Abiria: "Kuna Kiti au unasema panda tu!?"
Konda: "We taahira nini,hao wengine wamekaliandoo?! "

*******************************
Abiria: "Embu punguzeni sauti ya redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu ziko za kutosha, tusikilize na zako!?"

*******************************
Mmama: "Bwana ondoa gari joto sana!!"
Konda: "Uctuzingue wewe,shuka upande fridge...."

******************************
Konda: "Anti, kuna siti pale nyuma,ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe, sio muendaji!!! Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"

********************************
Sister duu: "Konda unanibana bwana..."
Konda: "Zinabanana ndizi haziongei, kama ulitaka kujiachia si ungekodi treni pekeyako!!!"

*******************************
Sharobaro: "Kuna kiti?!kama hamna sipandi..."
Konda: "Mpuuzi kweli, wa wapi wewe... Kama ulikuwa unaogopa kukosa kiti si ungebeba chako?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. inachekesha sana,,,, nimeburudika hasa baada ya kutoka kwenye pepa yangu ya funga semester....

    ReplyDelete
  2. Lmaooooooo!!!!!
    mdau texas

    ReplyDelete
  3. nimeipenda hiyo ya yesu na fridge

    ReplyDelete
  4. We! Michuzi hiyo ya kwanza unatudhiakia dini yetu! Ingekuwa Mtume SAW unamdhihaki hivyo saa hii ungeshapewa Fatwah! Lakini dini zingine zinauvumilivu. Tunaomba uondoe hii dhihaka hatufurahishi hata kidogo! Yesu ni Mungu na usifanye dhihaka na Mungu!

    ReplyDelete
  5. Yesu ni Mungu na dhambi kumdhihaki namna hiyo.Kuna kipindi watu walimchora mtume Muhamad kikatuni duniani ilikuwa haikaliki...nadhani haipendezi kuweka dhihaka hapa...hebu jaribu kudhihaki waislam na uwone moto wake.....wakristo tunauvumilivu...

    ReplyDelete
  6. Makonda wa Dar wana matusi kupita maelezo. Sijui ni nani aliwaroga??? Mungu awasamehe.

    ReplyDelete
  7. hivi kwani post ni za michuzi? au ni sisi mabingwa wa kucomment. siye tuandikao tusichafue hali ya hewa.

    ReplyDelete
  8. .............. hapo palipopigwa jamaa zetu mbona sipaoni ? umeondoa nini Ankal ? ........... mbona kuna ile dhihaka ya yule muimbaji anasema ameuonja utamu wa Yesu (Mtoto wa kike) lakini hamjekemea ?.......... anywway you make my day!

    ReplyDelete
  9. Je hawa daladala kwa nini hawataki kufuata sheria za barabarani. wanajivunia nini. wanaosimamia wanaonaje hali hii ya barabara kutotawalika? Nikisafiri kwa daladala hasa usiku nakuwa roho mkononi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...