Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, 
Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Mh. Omar Yussuf Mzee
Ujumbe wa Viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho unatarajiwa kuondoka Zanzibar hii leo kuelekea Beijing, China kwa ziara ya mafunzo ya wiki mbili.

Wakiwa nchini China viongozi hao wanatarajiwa kujifunza mambo mbali mbali ya kiutendaji pamoja na kutembelea maeneo muhimu ya uwekezaji yanayotegemewa kwa uchumi wa nchi hiyo.

Viongozi hao pia watapata fursa ya kutembelea Mji wa Shangai na Suzhuo ambapo pia wataweza kutembelea sehemu muhimu ikiwemo maeneo ya viwanda.

Mbali na Spika Kificho msafara huo utakuwa na Mawaziri nane na Naibu Waziri Mmoja wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Wengine ni wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Maofisa na Watendaji waandamizi katika Wizara mbalimbali pamoja na waandishi wa habari

Akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa kuagana na viongozi hao katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi,waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee amesema ziara hiyo ni muhimu kwa viongozi hao na Zanzibar kwa ujumla.

Amesema kwa kiasi kikubwa China imepiga hatua kubwa kiuchumi hivyo Zanzibar nayo kama inataka kuendelea ni jukumu la viongozi hao kujifunza na kuja kuitumia taaluma watakayoipata China kuja kuibadilisha Zanzibar.

Ujumbe wa viongozi hao unatarajiwa kurejea Nchini Desemba 20 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Duuh mawaziri nane! wote hao! naona ni wengi kwa safari, ni robo ya Baraza zima la mawaziri, hata kama ziara itakuwa imelipiwa na China, kundi zima la viongozi kwenda kujifunza sehemu moja haipendezi, basi angalau wangeenda watendaji wengi zaidi.

    ReplyDelete
  2. Basi ingekuwa watanzania bara ndio wanaenda wakati kuna sikuu ya mapinduzi wazanzibar wangenuna hao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...