Ile sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara  ambayo ilikuwa inasubiliwa na Watanzania wote nchini Italy, ilifanyika siku ya ijumaa tarehe 9 Disemba 2011. Sherehe ilipambwa na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italy kama vile Rome, Modena, Napoli, Siena na sehemu zingine na pia kuudhuliwa na wageni kadhaa kutoka nchi rafiki za Tanzania.

 Mgeni wa heshima alikuwa Kaimu Balozi, Mh. Salvatory Mbilinyi ambaye aliambatana na maafisa wote wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy. Sherehe ilianza kwa kuimba wimbo wa Taifa na baadae mgeni waheshima Kaimu Balozi Mh. Salvator Mbilinyi kuIfungua rasmi. 

Kaimu balozi alianza kwanza kwa kuelezea umuhimu wa kusherekea siku hii ya miaka 50 ya uhuru na baadae kuelelezea kistoria jinsi gani Tanzania ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni wa kiingereza. Mh. Kaimu balozi aliwashukuru pia Watanzania wote kwa ushirikiano wao walioonyeshe kwenye kuiandaa siku hii muhimu. 

Aliwashukuru zaidi viongozi wa jumuiya mbali mbali za kitanzania hapa Italy kwa ushirikiano waliouonyesha kwenye maandalizi ya sherehe hii. Mungu Ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 Kaimu Balozi  Mh. Salvatory Mbilinyi akikata keki ya miaka 50 ya uhuru
Katibu wa Modena Mh. mwinyimwaka  (shoto) na Katibu wa Rome  Mh. Andrew Chole Mhella

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu Urbun Pulse ametoa kitu kidogo nini kwenye ubalozi. Maana naona shughuli zote za ubalozi anapiga picha na kuchukua video yeye?

    ReplyDelete
  2. sasa wewe wivu wa nini? Mkimwona mhindi kapewa tenda hiyo mnasema rushwa mbongo mwenzetu kapewa tenda maneno kibao shut it boy/girl what ever you are

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...