Ankal, 
salaam zako popote pale ulipo na pia nakutakia kheri ya mwaka mpya pamoja na wana jamii wote duniani.

Ankal, nakuandikia hii e-mail kwa masikitiko makubwa sana juu ya customer service Tanzania nzima. Mimi naishi huku New York na nilikuja TZ na familia yangu pamoja na mashemeji zangu kuja kuwatambulisha kwa ndugu huko nyumbani na pia nilitaka hasa kuwaonyesha pia na mbuga zetu. 

Tumefika Tanzania kasheshe ilianzia uwanja wa ndege; mle uwanjani kuna watu sijuwi kama ni wa immigration ama vipi yaani wapo wanabangaiza tu cha maana wanachokifanya hakieleweki. 

Tulibabaishwa mle uwanjani mpaka tukaibiwa hivi hivi mikoba yetu wakati tunajaza makaratasi ya immigration tuliyokuwa tunajaziwa na hawa jamaa ( i think hawa ni wezi na wanakula na watu wa immigration). 

Cha kusikitisha wahusika wako pale lakini hawajali security ya watalii ama passengers. Siku iliyofuatia mimi na wife tukaenda benki kubadilisha pesa, kufika kule wale clerks badala ya kutushughulikia wakaanza kudengua tukawauliza nani anaweza kutushughulikia wanatuangalia tu, yaani hakuna hata aliyejitolea kuja mpaka nikaomba kuonana na meneja na I gave him a piece of my mind. 

Najiuliza, hivi hawa wafanyakazi wa benki wanafikiri kufanya kazi benki ndo mwisho wa dunia? Mbona bank clerks kazi zao za kijinga tu yaani kutoa na kujumlisha na kama hawana wateja kazi zao zinakuwa kushafisha madeski, zaidi ya hapa hawana lolote la kufanya. Sasa bila mteja watamfanyia nani kazi? Na watasafisha hayo madeski mpaka lini? 

Ankal, hivi viongozi wanaona kweli hivi vituko? Baada ya wiki chache tukaenda serengeti, ngorongoro, na seronera na huku tukakutana na vituko vipyaaaaaa! Kwanza tumefika kwenye lodge na kupakua mizigo yetu, badala ya wale wafanyakazi kutuongoza wapi pa kwenda wao wako bize kupiga stori za vijiweni huku wakituangalia kama vile kwa nini tumeenda pale. 

Baada ya kuwauliza vyumba vipo wapi wao wanatuambia nendeni tu huko nyuma mtaona milango iko wazi, hivi kweli is this customer service? Na kila unapoangalia mechi za Man Utd kila kukicha utaona mabango ya matangazo ya "visit-tanzania.co.tz" sasa tunatangaza nini wakati our tourism board is bogus, yaani ile board yote needs a complete overhaul. baada ya vituko vyote hivi, tukaenda pumzika bar na kuwuliza wahusika muda gani watu wanaenda mbugani. 

Receptionist hajuwi chochote na anajibu kwa kejeli kana kwamba tunamsumbua yaani dharau nje nje wakati people are there to spend the dollars the country so needs. Wakati tukiwa tunakunywa na kuomba tuongezewe wahudumu wakawa bize kuangalia mechi za ulaya, tunawaita wao wanaangaliana tu kuashiria kuwa mpira ni mtazmu zaidi ya kazi zao wanazozifanya pale (kuhudumia watu). 

Yaani kwa kweli TZ iko pathetic when it comes to customer service. Nimeshangaa mfanyakazi wa benki anaringa wakati kazi aifanyayo si ya maana? Yaani mpaka wahudumu wa mbugani wanakuwa na dharau kiasi hiki? Akal, tutafika kweli uko tuendako? 

kenya is no where near TZ kwa mbuga nzuri lakini wako way advanced than us katik utalii na ukienda mbugani kwao you feel the excitement jinsi unavyoshupaliwa as a tourist ila tanzania unachukiwa wakati unapeleka pesa za kigeni nchini. What the hell is lacking here? is it ubaguzi ama ujinga?

Mdau wa New York.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 88 mpaka sasa

  1. Hizi ni nyakati za kizazi MFU (Dead Generation) kwa Tanzania. Pole sana ndg yangu na jamaa zako. mbaya zaidi hakuna anayejali. kila mtu lwake ni Mungu tu kwa ajili ya wote.

    ReplyDelete
  2. pole sana kaka ila nataka nikwambie hivi wewe lazima utakuwa unamakosa kwa namna moja au nyingine. Unajua nizungumzie sisi watanzania tatizo letu tukisha kaa sana nje ya nchi tunaporudi nyumbani huwa tunarudi na dharau,mbwembwe na kuona watanieleza nini wabongo sasa huyo bwana ndio hicho alichokifanya karudi na nyodo kajiona yeye kaelevuka approach yako ni mbaya towards others even a cleaner , sasa unategemea watakusaidia kweli? Pale airport wote unaowaona pale ni watumishi wa serikali kuna uhamiaji,usalama wa taifa na watu wa kupambana na madawa ya kulevya sio kama unavodai ni watu wapowapo tu, hata wale potters wanauniform sasa swali utaibiwaje wewe kwanza mlikuwa wengi? Next time ukienda nyumbani nenda na heshima usiende kichogichogi ukawaletea watu madharau wabongo kudharauliwa hawataki!Kwanza jirekebishe wewe alafu rekebisha wale waliokuwa kule sababu wewe lazima utakkuwa unamatatizo alafu jifunze kurudi nyumbani atleast once a year uwe unazoea mazingira maana inavoonekana ujakanyaga bongo miaka mingi.

    ReplyDelete
  3. Ankal,nadhani huyu mlalamikaji ndio walewale kushusha suruali matakoni..malalamiko yake ni ya msingi tatizo ni jinsi anavyowakilisha hayo malalamiko inaonyesha ni mtu wa tabia za majivuno ya kitoto..sijui ana maana gani kudai wenzanke wa kazi za kijinga na bado anataka apatiwe huduma na hao anaodai wana kazi za kijinga..sijui yeye huko Ughaibuni alikokimbilia kazi gani ya maana aliyokuwa nayo..? Sijui na hiyo Dollars kiasi gani anachojivunia mpaka yeye kujiona ni bora kuliko hata hao watalii wa ukweli..? Kwa kifupi sidhani kama ndivyo mtu mwerevu anavyopaswa kukosoa au kutoa maoni katika nchi yake ya asili au nyumbani pale panapokuwa na makosa..

    ReplyDelete
  4. pole sana tabia hiyo ipo.ila nina waswasi na tabia yako pia haiwezekani toka airport,benki,mbugani unafanyiwa nyodo tu wakati watu ni tofauti kuna watu pia wakikaa ulaya basi nyodo kwenda mbele nakudharau wengine,dawa ya mwenye nyodo ni kua na nyodo zaidi yake

    ReplyDelete
  5. KAKA POLE SANA KWA YALIYOKUKUTA,ESPEACIALLY SISI TULIOZOEA MAISHA YA ULAYA KWENDA NYUMBANI INAKUWA KAZI,HAPA ULAYA TUMEZOEA UKIINGIA BANK UNAPOKELEWA HATA KAMA HUNA DOLLAR 100,SASA HUKO NYUMBANI HUWA SIJUI WANAWAZA NINI???WATU WANADHARAU,WEZI KILA KONA,POSTA,AIRPORT...OHHH HATA SIWEZI KUHESABU,POLE SANA NDUGU YANGU

    ReplyDelete
  6. Mdau wa NEW YORK haya ni MARADHI MAKUBWA NCHINI TANZNIA!.

    1.Wafanyakazi wa Benki na familia zao wananyodo na wanaringa sana utafikiri hakuna Kutsaafu ,kufukuzwa kazi au Kufa!

    2.Unaweza kwenda Benki ukakuta Teller mmoja ameweka kibao ''CLOSED''' likini yupo ndani anajibu meseji za simu na kuongea na simu yake!

    3.Ndio maana unakuta watu wasiokuwa rasmi ndani ya uwanja wa ndege wanaruhusiwa kwa mazingira ya wizi na rushwa tu!.

    SULUHISHO NI ''FREE MOVEMENT OF LABOR'' KTK JUMUIA YA AFRIKA YA MASHARIKI(EAC), MILANGO IKIWA WAZI TUTASHINDANA NA KUBWAGWA VIKALI NA KENYA,RWANDA,UGANDA NA BAADAE SOTHERN SUDAN WAPO VIZURI SAAANA HAWA!

    NI VILE SERIKALI YA TZ INABANA HILI KWA VILE INAJUA WATU WAKE NI WAJINGA NA WAVIVU!

    HAYA NI MADHARA YA MARADHI YA UNDUGU UNDUGU NA USHIKAJI USHIKAJI!

    DAIMA TUTAKUWA WA MWISHO!

