Askari wa Usalama Barabarani wakichukua maelezo toka kwa majeruhi hospitali ya mkoa wa Morogoro jioni hii
 Majeruhi wakifikishwa hospitali ya mkoa Morogoro
Picha na Habari na John Nditi, 
Morogoro.


ABIRIA wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine 29 kujeruhiwa na baadhi yao kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, baada ya basi la Upendo  ‘Travel Coach’ walilokuwa wakisafiria kutoka Mkoani Dar es Salaam kwenda  Iringa  kupinduka eneo la Doma , Wilaya ya Mvomero, Barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni ya leo Januari 3, mwaka huu eneo la Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero, katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa kwa kuhusisha basi lenye namba za usajili T 510 AMZ aina ya Scania.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo , ambapo  chanzo chake ni baada ya lori lililokuwa likitaka kulipita jingine  kutaka kugongana uso kwa uso na basi hilo, kitendo kilichomfanya derava wa basi kulikwepa na hatimaye kupinduka.
Hata hivyo alisema, maiti moja imetambuliwa kwa kina la Hamis Ramadhani Mbwana ( 26) mkazi wa Handeni Mkoani Tanga ,alitambuliwa baada ya kupekuliwa nguo alizovaa na kukutwa  leseni yake ya Uderava ikiwa na jina hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, maiti nyingine ambayo ni ya mwanaume bado haijatambuliwa na umehifadhiwa Chumba cha maiti cha Hosipitali ya Mkoa huo ikisubiri kutambuliwa.
Hata hivyo karibu majeruhi wengi walikuwa walikuwa ni  wanafunzu wa Vyuo, Shule za Sekondari na  Msingi , ambao walikuwa wakirejea kwenye maenao yao baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo, Firbert Nyoni , Maneno Abdallah , Aline Mhina pamoja na Salum Mfaume, walisema kuwa juhudi za dereva wa basi kulikwepa lori kiliwezesha

kuokoa maafa makubwa zaidi.
Kwa mujibu wa Mfaume aliyeunguzwa na maji la rejeta tumboni na mgongoni na kulazwa wadi ya majeruhu namba moja katika Hospitali hiyo , alisema , malori hayo yalikua wakifukuzana kwa mwendo kasi, na moja lilitaka kulipita jingine hali iliyosababisha kutaka kugongana  basi hilo, ndipo Dereva alilikwepa na kusababisha basi kupunduka.
“ Juhudi za Dereva wa Basi ndizo zimewezesha kupunguza vifo na majeruhi…lakini wenye malori walikimbia baada ya sisi  kupatwa na ajali hii…na mimi imeungua sana mgongoni na tumboni” alisema Majeruhi huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. I DON'T REALLY BLAME MADEREVA I BLAME THE GOVERNMENT, IF U DONT DEALLY WITH UR OWN PEOPLE WHO DO U THINK WILL LOOK AFTER THEM, WEKA SHERIA KALI KUHUSU VYOMBO YA BARABARANI THEN U WILL SEE WHAT HAPPEN,

    1) IF U OVER SPEEDING, UR LOSE UR D/L AND NOT ALLOWED TOR DRIVE FOR THE NEXT FIVE YRS,
    2)YOU DONT HAVE M.O.T YOU CAN'T USE UR VEHICLE, AND HAS TO BE TESTED KILA MWAKA.
    3) DRINK DRIVE, FINE AND LOSE UR D/L AND NOT ALLOWED TO DRIVE FOR 5YRS.

    AND THIS HAS TO BE REALLY STRONG,

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza, tatizo ni kwamba kila uamuzi unaochukuliwa na serikali unageuzwa dili na watu wa humo humo serikalini. Kwa mfano, kama mtu una pesa au cheo fulani huwezi kunyang'anywa leseni, hivyo sheria inakosa maana. Tunahitaji mabadiliko ya tabia kwa hali ya juu, nalo sijui linawezekana vipi wakati watu wanaona ni sifa na ujanja kuendesha ovyo.

