Mkurugenzi wa shirika la kusaidia maalbino Tanzania (Afrobino) Bw Babu Sikare akipokea msaada wa Viti 400 na madawati 200 jumla vyenye thamani ya Tsh. Millioni 45 kutoka kwa Mmiliki wa kampuni ya Alexander Global Furniture ya Houston, Texas USA. Bw Alexander
Bw Fumbuka akiionyesha Team ya Afrobino ubora na bei ya baadhi ya bidhaa vinavyopatikana Alexander Global Furniture. Alisema viti na madawati aliyokabidhi, yana uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 50 vikitumika vizuri.
Wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyokabidhiwa kwa Afrobino, Bw Sikare akishukuru kwa msaada; alisema katika ziara aliyofanya mapema mwaka huu kutembelea shule za wenye ulemavu Tanzania, aligundua uhaba mkubwa wa madawati kwa wanafunzi. 

Aliongeza kuwa Bw Fumbuka awe mfano wa kuigwa na watanzania kwa kujitolea chochote tunachoweza badala ya kuwa na fikira potofu kuwa wazungu pekee ndio wenye uwezo wa kusaidia.

Pia Sikare alitoa shukurani za dhati kwa kampuni ya HEFEMI Films ya Houston, TX, ESM Travel ya Chicago, IL na Pillarsis Software Systems ya Tanzania kwa muendelezo wa kusaidia albino kupitia Afrobino. Pia ameomba Serikali na vyombo husika kusaidia shirika hilo lisilo la kiserikari la Afrobino kwa kuondoa zengwe bandarini punde container la misaada litakapowasili mwanzoni mwa mwaka 2012.

Pichani, mikononi wote wamevaa band za blue (wristbands) zinazowakilisha Afrobino kwa ishara ya mshikamano

 Tembelea www.afrobino.org au tuma email: info@afrobino.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Babu Sikare....na Afrobino....hayo madawati tunaomba yaende kwenye shule zinazohitaji kweli msaada huko vijijini na sio yaishie shule zetu za Dar hapa...hawana shida !

    ReplyDelete
  2. Big up Fumbuka, tunahitaji kufuata mfano wako.

    Betram
    Bs Hyera Shipping LTD

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...