    ReplyDelete
  7. Poleni sana kwa yaliyowakuta,Nchi ya Tz haitaendelea kama watu hawatabadilika labia,Yote hiyo ni elimu duni na ushamba umewazidi baadhi ya wafanyakazi,sababu hawajui kuwa mteja ni mfalme,bila ya pesa za wateja basi wao hawatakuwa na kazi!Lakini kwa ujinga waliokuwa nao hawaelewi hilo.Yote hiyo ni njaa,ujinga na dharau waliyokuwa nao!Na hapo airport ndiyo imeoza kwa rushwa na wizi!

    ReplyDelete
  8. hapa mdau wa newyork umenena kuhusu customer service kweli ni poor na hii inapelekea kwenye mahotel mengi hasa Dar es salaam utakuta wameajiri wakenya inaonyesha wakenya wapo silias na kazi kuliko sisi .mfano ukienda sheraton ya zamani sasa hivi sijui wanaiita serena amini usiamini pesonel manager ni mkenya yaani wakenya wamejaa yeye si ndio meneja uajiri ataajiri wabongo wakati kakenya wenzake nao wanashida ya kazi?ni sehemu nyingi tu wameajiri wakenya kwa nafasi ambazo watanzania wanazihitaji na wana sifa.
    yaani kwa kweli watanzania tusipobadirika!! ili shirikisho la east africa litatucost unemployement kwa watanzania itaongezeka.yaani tunauzembe sana watanzania kuhusu customer service ukienda tanesco kuomba kuunganishiwa umeme ni balaa over sio haki yako kupata umeme,ukienda hospital hasa za serikali ndio balaa yaani tunatia aibu kwa kweli vyombo vya habari vitoe mada ya kujadiliana tena kwa sauti kubwa kuhusu uzembe tulionao watanzania ..hii kitu ni mbaya sana itatugharimu sana huko tuendako.

    ReplyDelete
  9. Salaam Alaykum,

    Ankal naependa kuungana na mdau hapo juu kwa uono wake.Ni kweli tatizo lipo sehemu nyingi sana katika nchi yetu si kwenye government agencies wala kwenye private sector.ILa napenda pia kumkosoa na yeye kwa kuita kazi za mabanker haswa hao ma bank clerk kuwa kazi yao ya kijinga kwa kuwa ni kujumrisha na kutoa,Hili si sawa kabisa kwa kuwa hakuna kazi ya kijinga duniani au yeye anaona kuishi NYC na kuoa mzungu ndio kafika peponi?Alitakiwa kutoa dukuduku lake bila kudharau mtu kwa kuwa kazi yake yeye hajasema na hata angesema inamsaidia yeye na familia yake na wala haimsaidii mtu mwingine aache dharau..Ustaarabu hauuzwi dukani

    ReplyDelete
  10. ndio tujuwe umeoa mzungu au ?!
    we mwenyewe huna adabu hata chembe na inaelekea kisa umetoka marekani na umeongozana na kijike chako cha kizungu ulitaka watu wakupokee kama mungu mtu ; "eti nna dola" , hayo maeneo uliyo yataja yoote hakuna sehemu ambayo sijawahi kupatiwa huduma na huduma zao ni za kiwango cha juu , labda nikushauri - we baki huko huko na kama ukitaka kutembelea mbuga nenda huko kenya hilo tangazo ulionalo kwenye mechi za manchester lipotezee kama vipi

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana na wewe yote lakini naomba niseme ume generalise sana kuhusu sisi clerks mbaya zaidi umetudharau kwani ulifika kwenye bank ngapi na kuona hayo? Is it all about staying in New York?

    ReplyDelete
  12. Mdau ungetutajia basi benki uliyokwenda na mbuga walizokuringia ili nasie tuweze kuwazodoa kwa huduma zao mbovu, najua kwako wewe ulichukulia poa but vipi kwa shemeji zako ulikojinasibu kuwa watanzania ni wakarimu.

    Nakubaliana na wewe 110% kuwa Bongo customer service ni poor mno.

    ReplyDelete
  13. Sorry buddy, this is the way bongo goes,I think it is a mixture of jealous and envy, with some serious inferiority complex issues, don`t worry soon things will change as these useless people will be out of work!

    ReplyDelete
  14. Yaani kaka yangu no kushangaa. Tanzania ndivo ilivo kwa sasa au na hapo nyuma ilikuwa ivo sijui. Ila baada ya kukaa ulaya na kurudi nyumbani mara kwa mara ndio nikaelewa nchi yetu ilivo. Pole sana kaka, air port za daa, kia ni rushwa,wizi na usumbufu kwa kwenda mbele. Walinikera sana ikabidi nibadili passport. Sasa ivi nabita kama mzungu hao wanaowaabudu kuliko wabongo wenzao.

    ReplyDelete
  15. Nakubaliana na kaka hapo juu!! Ni kweli kwamba something needs to be done... Huoupuuzi wa cashiers humo ktk benki ni balaa, na wakati mwingine hadi mameneja wao wanakuwa hovyo tu. Na si kweli kuwa hawawi trained kuhusu huduma kwa wateja hapana, ila tu ni kwamba watu wanafikiri as long as they are paid at the end of the month, who cares!!! Mimi binafsi nilishakutwa na meeeeeengi ya namna hiyo kiasi ambacho siku hizi nikiona tu ujinga nalianzisha right away maana hata useme kwa rais hakuna kitakachobadilishwa. It's a shame kusema ukweli.

    ReplyDelete
  16. Ubaguzi will be my final answer! Tanzania ni nchi pekee ambayo raia wake wanadharau wa-Tanzania wenzao na kutahmini wageni. Hata wamarekani weusi hulalamika sana na kusema wakienda TZ hupewa huduma mbovu compared to wazungu.

    Eniwei, pole. Next time kajirushe Jamaica tu. Bongo nenda likizo kasalimie ndugu na jamaa na rudi hapa. Usiende kama mtalii.

    Hiyo ni mabaki ya Ujamaa.

    ReplyDelete
  17. huu ni ujinga tu wa kutojua!!! leo hii mtu huyo huyo anaefanya nyodo kwenye sehemu yake ya kazi ukimfukuza anaanza kilio, hawafahamu ni watu wangapi wako vijiweni wanatafuta kazi za kufanya wao wanaleta mchezo!!!!! tena kwa kawaida huwa ni hawa hawa watu wa ngazi za chini ndio huwa na huu upuuzi wa kukwamisha mambo, ukienda kwa wakubwa zao huwa wako so friendly!! Nakuunga mkono mdau Tanzania kwa suala la Customer Care ni Zero tena nyeusi. Unaenda sehemu kupata huduma utafiri anakupatia bure na wakati umempelekea pesa!!!! wonders jamani wacha tu tuwe maskini hayo ni malipo ya kazi yetu. Hakuna kitu nachukia kama kwenda sehemu kupata huduma then unafika pale wahusika wanakuangalia tu kana kwamba umejinyea haaaaaaaaaaa. I hate!!!!!!! POLE SANA MDAU.

    ReplyDelete
  18. Mtoa mada wacha nikupe pole kwa yalokusibu, ila nadhani Tanzania hatuwezi kuendelea kama tutakuwa na watu kama wewe ambae huthamini kazi za watu, bank clerks ni kazi sawa na ya kwako ya kupiga boksi, sasa unapodharau wakati watoto wanaenda chooni na wanasoma kwa kazi hio hio unakuwa hueleweki. Inaonekana hata wewe ulikuwa na dharau kwa watanzania hopefully kwa kuwa ulikuwa na mzungu ika hakuna mtanzania atakaekuwa tayari kukuramba nyayo zako kwa kuwa umeongozana na master wako.
    Pole sana ila inakubidi uaenze wewe kubadikika

    ReplyDelete
  19. Pole mdau wa New York

    Ukiwa na shida za kibenki tafadhali njoo FNB Bank na utapata huduma nzuri zinazomjali mteja.
    Tupo mjini opposite Serena Hotel( zamani Moeven Pick), Quality Center na Penisular House Coco Beach.
    Mdau wa FNB

    ReplyDelete
  20. Mdau, kwanza welcome to Bongoland, nadhani umeondoka miaka mingi na kwa vile umekuja na mke na mashemegi wa kizungu (I presume!) ndiyo ukazidi kupandisha pressure. Pole sana kwa hilo lakini hiyo ndiyo siasa yetu ya ujamaa na kujitegemea na kuondoa unyapara kwani sote ni sawa.

    Pili ingesaidia sana kama ungetutajia jina la hiyo Bank waliyokufanyia jeuri hiyo, kwani siyo benki zote zilizo hivyo, na vile vile labda wangeona aibu kama wangetajwa kwa jina (naming and shaming inasaidia sana).