    ReplyDelete
  3. Umasikini ndiyo unaotuua kila siku barabarani.Hata siku moja mstari wa kuchorwa hauwezi kutenganisha magari yanayoenda na yanayorudi kwenye highway. dereva akiinama tu kuchukua coffee, au kubonyeza bottons za cd, woppers au fog lights, asipokuwa makini akapanic wakati wa kurudisha macho barabarani ni rahisi sana kuchinja abiria kwa staili ya uso kwa uso. Akikwepa kapindua maana anakwepea bondeni na kuliacha tuta la highway. Mstari unaweza kutenganisha incoming and outgoing traffic kwenye local roads only na siyo highy. Tutalaumu madereva bure, wao pia ni binadamu, they have bad and good days just like everybody else. Barabara zenye viwango vya highway zipanuliwe. Tukisema tuweke steal beams au concrete kama wenzetu ili kutenganisha wanaoenda na wanaorudi bado hatuna waiting areas servicing breakdowns. Kwahiyo mtu akipata flat tire maana yake kazui walioko nyuma yake. Lazima tuwe na walau lane mbili zinazokwenda, leni mbili zinazorudi, katikati steal beams au concrete barrier. Hii itaruhusu wenye haraka kuovertake ama kutumia lane za ndani na wasio na haraka watumie lane za pembeni.Unless we implement that changes highways zetu zitaendelea kuwa bucha za nyama. Tha's is the reality whether we agree or disagree. Poleni sana wafiwa na majeruhi. Tatizo tumezaliwa kwenye umasikini.

    ReplyDelete
  4. Hii inaonyesha ni jinsi gani nchi yetu iko nyuma ,badala ya kuwahudumia majeruhi ,police wanaanza kwahoji,thats stupidity.Wahudumieni kwanza halafu mahojiano baadae

    ReplyDelete
  5. money is the law ther is so many things to be sorted out 1st b4 tinkin bout mot o 2 ban some1 from driving corruption is the root n dis is from de top.

    ReplyDelete
  6. mbona wewe ni coward un aogopa nini in tanzania ders no freedom of speech y mani yangu huyatoi hii ni mara ya 10 sasa ur coward

    ReplyDelete
  7. Lets get serious jammani...mbona tunamalizika kila leo,inachosha,inasikitisha

    ReplyDelete
  8. HAO POLICE NDIO KAMA HUIVYO HAKUNA SHERIA ISIPOKUWA DEREVA ATATAFUTWA MPAKA APATIKANE ILI WAMTOE RUSHWA BASI MCHEZO UWE UMEKWISHA. NI UJINGA NA TUTAZIDI KUWA WAJINGA MPAKA DUNIA ITAKAPOKUBALIANA NA UJINGA WETU. NCHI HAINA SHERIA WALA KATIBA,SASA WADAU MNAFIKIRI ITAKUWAJE,HATA HOSPITALI HAZIPO HIO SIO HOSPITAL NI BALAA TU KWANI HATA HAO MAJERUHI, SANA SANA WATAPEWA PANADOL KUPUNGUZA MAUMIVU BASI HAKUNA EX RAY HAPO. WALA MUHIMBILI HAWANA WEWE UKIPATWA NA JANGA KAMA HILO NI KUFA TU
    HUYO RAIS HANA LOLOTE AFANYALO ZAIDI YA KUJILIMBIKIZIA HAZINA YAKE HANA LOLOTE ALILOFANYA KUNUFAISHA TAIFA ,CORRUPTION, MAJANGWA,MARADHI WAO WAKIPATA AJALI WANAPELEKWA INDIA KUTIBIWA NDIO KWAO HAO VIONGOZI HAPO MAJERUHI HATA BANDAGE YAKUFUNGIA KIDONDA HAKUNA, PLASTER WATANUNUA PRIVATE HOSPITAL ZA WAKUBWA WANAOJIONA WAO NDIO TANZANIA ZAIDI YA WENGINE

    ReplyDelete
  9. Wed Jan 04, 01:26:00 AM 2012 ANON WA NNE KUTOKA JUU UMENENA

    ReplyDelete
  10. Mdau wa pili, kinachotakiwa ni kubadili kabisa system kwa maana ya kuwaondoa wote walio madarakani kwa sasa. Mbona inawezekana kabisa, tuungane mwaka 2015 tuwe kitu kimoja tuwaondoe wote hawa wanyonyaji. They dont realy care about us citizens, nyie hamjashtuka tuu pamoja na vilio vyooote hivi???

