Baadhi ya wazazi waliojifungua wakati wa mkesha wa Krismasi wakiwa na watoto wao leo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo, Erika Massawe watoto 16 walizaliwa hospitalini hapo wakiwemo wakiume kumi na sita wa kike.Picha na Francis Dande

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hao wawili kama baba zao wapemba vile!

    ReplyDelete
  2. Kwani mpemba si ntu???

    ReplyDelete
  3. hongereni sana wamama kwa kupata zawadi ya watoto siku ya christmas!

    ReplyDelete
  4. this is a great blessing natamani.

    ReplyDelete
  5. kilichokufanya useme baba zao ni wapemba nini?tafadhali jibu kabla sijakasirika

    ReplyDelete
  6. I hope hawajaibiwa wengine maana Mwananyamala wezi wa vichanga

    ReplyDelete
  7. Mi naona wote baba zao watakuwa wachina kwa sababu naona kama vile watoto ni weupe sana..au labda tusime kuwa tunazaliwa wazungu lakini tunabadilika ngozi kwa sababu ya jua la africa au?

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza na wa pili hapo juu,,,,Mpemba anaogopwa kwa vile wao ndio wenye Maduka mengi hivyo inakuwa utata sana wakati wakopaji wakipita madukani hasa (wengi wao akina dada),,,,wanaweza saidia watu kuchangia mbegu ktk uzazi, inakuwa ndio nafasi ya Dhahabu kwao!

    ReplyDelete
  9. kuazliwa kwa watoto ukifatilia kwa karibu utagundua kuwa kila dakika ni watoto wasiopungua elfu 20 wanazaliwa duniani na kwa kila saa wanazaliwa na kwa kila siku wanazaliwa no matter siku ya eid wala mwaka mpya wa xmas

    na huyo aliesema watoto kama ni wapemba inaonekana kaumiziwa mkewe na mpemba ndio maana kitu cha kwanza kakumbuka wapemba maana itakuwa mpemba anamlipia kodi ya nyumba na huku ana kula bata na mkewe....hehhehehe raha sana

    mwaume kaza buti usikubali kuhudumiwa na kidume wa ukweli utakuja kugeuzwa simba wa malindi upakatwe na upewe chai

    au sio ankali? au nakosea?

    ReplyDelete
  10. Wamepata watoto lkn sura hazina furaha kabisa wanawaza jinsi ya kuwakuza na hali ngumu ya maisha mbele yao maana hawajui hata wakaanzie wapi....Mungu tuhurumie watanzania!!!

    ReplyDelete
  11. Jamani wamechoka bado hawajapata nguvu, kuzaa si kama kwenda chooni.
    Hongereni sana dada zangu, Mungu awajalie wakue vema.

    ReplyDelete
  12. Hawa akina mama wamechoka sana. mbona wamewapiga picha mabega wazi jamani? Yule wa kati kama anataka kulia vile!

    Hongeara na poleni sana jamamni.. kuzaa shughuli kweli kweli. Ukiona mtoto hamtii mzazi wake hiyo ni laana tosha

    ReplyDelete
  13. jamani sio kwamba hawana furaha, kujifungua jamani sio lele mama,uliza wazazi watakwambia. Ng'ombe mwenyewe na mwili ule lakini akimaliza kuzaa lazima akae chini,sembuse mwanadamu. Tuwaheshimu tu mama zetu jamani.

    Hongereni sana!

    ReplyDelete
  14. Uzazi si lelemama, acheni masihara jamani!

    ReplyDelete
  15. jamani watoto wapya jaani waliyozaliwa wanakuwa weupe baadae wanapata rangi zao kamili. Tumboni jua haliwaki na ngozi haipati vitamini kutoka mwanga wa jua.

    ReplyDelete
  16. Mie ni mwanamke na nimezaa vilevile kweli kuzaa si lelemama lakini tuseme ukweli hawa wazazi wenzetu hawana nyuso za furaha kabisa wanawaza ulezi utakavyo kuwa na pengine wengine toka ujauzito wanaume washa wakimbia au hawawajali. Kama maiti tu inaweza kuonyesha uso wa tabasamu kama mtu akifa vizuri basi hata kuzaa na kuchoka kwake bado nuru ya furaha itaonekana usoni. Uzazi sasa hivi si mchezo hasa ukianza fikiria ada za shule na watoto wa siku hizi miaka mitatu kesha jua shule na anaililia we acha tu haya na iyo elimu ya juu mikopo watoto wetu hawapati wanapewa watoto wa wakubwa au wenye majina du - kazi si kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...