    Tatu hao TANAPA ni Shirika la Serikali ndiyo maana wanafanya dharau kwani watalipwa mishahara yao hata kama hakufika mtalii hata mmoja. Hiyo ni changamoto kwa kweli. Wanataka ma allowance ya kwenda nje ya nchi kuhamasisha utalii na kumbe hawawezi hata kupokea wageni wachache wanaofika nchini kwa hiari yao.

    Mheshimiwa Waziri wa Utalii umesikia hiyo? ZUIA ZILE ALLOWANCES ZAO ZA MASAFARI HAWA JAMAA HAWAWEZI KUHUDUMIA WATALII WALIOKO NCHINI.

    Na hayo matv sehemu za kutoa service kwa nini zinaruhusiwa??????? Mengine huwa tunayataka wenyewe.

    ReplyDelete
  21. pole sana mjomba .. mm nakuunga mkono kabisa mimi nilishatembelea hizo mbuga sana lakini niliyoyaona si mazuri yaani wameridhika wanawaza tip tu hao wahudumu mbongo ukishuka na begi lako wanakuangalia kama nyanya chungu tu .. mm naona ni ubaguzi na pia kukosekana kwa nidhamu ya kazi (non professional)

    ReplyDelete
  22. Ndugu umesema kweli, watanzania inabidi tubaidilike, halafu tunalalamika wakenya wanautangaza waomlima Kilimanjaro na wanapata watalii wengi, mara wanakuja nchini na wanaajiriwa .Tuache fikra za kijinga. Sijui kama hawa wenye mahoteli wanajua hilo.Watu wa airport waache tabia zao mbaya ni kujiletea umaskini, wengine wanaanza kuomba pipi na chokolate au wanasubiri chenji.Hii ni dhana ya uvivu na tamaa.

    ReplyDelete
  23. michuzi acha kubania comments zangu , ziachia watu wazisome

    ReplyDelete
  24. POLE MDAU. LAkini mdau hii ni inatokea na inasababishwa na vitu mbalimbali. Unapona mambo kama hayo usidhani wakubwa wao hawajui...wanajua ila....kachomekwa tu. Mtu huyo huyo kama akifukuzwa kazi atakuambia maisha magumu. Tuangalie vipi wenzetu wanathamini kazi kiasi wawembele kwakila kitu mpaka kwenye maasi.

    ReplyDelete
  25. Mleta malalamiko, haya uliyoandika kwanye ujumbe wako sikubaliani nayo hata kidogo. Ndiyo watanzania wengi ni wazembe lakini si kwa kiasi hiki kama ulivyoelezea. Kwanza ukiingia uwanja wa ndege kabla ya kupita immigration desk hakuna mtu mwingine eyote zaidi ya abiria anayezurura hapo bila uniform. Pili forms za immigration ni rahisi sana kujaza, nyie shule yenu mliacha USA mpaka mtafute mtu wa kuwajazia?!! Hapa inaonyesha jinsi gani na nyie mlivyokuwa wazembe na wavivu wa kutumia akili zenu. Tanzania tupo nyuma kwenye huduma kwa wateja lakini si kama hivi unavyoelezea, hakuna bank utakayoingia tellers wasikusikilize. Acha uongo kama ni kweli kwa nini hutoi jina la hiyo bank na lodge mliyofikia mkienda mbugani? Acha hizo

    ReplyDelete
  26. Hapa UK ni hivyo hivyo wao ujanja wao kabla hawajachukua pesa yako. Watakupa maneno mazuri kabla hujalipa ukilipa tu they don't want to know you.

    ReplyDelete
  27. Pole sana ndugu yangu,yaelekea hukutaka kufanya booking kwenye kampuni ya tours, good kwasababu ni ghali.Hawo watu wa mahoteli kwa kweli hawajui lolote kuhusu pori wala low season na high season.Mimi ni guide na nime kaa serengeti,ngorox2,tarangire na manyara zaidi ya miaka saba nimeyaona hayo kwa wageni waliokuwa private kama wewe.next time kama utakwenda Pori jaribu kuwa na self indipendent tour guide wanauzoefu wakutosha kwa private clients.
    pia unaweza wasiliana nami kwa; confideus@yahoo.com (arusha).

    ReplyDelete
  28. Mdau ulitaka nani akunyooshee mambo? wewe umekaa ughaibuni unategemea nani ataijenga hii nchi yetu Tanzania kwa mafanikio kama sio wewe? Rudi utengeneze nchi yako sio kulaumu tu!

    ReplyDelete
  29. WEWE MPUUZI NINI!!!!!!!!! acha kututukana sisi wafanyakazi wa benki naona umelewa na kuishi huko ulaya! Airport sote tunapita mbona hayo unayosema hatuyaoni,kuna ulinzi wakutosha airport hamna mtu anayeigia bila kibali.Naona umechanganyikiwa na hao wazee unaowanawisha huko.

    ReplyDelete
  30. I am pissed off with this guy insinuation. Everything he said is mere fabrications. Please be really

    ReplyDelete
  31. Mi ninaishi UK pia, na nilikuja TZ yaani nilichoka na Customer service, yaani km vile unawabembeleza watu wakuhudumie. Nilienda CRDB bank, nilichoka, yaani hata smile hakuna mpaka nikahisi labda nimemuudhi mtu au sijui niongee vp. Mimi ndo ilibd nismile at least ili kuwe na good atmosphere. Nikaenda kulipa maji pale Morocco hao wadada walivyoniona naingia kwanza walinishusha juu mpaka chini halafu baadae baada ya kujivuta ktk kunihudumia, nikaambiwa nikachukue print mwenyewe aliyoiprint for me. I thought what the heck. Hivi wanapata training ya kazi za kuhudumia wateja hawa???
    Jamani smile gives longer life and makes you happier

    ReplyDelete
  32. Pole sana mdau. Mimi nadhani kuna laana fulani Tanzania, na mimi huwa naumia saana tu. Yaani kwa kweli customee care kwetu ni zero kabisa, tena mahali kote. Unaingia dukani muhusika anakuangalia tu kama kinyesi, kwa ufupi unabembeleza huduma unayoilipia. Hospitali ndo usiseme. Halafu eti tunasema wageni wanachukua kazi zetu. Mimi nadhani acha wazichukue tena kwa wingi, pengine tutatia akili.

    ReplyDelete
  33. Inaonekana mwandishi wa hii habari sio mtu wa busara. Yaani kuondoka Tz na kuishi U.S ndio kama vile amesahau jinsi biashara au castomer service ilivyo. Hayo ambo anayolalamika ni ya kweli, ila na yeye mwenyewe inaonekana ana dharau fulani, labda ndio maana walikuwa wanamdengulia.
    Sio kwasababu umetoka Marekani na mke/wakwe wamerekani eti ndio mambo yabadilike. Lakini unaweza kuongea na watu vizuri ili uwafahamishe kwamba wanaweza kufanya huduma vizuri zaidi ya wanavyofanya, sio kuwadharau.

    ReplyDelete
  34. Ndugu yangu pole sana, lakini JIA mbona utaratibu uko wazi kabisa, na hakuna urasimu wowote kama viwanja vya ndege vya USA.nahisi umeishi sana nje! na una kasumba za kubabaikiwa kwa kuwa uko na wageni.
    nafikiri next time tafuta kampuni nzuri ya kitalii na wataarange vizuri safari ya mbugani, ila ukichukua kampuni za bei bei rahisi lazima ukutane na hayo. Pia acha kasumba!

    ReplyDelete
  35. Mdau wa NY,

    Ameeeeeeeen to that, what more to add?

    Waziri yupo, Watendaji wapo, kazi kufurahia kuripoti shilingi mbili mbili zinazoongekeza kana kwamba UOZO UNAOENDELEA HAUKULIKANI

    ReplyDelete
  36. pole sana kaka, thats why we are still behind, Si wewe tu kila wadau wanaotoka nje kuja salimia wanasumbuliwa sana kisa unatoka ulaya... TUJIPANGE JAMANI EEH....

    ReplyDelete
  37. Mdau wa New York (NY), hiyo ndio nchi yetu na hizo ndizo changamoto ingawaje nyingi ni za kujitakia(kama hii). Nikupe pole sana kwa yaliyokukuta. Langu ni hili, ni kweli hili ni tatizo na una haki ya kujieleza ila ktk maoni yako uliteleza kijisehemu cha lugha na hivyo ufikishaji wa ujumbe (ladba niseme kwa sababu ya usumbufu ulioupata)hasa pale uliposema bank clerks kazi zao ni za kijinga!! Hili linaibua maswali, moja na la haraka haraka likiwa ala hivi mdau wa NY alikwenda kupata huduma ya kijinga kwa mfanyakazi wa kijinga (bank clerk)!!. Ni mengi lakini niishie hapo tu kwa kusema naungana na wewe kuzisema kero tunazokumbana nazo. Italeta maana kama tutaepuka kutumia lugha itakayotufanya tuonekane nasi tuna matatizo hata kama si yanayoangukia katika kundi la customer service/care. Nikupe pole tena.

