Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akikata utepe kuzindua mbio za kumi za Kilimanjaro Marathon 2012 zitakazofanyika Februari mwakani. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto), Listone Metacha, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Mkurugenzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon, John Bayo. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akifurahia baada ya kukata utepe kuzindua mbio za kumi za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Februari mwakani. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto), Listone Metacha, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Mkurugenzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon, John Bayo. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.

Na Mwandishi Wetu, Moshi

WANARIADHA wa Tanzania wake kwa waume wamepewa changamoto kuhakikisha wanashinda mashindano ya riadha ya kimataifa ya Kilimanjaro Marathon, yanayotarajiwa kufanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Februari 26, mwakani.

Changamoto hiyo imetolewa na meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo iliyofanyika mjini Moshi, mwishoni mwa wiki.

“Napenda kutoa changamoto kwa wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanashinda medali za dhahabu katika mashindano ya mwakani ambayo ni ya 10 tangu kunzishwa kwake”, alisema.

Aidha alitoa changamoto kwa uongozi wa chama cha riadha nchini, (RT), kuanza kuwaandaa wanariadha mapema ili waweze kutimiza azma hiyo na kuiletea Tanzania sifa.

Kavishe alisema kuwa washiriki wa mwakani wana kila sababu ya kujituma zaidi kutokana na wadhamini wakuu wa mashindano hayo bia ya Kilimanjaro Premium Lager kuongeza zawadi kwa washindi wa kilomita 42.1 kwa asilimia 100. Alisema ongezeko hili la zawadi ni maalumj kwa ajili ya maadhimisho ya miaka kumi yam bio hizi.

Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, Kavishe alisema kuwa washindi wa kwanza watajinyakulia shilingi milioni 6, milioni 3 na milioni 1.75 na kwamba Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kutoa zawadi zenye dhamani jumla ya shilingi 22. Kwa mujibu wa Kavishe,zawadi zote kwa ujumla zinatarjiwa kuwa na thamani shilingi milioni 50.

Aliendelea kusema katika mashindano ya mwaka 2011, mshindi wa kwanza kwenye kilomita 42.1 alizawadiwa shilingi milioni 3, wa pili milioni 1.5 na wa tatu shilingi 850,000.

Akiongea katika half hiyo, Mkuu wa Mkoa Gama aliwapongeza wadhamini wa Kilimanjaro Marathon kwa kuongeza kiwango cha zawadi jambo ambalo alisema litasaidia kuwahamasisha washiriki kujitokeza kwa wingi zaidi.

Alisema mashindano hayo ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro na hii ni kutokana na wingi wa washiriki ambao alisema huongeza pato la wakazi wa Mkoa huo.

“Mwaka 2011 takribani watu 5,000 walishiriki na wote hawa walitumia vyakula, vinywaji na malazi katika mahoteli ya mkoani hapa, hivyo kuongeza kipato cha mwana Kilimanjaro”, alisema.

Gama alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kuendeleza tabia njema ya ukarimu waliyo nayo kwa wageni ill kudumisha mahusiano mazuri kati ya wana Kilimanjaro, Watanzania kwa ujumla na washiriki wanaotoka nje ya nchi ambapo alisema serikali mkoani humo itahakikisha hali ya usalama inakuwa shwari wakati wa mashindano hayo hapo mwakani.

Kilimanjaro marathon ya mwaka 2012 Kilimanjaro Marathon itagawanywa katika makundi manne, ambayo ni pamoja na yale ya kilomita 42.1 yatakayojulikana kama Kilimanjaro Premium Lager Marathon,mashindano ya nusu marathon; mashindano ya nusu marathon kwa watu wenye ulemavu na ambayo yatadhaminiwa na GAPCO na yale ya kilomita tano ambayo yatadhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Mbali na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu, wadhamini wengine ni pamoja na GAPCO Tanzania; Vodacom Tanzania, CFAO Motors, Tanga Cement, Tanzanite One, Keys Hotel, Precision Air,Kilimanjaro Water, TPC Sugar, Southern Sun, KK Security na Bodi ya Utalii Tanzania, (TTB).

Mashindano hayo yanaandaliwa na kampuni ya Wild Frontiers yenye makao yake makuu Afrika Kusini na kuratibiwa na kampuni ya Executive Solutions ya hapa nchini kwa ushirikiano wa karibu na chama riadha nchini RT na kile cha Mkoa wa Kilimanjaro, (KAAA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...