    ReplyDelete
  11. POLE SANA DADA NAONA MKONO UNKUUMA SANA...HAPA NDIO PETU BONGO

    ReplyDelete
  12. yeye polisi wa bongo hana kazi zaidi ya kwenda chukua rushwa huko barabarani, baada ya kuwapa huduma kwanza, kanunua karatasi kiosk eti awahoji waathirika! kweli hio ndio Tanzania ? mimi sirudi huko wala sikusahaau kitu. Haiwezekani kila siku sisi tu watanzania ndio watu wa kufariki kwa ajali za barabarani kama mbwa pori yaani haieleweki ni kwa nini.Hazipi siku mbili lazima utasikia kuna BUS limeua kumi, 20,43. sasa itakuwaje inamaana waliotengeneza hayo magari wenyewe wazungu ni wajinga -

    Dereva atakae UA kwa makusudi na yeye auawe kwa kupigwa mawe National Stadium kama wanavyofanya SAUDIA .dereva anatakaapige trip nane za Dar Moro kama anakimbiza mahindi sokoni kweli hajui kama anabinadamu ndani ya gari, kweli na ni kwanini ni kila siku hayo matukio?

    Mdau Holland

    ReplyDelete
  13. UMAKINI KTK USALAMA BARABARANI:

    ILI KUPUNGUZA WIMBI LA MAAFA YA AJALI,

    Mamlaka zisiwe zinaishia tu kugawa Leseni za kuondeshea vyombo vya moto tu:

    LAZIMA HAYA CHINI YAZINGATIWE:

    1.WENYE LESENI WOTE NI MUHIMU KUPEWA MAFUNZO YA MARA KWA MARA NA KUKAGULIWA MAKOSA YA UENDESHAJI,,,HASA WATAKAO KUWA NA REKODI YA AJALI!

    *****INGAWA TAYARI WALISHAPITIA MAFUNZO YA UDEREVA NA WANAZO LESENI,,,WASIISHIE KUENDESHA KWA MAZOEA TU INAWEZEKANA WANAENDESHA KIMAKOSA IKAWA WANAJIJUA AU HAWAJIJUI!*****.

    2.AFYA NI KAMA KITU, MTU ANAWEZA KUWA MZIMA MUDA HUU LAKINI WAKATI UJAO AKAWA SIO MZIMA KIMAUMBILE AU KIAKILI!

    *****INAWEZEKANI KIPINDI FULANI MTU AKAENDESHA CHOMBO HUKU AKIWA AKILI ZAKE SIO TIMAMU!*****.

    ReplyDelete
  14. afrika afrika tu yaani hata hili basi lifike hospitali siwatu washapoteza maisha yao duh.

    ReplyDelete
  15. Duhh, suluhisho ni upimaji wa afya kwa maderva mara kwa mara, afya ya akili, afya ya maumbile, afya ya macho na vinginevyo sanjari na mafunzo ya kanuni anuai za usalama barabarani!

    Ama sivyo wooote tutaishia barabarani!

    ReplyDelete
  16. Unakuta mtu alipata leseni tokea mwaka 1978 kimpango mpango kwa kutuma picha ya pasipoti Arusha kwa Mjomba wake Trafiki akatumiwa leseni kamili!

    Huyo dereva tokea hiyo 1978 ame renew leseni mara kibao na sasa anapata mpya ya TRA lakini hajawahi kuuona mlango wa Hospitali inawezekana huyo mtu sasa ni Taahira!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...