    ReplyDelete
  38. Mdau inaelekea umeondoka miaka mingi sana na ulikuwa huna tabia ya kwenda na kutembelea nchi yako mpaka umesahau tabia na desturi zetu.

    However!!!Pengine ulishuka na manjonjo mengi labda ndio maana wakakudharau.Kwani viza mpaka msaidiwe kuijaza hamuwezi kujaza wenyewe?

    Mbona sisi wabeba box wengine tunakwenda kila mwaka na mambo hayatutokei kama unavozungumzia?Pamoja na kwamba customer service sio ya kuridhisha lakini unavozungumzia hayo ni kama kejeli kwa upande mwengine.

    Au ulivoshuka na shemeji zetu ukadhani watatetemekewa kama zamani tukiona wazungu tunawaona kama mungu(stakafirullah)
    Ni simpo tu mbona ukishuka na ndege unaingia ndani na kujaza form yako ya visa halafu unawakabidhi customs dirishani na usubiri kuitwa mambo yamalizike.Ukimaliziwa prosess yako basi unapita na kuchukua mizigo yako na kusachiwa kidogo tayari umetoka nje.

    Usitukane hivo ndugu zetu bwana sio wabaya kiasi hicho unavowazungumzia.Usisahau kwenu bwana home sweet home.

    ReplyDelete
  39. Mdau pole sana,hawa watu sio bank tu au mbugani ni sehemu nyingi sana,nyumbani wanajali mtu wanaemjuwa au awe mzungu.Umeuliza swali,kuwa huwo ni ubaguzi au ujinga,,nakujibu!Huwo ni ubaguzi wa kijinga kwani wao ni wapumbavu kupindukia,wanambagua mtu mwenye rangi yao,,na kumshobokea wa rangi nyingine,na kuhusu ujinga ni wajinga mnno mno,kwani hawajui hicho kibarua cha hapo bank kikiisha na yeye hana tena mshahara,kwani bank mtu unaweka pesa yako mwenyewe wala hununui kitu,,hiyo tabia walikuwa nayo haswa bank ya posta lakini watu walivyolalamika sana wakajirekebisha kidogo,,,Hiyo habari yako ingetakiwa ifike katika vyombo vya habari ambavyo watu wengi wanaangalia ili ujumbe usambae maana hii tabia kwa Tanzania imepita kipimo,,hapo Airport wamejaa wezi wanaruhusiwa kuingia ndani na kuwababaisha wageni,,,mimi ilitokea mume wa rafiki wangu wakamnyanganya pass yake eti awaambie kaipataje,,tulivyoona hivyo haraka rafiki yangu akaingia ndani kwa kuwa alikuwa na cheo kidogo kuruhusiwa,kuingia,,ndo akamuhoji huyo kijana kwa nini amnyanganyaa pass yake,,akaomba samahani ,,,ho ho nilikuwa namuuliza tu!yaani ni maajabu na wanatia aibu sana,,serikali iangalie hili jambo kwa makini ama sivyo TZ itapoteza watalii wengi kwa tamaa za wafanya kazi,,na wenye ujinga kama huu wa kupindukia.Wageni wakitoka huko wanasimliana habari kama hizo,,mtu anasema sirudi tena
    Ahlam,,,UK

    ReplyDelete
  40. Bongo badoooo!!! Huduma kwa wateja ni non-existent. Tuna safari ndefu sana kuweza kufikisha huduma inayotolewa kwa wateja iweze fika walao kama majirani zetu Kenya. Viongozi wetu hawatoi huduma kwa wanaowaongoza sembuse hao ma-clerk wa benki, ama wa pale kiwanja cha ndege. Tunahitaji viongozi vichaa wanaoweza fanya maamuzi magumu. Fukuza kazi hawa wote wanaoringa ringa, kuna watanzania wengi sana wanatafuta ajira, bora hao wachache watakaobahatika kua na ajira wawe watu wenye mapenzi na kuheshimu kazi zao.

    ReplyDelete
  41. Huyu bwana ndiye mjinga. Ukiudhiwa na mtu ama baadhi ya watu si busara kutukana kila mtu. Mie binafsi naishi New York na majuzi nimetoka nyumbani; sijapata adha kama ya huyu bwana, lakini siwezi kusema hayakumsibu. Hata hivyo niujinga mkubwa kwa upande wake kwa sababu ya hayo aliyoyakuta benki kuwatukana mabenk clerks wote! Hata huku tuishipo zipo adha nyingi tu! Tusijifanye hatuyaoni ama kuwadanganya wengine.

    ReplyDelete
  42. You should drink some cement to toughen up, didn't you know the reall situation in Bongo? How long have you been living in NY. Man up mate!!!

    ReplyDelete
  43. Mdau kutoka New York, kwanza nafurahi, kama mmojawapo wa wapenda maendeleo wa nchi yangu, kwa ww kuelezea challlengses ulizokumbana nazo/constructive comments kwa ajili ya kuboresha huduma/customer care katika maeneo mbalimbali uliyoyataja hapo (airports, kwenye mahoteli, mbuga za wanyama - kwa ujumla sehemu zote zinazo-deal moja kwa moja na utalii)- kwa ajili ya maendeleo ya tourism industry in tanzania.

    Pamoja na hayo, naanza kupata shaka na maelezo yako, kuwa katika vacation yako Tanzania, hakuna hata sehemu hata moja ambayo walikuhudumia vizuri (customer care ilikuwa vizuri)- kitu ambacho siamini. Hapa picha ninayoipata, ni kuwa inawezekana na ww pia utakuwa na matatizo ndo maana kila sehemu uliyokwenda umekumbana na mikasa, kwa kuwa, inavyoonekana na ww mwenyewe ni mtu wa mikasa !

    Vilevile, picha nayoendelea kuipata, ww aina ya watu wakiwa na hela mnataka muabudiwe. Mfano: ukienda baa, yule muhudumu, huwezi ukamuita/ukamuuliza kwa ustarabu – utaauliza kwa kejeli na dharau! Or unaweza ukamuita ’’ We Mal**ya hebu niletee bia baridi hujui kama nalipa kwa US Dollar?’’’!! au ‘’ww muhudumu hujui kama mm natoka NY – njoo unihudumie, alaa’’ - sasa kwa style hii unategemea nani akuhushimu!! Hii kitu nime-experince kutoka kwa jamaa zangu ambao wanatoka ng’ambo na wanakuja bongo kwa vacation – some of them wamekuwa na vitabia vya namna hii. – Heshimu uheshimiwe!

    Pia, nimeiona tu, ww ni mmoja wa watu wenye dharau na kejeli – kifupi ww mwenyew sio muugwana, hata ukiangalia katika baadhi ya maelezo yako, unakashifu kazi za watu kuwa ‘’….. Bank clerks ni kazi za kijinga…’’, na mara ‘’…receptionists hawajui lolote…’’ !! – unaweza kutoa maani yako na yakawafikia wahusika vizuri bila kutumia lugha za dharau. WAugwana ndo tunafanya hivyo!

    Mm mwenyewe nakaaa ng’ambo na mara kwa mara huwa naenda bongo, offcourse, huwa nakumbana na vituko vya hapa na pale ambavyo vina-bore na kutatisha tamaa – lakin pia kuna sehemu ambazo wameanza kufanya vizuri. Ujumbe utakuwa umewafikia walengwa, ila na ww pia, unatakiwa ujiangalie na kauli zako zinawezakana pia ikawa wewe ni chanzo cha hayo yote.

    Hayo ni mawazao yangu tu, na wote tupo katika kuboresha na kujenga!

    ReplyDelete
  44. Spot on. I had same experience five years ago.

