sehemu usiyoijua na Mchina usiyemuamini au asiyeaminika.
  3. Usichukue mula usiku labda iwe ni dharura isiyosubiri, na inapobidi basi tafuta benki zilizo wazi.
  4. Epuka mikwazo na Wachina ikiwemo kugombea wachumba, kwani hasira kwenye jambo A linaweza kuwa ni  kichocheo kwa tukio B (mnajua ninamanisha nini hapa).
  5. Epuka "Ganbei" (mitoko) ya ajabu na Wachina. Hii haswa kwa wale wanaojiachia kwani wanaweza tumia vilevi kukuzimisha au kukuwekea kitu.

Niishie hapa, haya niliyoyasema ni kwa ajili ya usalama wa wote na ni maono binafsi. Mnakumbuka tukio lililomtokea jamaa wa Rwanda (Burundi) mwaka jana. Shime mjilinde!
source: http://www.wavuti.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kuweni na tahadhari,,,uhalifu ni dunia nzima, tena kila sehemu na kiwango chake!.

    ReplyDelete
  2. Kweli mdau wewe ni muungwana,hizo ndo ujumbe wa maana wa kuwatahadharisha wenziwe kitu kama hicho cha hatari!Ubarikiwe sana sana!wengi wanatakiwa wafuate mwenendo wako,,Shukrani,,,,
    Ahlam...UK

    ReplyDelete
  3. Mangi wa KiboshoDecember 07, 2011

    asante ndugu kwa taarifa kumbe na huko kuna wanyamwezi na wasukuma kama huku kwetu wanaoua albino?

    ReplyDelete
  4. Nimependa sana uungwana na uzalendo uliouonesha mdau. Mungu akubariki sana. Umeonesha ni jinsi gani ambavyo una mapenzi mema na watanzania wenzio. God bless

    ReplyDelete
  5. Si China tu na Far East ndio sana ma Taiwan Thailand Philipinese huku hatari muwe makini hata mnavyopeleka wagonjwa INDIA mbona wengi wanaondoka kama kweli kuna madaktari(Waganga) bingwa.

    ReplyDelete
  6. Wewe uliotoa taarifa hizi ni muungwana sana na mfano wa kuigwa kwa kujali maisha ya wenzio. Ndugu zangu Watanzania tuzingalie tahadhari hii.

    ReplyDelete
  7. Kumbe viungo ni mali mpaka China, loh!

    Lakini nimpe hongera aliyetupa tahadhari hii kwani imetufungua macho sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...