Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akijaribu kuliendesha trekta kabla ya kukabidhi matrekta mawili kwa wakulima wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Singida, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi matrekta mawili diwani wa Kata ya Kwadelo mkoani Singida, Omari Kariate, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo. Trekta hizo ambazo ni mkopo kutoka Shirika la SUMA JKT ni kwa ajili ya wakulima wa Kata hiyo. Wengine pichani ni Wajumbe kutoka Chama Cha Wakulima wa Kata hiyo waliohudhuria makabidhuano hayo. (Picha na Bashir Nkoromo).

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amewataka viongozi kuongoza kwa vitendo badala ya maneno.

Nape alisema hayo wakati akikaidhi matrekta mawili kwa wakulima wa Kata ya Kwadeo wilaya ya Kondoa mkoni Singida, katika hafla iliyofanyika leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.

Wakulima wamepata matrekta hayo kwa mkopo kutoka Shirika la Suma JKT, kupitia mpango wa kuhamasisha kilimo cha kisasa unaosimamiwa na diwani wa kata yao ya Kwadelo, Omari Kariate.

Wamefanikiwa kukokpeshwa matrekta baada ya kuweza kulipa asilimia 50 ya gharama yote ya ununuzi ambayo trekta moja ni sh. milioni 25.

"Ili mapinduzi ya kweli yaweze kufikiwa katika kilimo na sekta nyingine za maendeleo ni lazima sasa viongozi waepuke mtindo wa kufanya kazi wa nadahria tu, badala yake wajikite katika kuonyesha vitendo, diwani huyu ameonyesha mfano mzuri wa kuingwa", alisema Nape.

Nape alisema hatua ya diwani huyo kuanzisha mpango na kuuhamasisha kwa wananchi hadi kukubalika na kuweza kutoa matunda si jambo la mzaha ni suala la dhamira ya kweli katika uongozi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, diwani wa Kata hiyo, Kariate alisema, mpango wake wa kuhamasiaha wakulima kuwezeshwa kutumia matrekta umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa sasa kata hiyo ina jumla ya trekta tisa zote za mkopo kutoka SUMA JKT.

Alisema, kupitia mpango huo sasa wakulima wa kata hiyo wanaweza kulima kisasa zaidi na hivyo kujipatia mavuno mengi kuliko kutumia jembe la mkono. wilaya ya Kondoa hulima mazao ya mahindi, uwele na alizeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi hiyo ya kata ya kwadelo ipo wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma na sio Singida.
    Mdau wa kirangi
    Masomoni Malaysia

    ReplyDelete
  2. Hivi siku hizi primary hamfundishwi jigrafia? Maana wilaya ya Kondoa miaka yote tangu enzi ya mkoloni iko mkoani Dodoma leo hii imehamia mkoa wa Singida? Kweli kiwango cha elimu kimeshuka sana Bongo.

    ReplyDelete
  3. Big up sana Kariati! Naona jitihada zako za kimaendeleo unazidi kuzidhihirisha. Naamini utafanikiwa zaidi! Hamasisha maendeleo. Kila la kheri.

    Mdau- Uzunguni, Dom

    ReplyDelete
  4. trekta la mkopo nalo lazima ukabidhiwe na Nape Nnauye? ama kweli chama kimeshika hatamu.

    ReplyDelete
  5. Mheshimiwa Michuzi,
    Hiyo habari unaweza kuirekebisha kidogo. Dunia nzima watoto wetu wanasoma Kondoa ipo mkoani Singida, na si kweli. Wilaya hiyo ipo Mkoani Dodoma.

    Asante sana...
    Mdau,
    USA

    ReplyDelete
  6. Hivi huyu Nape hio Balzer (Jacket) hanaga lingine? Maana toka alinunue ile safari yake ya US imekuwa likirudiwa mnoooo.

    Kingine sasa hivi, ni iPad yake. Kila mkutano anaiweka mbele pale...........haaaa. Ya nini jamanii? Kazi yake ni nini hasa, hufanyi presentation wala nini! Probably hata siyo 3G, kwahiyo hawezi kupata internet mpaka aweze kupata free WiFi ambayo si rahisi maeneo anayokwepo....Kazi kwelikweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...