    ReplyDelete
  45. Mdau kutoka New York, kwanza nafurahi, kama mmojawapo wa wapenda maendeleo wa nchi yangu, kwa ww kuelezea challlengses ulizokumbana nazo/constructive comments kwa ajili ya kuboresha huduma/customer care katika maeneo mbalimbali uliyoyataja hapo (airports, kwenye mahoteli, mbuga za wanyama - kwa ujumla sehemu zote zinazo-deal moja kwa moja na utalii)- kwa ajili ya maendeleo ya tourism industry in tanzania.
    Pamoja na hayo, naanza kupata shaka na maelezo yako, kuwa katika vacation yako Tanzania, hakuna hata sehemu hata moja ambayo walikuhudumia vizuri (customer care ilikuwa vizuri)- kitu ambacho siamini. Hapa picha ninayoipata, ni kuwa inawezekana na ww pia utakuwa na matatizo ndo maana kila sehemu uliyokwenda umekumbana na mikasa, kwa kuwa, inavyoonekana na ww mwenyewe ni mtu wa mikasa !
    Vilevile, picha nayoendelea kuipata, ww aina ya watu wakiwa na hela mnataka muabudiwe. Mfano: ukienda baa, yule muhudumu, huwezi ukamuita/ukamuuliza kwa ustarabu – utaauliza kwa kejeli na dharau! Or unaweza ukamuita ’’ We Mal**ya hebu niletee bia baridi hujui kama nalipa kwa US Dollar?’’’!! au ‘’ww muhudumu hujui kama mm natoka NY – njoo unihudumie, alaa’’ - sasa kwa style hii unategemea nani akuhushimu!! Hii kitu nime-experince kutoka kwa jamaa zangu ambao wanatoka ng’ambo na wanakuja bongo kwa vacation – some of them wamekuwa na vitabia vya namna hii. – Heshimu uheshimiwe!
    Pia, nimeiona tu, ww ni mmoja wa watu wenye dharau na kejeli – kifupi ww mwenyew sio muugwana, hata ukiangalia katika baadhi ya maelezo yako, unakashifu kazi za watu kuwa ‘’….. Bank clerks ni kazi za kijinga…’’, na mara ‘’…receptionists hawajui lolote…’’ !! – unaweza kutoa maani yako na yakawafikia wahusika vizuri bila kutumia lugha za dharau. WAugwana ndo tunafanya hivyo!
    Mm mwenyewe nakaaa ng’ambo na mara kwa mara huwa naenda bongo, offcourse huwa nakumbana na vituko vya hapa na pale ambavyo vina-bore na kutatisha tamaa – lakin pia kuna sehemu ambazo wameanza kufanya vizuri. Ujumbe utakuwa umewafikia walengwa, ila na ww pia, unatakiwa ujiangalie na kauli zako zinawezakana pia ikawa wewe ni chanzo cha hayo yote.
    Hayo ni mawazao yangu tu, na wote tupo katika kuboresha na kujenga!

    ReplyDelete
  46. hawajali tips, kama ndio hivyo usitoe sent tano nyekundu ya tip. Wajinga hao!

    ReplyDelete
  47. Ni kweli custumer service hapa kwetu ni tatizo. Ila kutokana na maelezo yako,na wewe unaonekana ulikuwa na matatizo, inawezekanaje uone kazi ya mwenzio sio ya maana? kuishi Marekani sio lazima ukija Tanzania kila mtu ajue. Tujifunze kuwathamini wenzetu bila kujali nafasi au kazi zao,kila mmoja ana umuhimu kwenye kazi yake ndugu yangu.

    ReplyDelete
  48. Ni kweli kabisaa.
    Mimi leo yamenikuta pale Azikiwe CRDB AZIKIWE Branch leo 28/12/2011. Kwenye information Desk kuna dada mmoja amepaka lipstick kali mdomoni anadharau hakuna mfano.
    Nimepoteza ATM card yangu sasa kwenda pale ili nipewe nyingine, akaniambia inabidi nilete polisi report, kumbe unapoenda kuchujua
    polisi report unabidi uende na barua toka bank ya utambulisho, sasa yeye hakunipa hiyo barua, baada ya kwenda polisi na kugonga mwamba
    nikarudi, nikamkuta nikamuuliza kwanini hakunipa hiyo barua ya utambulisho wakati anajua inahitajika, alinijibu kwa dharau
    eti sikuonyesha interest ya kwenda polisi kuchukua barua. Dharau zake zilinisababishia usumbufu mkubwa na mpaka mambo yangu mengi ya kazi yamelala.

    ReplyDelete
  49. Kaka acha ushamba na kuwa kibaraka wa wazungu. Ina maana hukukutana na zuri hata moja la TZ??? Mbona sisi tukienda nyumbani TZ tunaona kuna mabadiliko?? au mwenzetu hukuona changes hata moja?????? Au kwa kuwa umeolewa New York????

    ReplyDelete
  50. Mdau wa Newyork unaweza kututajia ni benki gani na ni lodge gani ulitembelea na kukutana na hizo huduma duni kwa wateja? Najua tunayo matatizo kwenye hilo eneo lakini hii hadithi yako naona kama imetiwa chumvi vile???

    ReplyDelete
  51. Pole kaka.ila hiyo ndio Bongo,inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  52. Tanzania hatuwezi customer service na wala hatukubali kuwa hatuwezi. Mifano ya kuigwa tunayo hapo jirani Kenya lakini bado tunashindwa kujifunza toka kwa jirani zetu.

    ReplyDelete
  53. Mdau wa New York,,,hii ndio Bongo Jambaland!, Jamba Republic!, Jamba Federation!

    Ukarimu wa huduma hakuna kabisa!, Akili kichwani.

    Kisu chako ndio mkombozi wako,hatuna AKAUNTI ZA BENKI, kama zipo HAZINA KITU KABISA!!! hatutumii CREDIT CARDS (kadi za mikopo) ,tunatumia (hela mkononi)CASH ON HAND!

    ReplyDelete
  54. Pole ndugu yangu. Kwa wewe uliyezoea maisha ya wenzetu huku ulaya ambako kazi yoyote huheshimiwa kwa asilimia 150%, kila utakachokiona huko utapata dosari tu. Sioni kama utakiona chochote kizuri kama siyo chakula kilichopikwa kinyumbani na kuwa hujakila kwa muda mrefu. lakini nimeona nichangie jambo moja kati ya uliyoyagusia; Customer care. Utamaduni wa customer care, kwa kiasi kikubwa siyo wetu/waafrica. Tuna kitu heshima, kwamba kiasili tunawaheshimu wageni, watu wazima na walio na madaraka ou nafasi Fulani katika jamii. Lakini hii nayo siku hizi inaanza kuisha kwa kushinikizwa na wenye ukwasi; mpaka msimamizi awapo; kama kuna maslahi nk. Sasa kuliua hili ni lazima kuwepo na nguvu kubwa mbili katika jamii. Moja ni soko la ushindani (kwamba kama hutoi huduma unaachwa kwenye biashara) na mkakati au mfumo wa serikali kushinikiza hali hii iwepo. Nilisemee hili la serikali kushinikiza (mfumo). Haitoshi kwa serikali kuendelea kusema utalii (mfano) ni nguzo moja wapo kwa uchumi wanchi wakati misingi yake kaitiliwi mkazo au hata kuingizwa katika mitaala ya elimu. Naweza kusema kitu kimoja tu, kwamba. Kama ingekuwepo nia, au mimi ningekuwa na maamuzi ningeunda mitaala kulingana na maeneo. (kanda ya kaskazini Arusha, Kilimanjaro na Mara), somo kuhusu utalii, kusindikiza watalii, kuhudumia watalii, kutunza mazingira, utamaduni wa asili nk nk. yangeanza kufundishwa kuanzia shule ya msingi na kukaziwa sekondari. Kama mtoto kwa miaka karibu kumi anaelezwa umuhimu wa utalii kila siku, anapomaliza shule, na atakapokuwa katika mazingira yake atachangia katika kufanikisha utalii kwa njia moja au nyingine. Baada ya miaka miongo kadhaa, kanda nzima itakuwa inazungumza lugha na kuwa na tabia moja. Nenda ushelisheli, angalia miji inayotegemea kitu fulani katika uchumi wake. Elimu na makuzi kwa watu wake huelekezwa huko. Sisi, bado tunatoa general education. Sidhani kama tunaweza kubadilika. Tujadili.

    ReplyDelete
  55. Mdau wa NY Bongo unatoka Kijijini ktk msimu wa mazao unarudi na Gunia lako LIMEJAA MINOTI lakini lina vumbi jekundu!!!...Unaingia Benki TELLER anakwambia wewe Babu wa Shamba Gunia lako weka hukooo pembeni, kungúta vumbi halafu ndio uje hapa Dirishani!...EBO!

    BENKI ZA USWISI HUKO KWENYE WANAO ZIJUA FEDHA UKIINGIA KAMA KIBABU HICHO UTAPOKELEWA KAMA NABII!!!

    HII NDIO UKISIKIA MTEJA NI FALA NA MTWANA NA SIO MFALME NDIO HAPA BONGO!!!!!!

    ReplyDelete
  56. You are a braggart, a sook and - worst of all you live in NY. For gawd's sake grow up. We know u did tough without your make-up kit and food massager. You are the most metrosexual Tanzanian ever eparoted to USA.

    ReplyDelete
  57. Watanzania wenzangu mnaokataa ama kupinga experience ya huyu ndugu yetu naona ni nyinyi ndiyo mlio na matatizo kwani hamtaki kubadirika na kuambiwa ukweli. Mtu lazima useme ukwelii na aliyoyasema huyu jamaa mbona yana exist Tanzania? I go to TZ kila mwaka na pale uwanja wa ndege kweli hawa shadow workers mbona wapo? Tena ukitua tu pale utawaona wanakuja kukuuliza kama unataka visa. Pengine jamaa alitaka asaidiwe baadhi ya vitu katika kujaza hiyo visa, ila ki ukweli hawa watu wapo uwanja a ndege na wala hawana uniforms. I saw them with my own eyes, sasa wadau mnakataa nini hapa? Na kama watakuwa pale bila viongozi kujuwa basi watakuwa wanakula na baadhi ya wafanyakazi wa immigration. Benki nyingi TZ clerks wako hivyo hivyo, wameweka dharau mbele badala ya customer care. TZ huna haja ya kudharau benki clerks, wao ndiyo wanakudharau wewe yaani ukiingia tu kwenye baadhi ya benki wafanyakazi wanakutazama toka chini mapaka juu na kunyanyua midomo yao as if they are above the law. Mi nafikiri hili husababishwa na kupachika watoto wa mjomba ama mashangingi wao makazini when they are NOT qualified. In general, aliyoyasema huyu mdau do exist and I think wa TZ wengi makazini aren't qualified due to kupachikwa maofisini na vigogo.

