TANZANIA imekuwa kileleni mwa nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa kasi ya ukuaji sekta ya elimu, imeeleza ripoti maalumu iliyotolewa hivi karibuni

Katika ripoti hiyo, iliyotolea na shirikisho maalumu la taasisi zinazosimamia elimu katika ukanda huo, Kenya imeshika nafasi ya pili katika somo la Hisabati, baada ya Mauritius.

Ingawa zimekuwa vinara katika somo hilo, kwa mujibu wa Shirikisho la Kufuatilia Ubora wa Kitaaluma katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Tanzania inaongoza kwa ujumla hasa kwenye stadi za usomaji, ikifuatiwa na Shelisheli, Mauritius na Swaziland.

Shirikisho hilo linahusisha wafuatiliaji wa pamoja kutoka katika Wizara za Elimu na Mabaraza ya Mitihani ya nchi 15 zilizoshirikishwa katika utafiti huo. Nchi zilizobaki katika ukanda huo wa Afrika Mashariki na Kusini zikiwemo Malawi, Zambia, Lesotho, Namibia na Uganda, kwa mujibu wa matokeo hayo zimeripotiwa kufanya vibaya hasa katika somo la Hisabati, baada ya kubainika kwamba wanafunzi hawawezi hata kukokotoa matatizo kwa kutumia kanuni ya msingi kwenye somo hilo.

Shirikisho hilo limetoa taarifa hiyo iliyoiinua Tanzania, baada ya kufanya utafiti kwa kuhojiana na wanafunzi 4,436 wa darasa la sita kama sampuli kwenye shule 193 katika nchi husika. Nchi za Malawi, Zambia, Lesotho, Msumbiji na Uganda, zimeripotiwa pia kufanya vibaya zaidi katika suala la stadi za usomaji.

“Viwango vya ubora wa elimu katika nchi 15 bado ni duni japokuwa kumekuwa na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na serikali za ukanda huu kwa ajili ya kuboresha viwango hivyo,” alisema mkuu huyo wa shirikisho hilo, Demus Makuwa. Utafiti huo ulijumuisha majaribio ya somo la Hisabati kwa wanafunzi hao kwenye nchi hizo 15.

Shirikisho hilo linahusisha mtandao maalumu wa Wizara za Elimu kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kielimu na malengo ya maendeleo ya milenia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wadau naomba kama kuna website yoyote ambayo ningepata source ya hii habari.

    ReplyDelete
  2. Mnaona sasa?

    STADI ZA ELIMU TUPO JUU AFRIKA MASHARIKI

    Ohhh Tanzania,,,kila kitu tupo nyuma, haya sasa habari ndio hiyo!

    Ohhh Tanzania,,,Uhuru miaka 50, hatuna maendeleo kabisa!

    Unakuta mtu anampeleka mwanae kusoma Kenya au Uganda kwa vile lugha ya masomo kule ni Kiingereza!

    Nani aliwaambia kuwa kujua lugha ya Kiingereza ndio kuelimika?

    Japan ,Ujerumani, Ufaransa na nchi zingine zemeendelea ,je zinatumia lugha ya Kiingereza?

    Mara nyingi watu wenye mawazo pinzani ya kuirudisha nyuma Tanzania kwa ulinganishi wa mambo mbalimbali hawana vigezo wanapoulizwa!

    Tujaribu kubisha kwa hoja!

    ReplyDelete
  3. Mdau Mtoa maoni wa kwanza,,,mambo kama haya usitafute source kama web site,

    Chukua vyanzo (source) kama

    Mashirikisho ya Kimataifa kama:
    -UNESCO
    -UNICEF
    -UNDP
    -WORLD VISION

    Na mashirika ya Balozi kama:
    SIDA- ya Ubalozi wa Sweden
    CIDA-ya Ubalozi wa Canada
    DANIDA-ya Ubalozi wa Denmark
    NORAD-ya Ubalozi wa Norway na mengineyo,

    huko wanatoa ulinganishi wa nchi nyingi kwa taarifa zilizokusanywa kwa pamoja (consolidated report) na matokeo yanatolewa,

    Huku wakitumia (scientif criteria in accessment) vigezo vya kisayansi na kitaaluma badala ya Siasa na hawako biaised,,,huko ndio utahakikisha na kujua mbivu na mbichi!

    ReplyDelete
  4. Tatizo ktk Watanzania wengi daima wana mawazo mgando, wengi wanajua sisi kila siku na kila kitu tupo nyuma tu!.

    Ndio maana taarifa kama hizi zikitoka watu wanakuwa hawa amini amini vile, kumbe habari ndio hiyo!

    Yawezekana taarifa hiyo imetoka ktk mashirikisho kama hayo hapo juu Mdau wa 3 ameyaelezea ambayo yanapima mambo (mfano mitaala ya kielimu) kwa kutumia akili sio muonekano tu au kusikia.

    Kwa vile kasumba na utamaduni uliopo ni kuwasafirisha watoto kusoma nchi jirani bila kutumia vigezo, basi kila mtu anafuata mkumbo tu!

    Tena leo asubuhi hii nilikuwa na maongezi ktk Kijiwe cha Kahawa na Wadau hapa Dar Es Salaam tukakuta baadhi ya viongozi hapa Afrika Mashariki walisoma University of Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  5. Ripoti hiyo ya Sept 2010 inapatikana hapa:

    http://www.sacmeq.org/reports.htm

    SACMEQ III Policy Series, Policy Issues Series Nr 2: Makuwa, D.(2010)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...