    ReplyDelete
  58. Mdau wa NY, nakubaliana na wewe kabisa. Huduma za wateja kwenye nchi yetu inasikitisha sana. Kuna wadau wametoa comment huku kwa jamaa kaondoka lini Bongo mpaka aone hivi ni vitu vipya!!! Inasikitisha kusoma comments za namna hiyo....ina maana hatutaki kubadilika. Kama huduma ikiwa mbovu ndio haitakiwi kurekebishwa!!?? Muungano wa Afrika Mashariki tumepiga kelele kwamba wenzetu Kenya wako mbele sana na sisi hatujajiandaa, sasa tutajiandaa lini kama hatutaki kurekebisha vitu vidogo kama huduma za wateja!! Mimi nimeshuhudia uduni wa huduma hizi mwaka jana CRDB, kuna dada alikuwa ananihudumia kwa kiburi na amenuna utadhani nilikuwa nachukua hela kwenye account yake!! Airport kuna matapeli ndani na viongozi wa Immigration wanalifahamu hilo. Mbaya zaidi ni kwamba matapeli hao wamevaa uniform na beji kama wafanyakazi wengine. Nilishuhudia hiyo baada ya kutapeliwa mwaka jana na kurudi Airport kumwulizia mtu aliyekuwa akinihudumia na ambaye ndie alinitapeli nikaambiwa hafanyi kazi hapo na huwa anaonekana mara kwa mara! Nilibonyezwa baadaye kwamba watu wa namna wapo hapo Airport, ambao wanatoa asilimia fulani wanazotapeli kwa viongozi na wafanyakazi pale Airport!!!
    Huduma za nchi yetu kweli ni mbovu na pia ni kweli wengi wa watoa huduma hizo kwa mtazamo wangu naona kama hawazithamini kazi zao au hawazifurahii. Kwa nini mfanyakazi ukae unatazama TV wakati wa kutoa huduma. Kama hicho kipindi cha TV ni muhimu zadi chukua day off ukae nyumbani na uachie wanaotaka kufanya kazi wafanye. Huduma ya hiyo hoteli uliyoenda mdau wa NY kweli ilikuwa mbovu. Penye huduma nzuri muhudumu atakuwa anapita mara kwa mara kwenye meza ya mteja kuangalia kama anahitaji huduma na sio mteja kupiga kelele za kumuita muhudumu! Tubadilike tu katika huduma za wateja la sivyo tutaendelea kupiga kelele za hakuna kazi na uchumi mbovu huku sisi wenyewe tukiwa tunazifukuza hizo kazi!!!! Kwenye ofisi za mawizara ndio kumeoza zaidi wala nisiendelee.

    ReplyDelete
  59. WAZUNGU WANATOA TIP, WATANZANIA HAMTOI TIP YOTOTE NDIO MAANA MKIENDA KWENYE UTALII MNADHARAULIWA!!!MIMI NILIPELEKA RAFIKI WAZUNGU WATU WA MBUGANI WALIPONIONA NAAMBATANA NAO WAKAJUA GEMU IMEVUMBA!!! KUHUSU BENKI SINA COMMENT...

    ReplyDelete
  60. JAMANI MIMI MTOTO WA WAZIRI, YANI HAPA MSHUA ANASOMA COMMENTS ZENU ANACHEKA TUU ANASEMA HAWA JAMAA WATALALAMIKA SANA.....SIO KAZI YA WAZIRI KUWAFUNDISHA KAZI WAFANYAKAZI NI KAZI YA WAZAZI WAKE

    ANASEMA MBONA HATA POSTA BARUA/MIZIGO INAIBIWA NA KUPOTEA?HIYO SIO KAZI YA WAZIRI KUWAFUNDISHA WAFANYAKAZI KUACHA WIZI NI KAZI YA WAZAZI JAMANI

    ACHA MIMI NAWASHAURI WATANZANIA WOOTE WALIO NCHI ZA NJE KUTUMIA KAMPUNI ZA KIGENI KAMA DHL AU FEDEX KUTUMA MIZIGO KWANI WAZUNGU WAKISHAKUWA NA HELA NYINGI NA SISI MISAADA ITAONGEZEKA

    MTOTO WA WAZIRI.

    ReplyDelete
  61. msiikatae jamani, ni kweli haya mambo yapo. mimi naishi tz lkn nilisafiri kwenda USA kutembea niliporudi nikiwa katika ndege kuna wazungu wakawa wanasema hii airport ni worst. jamani ni kweli wizi upo, mi sikuibiwa ila kuna mtu alinionya niangalie mizigo kwani kuna wizi siku hz. pia watu wanaomba sana hela pale airport na mizengwe ni mingi mno. ila ndio hivyo tena. na ni mwaka jana sio zamani wala nn

    ReplyDelete
  62. Safi sana watu wa Airport Bongo tena ilibidi muwarukishe kichura hao wazungu na kibaraka wake huyo. Kwani hata wao (Wazungu wanatunyanyasa sana huku Ughaibuni) Ukipita Amsterdam Airport kama wewe ni Mswahili utanyanyaswa kinoma hata huko uswahilini kwao wananyanyasa sana. BIG UP WA TZ ENDELEEENI HIVYO HIVYO kila mtu anajivunia nyumbani kwake muda wa kujipenedekeza kwa wazungu umepita.

    ReplyDelete
  63. huyu jamaa wa newyork atakua na matatizo,kwa nini ajaziwe form na anajua kusoma?asidharau customer care ya bongo,ulaya tunaongozwa na mabango na ni mara chache utakutana na watu.tz huduma ya kuchange pesa bureau de change siyo bank.ukiyenda mbugani una iternarly na tour operator na siyo unamuuliza kila unayemuona.acha dharau kabisa kila sehemu na taratibu zake na heshimu kila mtu na siyo unapeleka nyumbani nyodo za Newyork.

    ReplyDelete
  64. wahudumu wenye dhereu kwenye kazi ni pambafff!!!!

    ReplyDelete
  65. Heshima kitu ya bure bwashee. Watanzania ni watu wakarimu sana kwenye sehemu zao za kazi, ukiwapa heshima utapata heshima back maradufu, from the airport to anywhere else. Kwa mtazamo wangu, tatizo kubwa la watu ni takrima, watu wako driven sana na takrima, especially sehemu za serikalini, lakini private sectors, i.e. hotels nakadhalika sijawahi kupata tatizo lolote.
    Nimetembelea mpaka Zanzibar, watu wacheshi mno.

    Ushauri wangu, wewe nenda bongo ji-mix kimtindo, utafurahi. Tena ukiwa unapiga vi tip vya hapa na pale unaweza kulambwa hata miguu.

    Ipo siku tutafika, till then show R-E-S-P-E-C-T.

    Mdau wa NY vile vile.

    ReplyDelete
  66. kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  67. Mimi ni Mtanzania ninaye ishi nje ya nchi na huwa natembelea nyumbani kila mwaka,kwaupande wangu sikubaliani na malalamishi yaliyotolewa nahisi kaka unadharau sana.Watanzania wengi walio nje wanapenda wakifika nyumbani wanyenyekewe kisa wanaishi nje,huo ni ushamba na ujinga,next time ukienda nyumbani jaribu kuwa na heshima na kupunguza maringo huta pata matatizo.Tanzania ni kwetu kaka kamaunaona unachakubadilisha beba mabegi urudi ukasaidie!Ilasijui hata kama umeenda shule kwani hata form za immigration ulisaidiwa kujaza na hao ulio watukana nakuwaona wajinga!Grow up!

    ReplyDelete
  68. Hoi Hoi..Kazi ipo.Niko USA Los Angeles na nilikuwa bongo last year.Bongo mambo tambarare tu!!
    Huyu jamaa wa New York hana tofauti na rafiki zangu ninaowajua,Dharau tu! Hata hapa Los Angeles ukishasema unatoka NY wanakujua kuwa wewe ni Bishoo! Why? Mabishoo wengi wa kitanzania walikwenda kuishi NY labda kumuona P.DIDDY

    Mabishoo wengine walikwenda Texas.Ni los Angeles tu katika miji mikubwa ya USA ndio inawatanzania wana hekima na muono.

    Hey NY guy.. next time ukienda bongo try to be humble halafu tuandikie.Tanzania ni third world country for a reason...what you see is what you get.. shut up and enjoy.

    I love Tz.

    ReplyDelete
  69. Shamba labibiDecember 29, 2011

    Mimi niliombwa "hela ya soda" na mfanyakazi wa airport mwezi uliopita. Uwanja mwingine wa ndege tulipata matatizo Kilimanjaro International Airport. Ndege yetu ilifutwa, ila hawakutuambia, nilisikia tu kwa wateja wengine waliokuwa wamepanga foleni. Tukasubiri wee mwisho wake wakapakiza ndege kusema inaenda Dar, lakini walikosea kumbe ilikuwa inaenda Zanzibar! Ikabidi abiria wengine washushwe. Masikini ilibidi nisaidie mdada mmoja mmitaliano ambae alikuwa hajamuelewa mfanyakazi wa KIA jinsi alivokuwa akitoa ujumbe kwa wasafiri. Kiingereza kilikuwa hakitoki na jeuri mbele kwa mbele, mpaka yeye na mfanyakazi mwenzake walikuwa wanagombana mbele yetu. Customer service ni mbovu, na wanaobisha hapo juu ndio tatizo. Badala ya kusikiliza yaliyojiri mnamtukana na kusema kuwa anaringa sababu amekuja na mzungu. Kwani alisema wapi kuwa kaja na mzungu? Wacheni ushamba. Nilisafiri Kenya na Tanzania miezi kadhaa iliopita na kweli TUMEPITWA Tanzania. We will only wake up and act right when there is competition, so bring on the competition! It is time!

    ReplyDelete
  70. Mdau wa New York, Wafanyakazi wa Mamlaka za Kibongo zinazoongoza kwa Dharau na Huduma kwa Wateja Dhaifu dhidi ya Wateja ni kama hizi hapa ktk Orodha:

    1.MABENKI YOTE:::
    -CRDB
    -NBC
    -NMB
    -STANDARD CHARTERED
    -BARCLAYS
    -STANBIC
    -Na zingine zote hata za Kila hoi kama BOA,TPB,AKIBA,ACCESS,DTB n.k.

    2.IDARA NA MAMLAKA ZA KISERIKALI:::
    -TRA
    -DAWASCO
    -TANESCO
    -TTCL
    -NSSF,PSPF,PPF,LAPF,GPF n.k

    3.MAMLAKA ZA SERIKALI::::
    -UHAMIAJI
    -IDARA ZA HUDUMA KTK MADIRISHA YA WIZARA ZOTE
    -VIZAZI NA VIFO
    -HOSPITALI ZA RUFAA NA ZA MAENEO MAALUM

    4.MAKAMPUNI YA HUDUMA:::
    -VODACOM
    -TIGO
    -AIRTEL
    -ZANTEL

    Ukisikia MIUNGU WATU ni WAFANYAKAZI WA TAASISI HIZO HAPO KTK MAFUNGU MA 4 JUU hapo ni DHARAU na RUSHWA KWA KWENDA MBELEEE!!!.

    HAWA WATU WANASAHAU KUWA INABIDI WAFUNGE MIKANDA KWA USHIRIKI WETU KTK JUMUIA YA AFRIKA YA MASHARIKI-EAC.

    WATAMBUE KUWA KUTAKUWA NA USHINDANI NA ULINGANISHI KTK MAKAMPUNI NA HUDUMA ZA KIJAMII ZA KISERIKALI KTK ENEO LETU HILI LA NCHI 5 SASA!!!.

    WAKIFANYA MCHEZO WATARUDI MAJUMBANI KUKAANGA MIHOGO BAADA YA KUMWAGWA KAZI NA WAFANYAKAZI WANAOJUA WA NCHI JIRANI RWANDA, UGANDA,KENYA NA UGANDA KTK UMOJA!!!!

    ReplyDelete
  71. kwanza wewe huko ulaya unafanya kazi gani siyo kusafisha naniliii, loooh halafu mi hata cendelei kusema ntachafua hali ya hewa bure!

    ReplyDelete
  72. NDUGU YANGU POLE SANA. HAPA TANZANIA MTEJA NI FALA NA SI MFALME KAMA WASEMAVYO WENGI. HILI JAMBO LINATOKANA NA KWAMBA WATU WANAPEANA AJIRA KWA KUFAHAMIANA, KWA HIYO INAKUWA VIGUMU SANA KUMUWAJIBISHA MTU HATA ASIPOFANYA KILE KILICHOMPELEKA KAZINI. NI MARA NYINGI SANA UTAONA BANK TELLER ANASITISHA HUDUMA ILI AANDIKE UJUMBE KWENYE CM YAKE YA MKONONI. LAKINI NADHANI BANK ZA KIGENI ZINAZOKUJA ZITASAIDIA KIDOGO KWA KUONGEZA USHINDANI.

    ReplyDelete
  73. POLE SANA MDAU
    Mimi naishi Tanzania na nimewahi kufanya kazi benki ( Barclays)
    Yaliyosemwa na mdau ni UKWELI MTUPU...
    Customer care ni mbovu sana kwenye mabenki na ofisi nyingi za serikali..
    makampuni ya simu ndo usiseme... Vodacom is a nightmare...
    I have not been in Europe or USA but in Kenya several times...
    Kenyans bana are smart.. ukienda duakani kuspend elfu 10 unajikuta umeacha laki....
    Tunahitaji kubadilika watanzania
    Dstv tanzania is the best in customer care..
    ILA NI UKWELI PIA KUWA MNAOTOKA ULAYA MNAKUJA NA NYODO NA DHARAU NYINGI..( KISHAROBARO ZAIDI)... HAKUNA BINADAMU ANAEPENDA KUDHARAULIWA ..JIREKEBISHENI

    ReplyDelete
  74. mimi sidhani huyu jamaa kama ni mtanzania kweli. Kama kusafiri wengi tumesafiri na tumerudi lakini immigration procedures ziko wazi kama kweli una nyaraka zako sahihi.

    Pili sijui ni benki gani au bureau de change inayoweza kumtengulia mteja kiasi hicho anachokisema.

    Analinganisha na kenya bila kutoa reference ni lini ameenda kenya au ndo kasikia watu wakisema..

    Hana lolote zaidi ya ulimbukeni

    ReplyDelete
  75. UBOVU WA HUDUMA KWA WATEJA KTK TANZANIA::::::::::::::::::::::

    Uozo huu unaletwa kwa mambo makuu kama hapa chini:

    1.RUSHWA,
    Ya FEDHA ,ya NGONO wengine wanafikia KULAWITIWA ILI KUPATA KAZI!

    (Hebu angalia mtu anapata kazi kwa kulawitiwa, akifika kazini atafanya kazi vizuri kweli?...lazima atakuwa na kiburi kwa vile aliipata kazi kwa kudhalilika na sio kwa sifa stahiki)

    2.UPENDELEO NA UBINAFSI,
    Watu wanasaidiana sana ,unakuta mtu hana ujuzi wa kazi husika lakini kwa misingi ya vimemo anawekwa anakaa kama SANAMU LA MICHELLIN huku kanuni za kazi hiyo akiwa hazijui!

    3.KUGHUSHI,
    Watu wanatafuta kazi wakikuta sifa hawana wanaingia Mtaani wanafyatua vyeti wanaandika CV wanatuma maombi wanatumia kujuana juana au wanahinga wanapata kazi.

    SASA WANDUGU KAZI ZINATAKA UJUZI NA KUFUATA KANUNI ZAKE, SASA KWA MAZINGIRA HAYO MATATU 3 HAPO JUU INA MAANA UNAOWAKUTA KATIKA MADIRISHA YA HUDUMA KWA WATEJA TANZANIA SIO WASTAHIKI WA HAPO, WENYEWE WAPO MITAANI WANACHOMA MAHINDI!

    ReplyDelete
  76. Mdau ujumbe wako ulikuwa sahihi ila umeuleta kidogo si vizuri sana! haya matatizo ni kweli yapo, ingawa si kila sehemu na si kwa kila mfanyakazi! Mi ntatoa mfano mdogo tu, nilikuwa nasafiri kwenda Canada mapema mwaka huu, pale Mwl Nyerere Airport kuna vijana sikuwaelewa kabisa! wananiuliza passport niliipataje, ilhali nimeshasafiria hadi Australia na ina mihuri mingi tu! Kwa kweli walinishangaza sana! Baadae nikajua shida yao. Waliendelea kunifuatilia hadi nilipopanda gorofani kwa check in ya pili! Eti wananiuliza nnawaachaje! Aibu gani hii! Niwaacheje nimewaajiri!? Natamani nimtaje mmoja kwa kuwa hata jina lake nalikumbuka kwani alivalia kitambulisho! Kwa hiyo kimsingi watanzania wenzangu haya matatizo yapo na yanatia aibu!

    Pili sina hakika kama ni kweli kuwa Amsterdam kuna hayo manyanyaso aliyosema anony hapo juu! Nimepita Amterdam zaidi ya mara sita sijapata tatizo lolote! Tuache ushabiki, tuzungumze uhalisia, bado tuna shida katika nyanja ya huduma kwa wateja! Unaombaje mteja hela??!

    ReplyDelete
  77. Jamani watanzani acheni tabia ya kutokuwa wakweli, hao waliosema kuwa huyo kaka ana nyodo eti sababu katoka ulaya ni wajinga na hawajui maendeleo.
    Kusema ukweli alichokiongelea ni cha kweli kabisa watanzania hatuna customer care nzuri. We nenda baa tu uone jinsi unavyuodharauliwa na muhudumu wa bar wakati pale umeende kunywa pesa yake ili yeye aweze kulipwa japo msharaha lakini dhara ni nyingi, Huko kwenye mbuga za wanyama na mahoteli ya kitalii ndo usiseme yaani wnajiona kuwa ndo wamepata kazi nzuri kuliko watu wote. Yaani huko kwenye mabenki ndo kabisa, ni benki chache sana ambazo nafikiri wanapata japo kwa mwaka semina mara moja za customer care lakini hao mateiller wanajiona ndo wamefiki wakati ndio kazi ya chini kibenki.Pole sana kaka yangu, mitanzania ndio hiyo sijui tutabadilika lini. Ulalamishi tu na kudharau maoni ya watu.

    ReplyDelete
  78. CUSTOMER CARE TANZANIA IMEOZA NA INANUKA UVUNDO....!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    1.HUDUMA KWA WATEJA YA MAMA NTILIE, AU KUTOKA KWA CHANGU DOA USIKU IPO JUU ZAIDI SANA TU, KULIKO YAO KTK TAASISI!,(HII WAKUBALI AU WAKATAE SHAURI YAO,,,ILA UKWELI UNAUMA)

    2.WACHA HUKO MBALI UGHAIBUNI MAREKANI NA ULAYA, HUWEZI IWEKA TANZANIA KATIKA ULINGANISHI WA HUDUMA KWA WATEJA NA JIRANI ZETU KAMA, UGANDA,RWANDA,BURUNDI,ZAMBIA,MALAWI,MSUMBIJI NA KENYA!(HII WAKUBALI AU WAKATAE SHAURI YAO!,,,ILA UKWELI UNAUMA!)

    (WE NEED EXCELLENCE!),(TUNATAKA UFANISI!)

    MDAU WA NEW YORK ALIEKUJA NA WATU WAKE KUTUMIA US$ ZAO WALISTAHILI WAPEWE HUDUMA KULINGANA NA HELA YAO NA SIO VINGINEVYO, (HUDUMA CHINI YA KIWANGO)...SASA KWA NINI ASILALAMIKE?

    HAO WANAOKATAA NDIO WALE WALE, INAWEZEKANA NDIO WALIO FRONT DESK ZINAZOLAUMIWA AU LABDA WANA ND
    UGU NA HAO (MIUNGU WATU WAJINGA) WALIPO KTK MADIRISHA YA MBELE YA HUDUMA KTK TANZANIA, SIO BURE!,,,SASA WANATETEA NINI?

    ReplyDelete
  79. weee anon wa
    Thu Dec 29, 08:12:00 AM 2011

    jamaa kasema anatoka new york. new york sio ulaya wewe!!!!!

    ReplyDelete
  80. HANA LOLOTE MDAU WA NY, UNAJAZIWA FORM ZA IMMIGRATION??????!!!!. DAH SHAME, ATI NIMEKUJA NA SHEMEJI ZANGU,, KWAIHIYO NDIO IWEJE SASA. MBEBA MABOX TU HUYO. NA LAZIMAA ATAKUWA AMEPIGA MLEGEZO,,, EEH. KUA KAKA JIFUNZE KUTOA MAONI KISTAARABU SIO KWA LUGHA ZAKO HIZO ZA KIMLEGEZO!! BIG UP BONGO.

    ReplyDelete
  81. TO ALL CUSTOMER CARE STAFF IN TANZANIA-(KWENU WAFANYAKAZI WOTE WA HUDUMA KWA WATEJA-TANZANIA)
    ------------------------------------
    ONCE YOU ARE MARRIED WOMAN YOU ARE NOT SUPPOSED TO SLEEP WHILE WEARING A JEANS PANT!
    ------------------------------------
    MARA MNAPOKUWA MMEOLEWA HAMSTAHILI KULALA NA KAPTULA NZITO!
    ------------------------------------
    BE FOOL OR DUMB, THE CUSTOMER DESERVES A BRIDE GROOM CARE!
    ------------------------------------
    HATA AWE MJINGA AU TAAHIRA, MTEJA NASTAHILI HUDUMA KAMA BWANA HARUSI!
    ------------------------------------
    THAT IS ALL!, Thanks!
    ------------------------------------
    HAYO NDIO YOTE!, Ahsante!
    ------------------------------------

    ReplyDelete
  82. MDAU WA NEW YORK ,,,yeye JEMBE na amekuja na DOLLA, ingawa bosi huyo Form za Immigration anajaziwa,,,sasa kwa nini CUSTOMER CARE WA TANZANIA WASIMBEBE MGONGONI EENH?

    ReplyDelete
  83. Duuh kudadadeki... coments zaidi ya 80... lakini bado sijamuona humu prince mashaka akichangia.

    ReplyDelete
  84. OYA ACHA NYODO .UNATUSAGIA WABONGO WAKATI MKIFA HUKO NY MNATUOMBA TUWACHANGIE MRUDISHWE HOME .ACHA HIZO,NA UKITAKA KUJUA SISI TUNAPETA NA BONGO YETU WE NJOO UUGUE UENDE MUHIMBILI HALAFU USITOE KITU UTEGEMEE MSAADA KAMA NI KANISANI UTADEDI UNAJIONA

    ReplyDelete
  85. Hawa ma CUSTOMER CARE WA BONGO/ HUDUMA KWA WATEJA WANAKERA SANA!

    Mfano kazi ya Dirisha la Mbele /Front Desk ni kazi nyeti sana ingawa kimuonekano inaonekana ni Dhalili, hilo wenyewe hawalifahamu wao na Mabosi wao.

    WATAALAMU WANASEMA ,MWENENDO WA SEHEHU UNAYOTEMBELEA KAMA NI KAMPUNI AU TAASISI UNAAKISIWA NA ATAKAVYOKUCHUKULIA MTU WA DIRISHA LA MBELE!

    ''THE WHAT ABOUT OF THE BUSINESS OUTLET YOUR ARE APPROACHING IS REFLECTED WITH FRONT DESK STAFF'S CARE!''

    ReplyDelete
  86. Poor Customer Care in Tanzania/ Uduni wa Huduma kwa Wateja ktk Tanzania.

    Hii inachangiwa na ile dhana ya kila mtu kwa vile yumo ndani ya mjengo huo wa Taasisi au Kampuni hata kama ni mpika chai au Mesenja anajichukulia na yeye kama Bosi!

    ReplyDelete
  87. Customer Care Tanzania/ Huduma kwa Wateja Tanzania.

    MBAYA ZAIDI TAALUMA HII INACHUKULIWA KUWA NI YA KIKE ,AMBAPO KIGEZO NI UZURI TU, NA WAO WENYEWE WANAONGEZA SIFA ZA ZIADA KUWA NI JEURI,NYODO NA MARINGO!

    Imejaa Wasichana wasafisha kucha na waosha miguu TU, wengi hawana sifa za elimu na ni aibu wengi KIINGERZA mgogoro hawajui au wanababaisha tu, wanaghushi, wanatumia rushwa ya ngono na uchawi kupata kazi!

    NDIO MATOKEO YAKE HAYA!

    ReplyDelete
  88. Kijana inaonekana ni walewale kata k"jeans chini ya matako" heshima 0 .. Mbona mimi nipo u.k na kila bank au ofc ninayo kwenda napokelewa vizuri na wakina dada na makaka. Ngoja nikufundishe wewe ngoima , umeongia maali badala ya kusema wewe au njoo hapa niudumiye sema samahani au Naomba usisema ela yako na Bado Niombe samahani au Niombe lah ni jinsi tulivyo funswa na utamaduni wetu ulivyo .. Issue vijana wa u.s heshima hamna kabisa yani kila mnapo kwenda mpo kishari na mnajiona mnajuwa sana. Mfano - Mwaka jana nilikuwa na dada yangu anaishi u.s wote tulikuwa likizo Tanzania ila ilibidi nimfundishe jinsi ya kuongea na watu adi wazazi sijuwi mnajisahau au ulimbukeni .... Nafikiri mungu awasaidiye nyinyi siyo Tanzania .... I love Tanzania na watu wake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...