Baadhi ya Polisi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa marehemu Kijanda wakielekea kuzika huko Kahangara Magu, Mkoani Mwanza. Mwandu aliuawa kwa kupigwa risasi shingoni na jambazi wakati akiwa katika harakati za kumkamata
                            Polisi wakiweka chini jeneza la marehemu kabla ya mazishii
  Robert Manumba (DCI) akitoa salamau za jeshi la polisi baada ya mazishi ya PC Kijanda aliuawa na jambazi kwa risasi
                                                   Jeneza lenye mwili wa marehemu Kijanda
 Askari wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya  Jeneza lenye mwili wa marehemu Kijanda
 Askari wa Jeshi la Polisi wakitoa heshima wakati wa mazishi ya askari mwenzao marehemu PC Kijanda Mwandu, katika makaburi ya kifamilia eneo la Kahangara, wilayani Magu, Mwanza juzi, Mwandu aliuawa kwa kupigwa risasi shingoni na jambazi wakati akiwa katika harakati za kumkamata
  Maaskari wakiushusha mwili wa maremhu PC Kijanda kaburini ,mazishi yaliyofanyika Kahangara Magu
                        Baadhi ya ndugu, jamaa wa marehemu wakiweka mashada juu ya kaburi la PC kijanda
 Askari wa Jeshi la Polisi wakitoa heshima wakati wa mazishi ya askari mwenzao marehemu PC Kijanda Mwandu muda mfupi baada ya kuzikwa katika makaburi ya kifamilia eneo la Kahangara, wilayani Magu, Mwanza.Picha na Mdau Mashaka  Baltazar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mungu amurehemu marehemu. Itakuwa kheri kama Jeshi la Polisi litapata somo kutokana na tukio hili ya kwamba mbwa akikuzoea atakufuata mpaka kwa msikiti. Majambazi wanayajua hivo si vyema kuyalea, ona sasa yamewaua askari wenyewe!

    ReplyDelete
  2. Kwanza niwape pole familia, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki cha majonzi. Pili ni kwa jeshi la polisi kwa kuwa limempotesa askari wake liliyempa mafunzo ili aweze kufanya kazi za usalama wa raia. Naamini huyo jambazi alikuwa akifanya ujambazi wake mahali penye watu. Je hao wananchi walisaidia vipi katika purukushani hizo? Wakati askari polisi anapigwa risasi alikuwa peke yake? Kama alikuwa peke yake nawashauri polisi waongeze askari wanapofanya doria mitaani na kama ni jambazi kusiwe na mjadala wa kumkamata akiwa hai. Acheni hao wanaharakati wa haki za binadamu wapige kelele kwani mwananchi au polisi anapouawa wanakaa kimya kama vile hawapo duniani. Ila jambazi akiuawa ndiyo wanaibuka na kudai haki za binadamu. Hao wanaowaua hawakustahili kuishi? Tena unakuta ana familia inayomtegemea. Wanaharakati msiangalie fedha za wafadhili tu, muangalie na utu. Kama mnafuatilia mambo duniani wiki iliyoishia tarehe 7 Januari 2012 kuna kijana wa darasa la nane huko Texas - marekani alikuwa na bastola ya bandia na akawa anatishia kuua. Polisi walipokuja wakamwamuru aidondoshe chini bastola yake akakataa na kuendelea kutishia kuua. Kilichofuata polisi walimpiga risasi tatu akafa. Walikuja gundua kuwa ilikuwa bastola bandia baada ya kumwua. Angekubali kuitupa chini angekuwa hai hata kama ni mahabusu. Polisi jamani "BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA". Lakini chonde chonde yasije yakajirudia ya wauza madini wa Morogoro.

    ReplyDelete
  3. Mazingira ya maujai ya Askari Polisi, Inaonekana yeye Marehemu alifanya kazi kiuadilifu isipokuwa tatizo baadhi ya Askari sio waaminifu katika kazi na mara kadhaa wamekuwa wakishirikiana na Wahalifu mbalimbali.

    ReplyDelete
  4. Du! poleni wafiwa inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  5. R.I.P:Mwenye taarifa tukio lililosababisha kifo cha huyu kijanda anisaidie.Nimesoma alipigwa risasi ya shingo na jambazi..Wapi?Geita mgodini?

    David V

    ReplyDelete
  6. poleni sana wafiwa tunaomba serikali iwe makini sana washirikishe wanajeshi kufanya ulinzi na kupambana na majambazi

    maana wanajeshi hawana kazi zaidi ya kula kulala wanasubiri vita mpaka wanastaafu

    hali inatisha sana ikiwa majambazi tu wanaelekea kulishinda jeshi la polisi je patakapotokea machafuko makubwa kweli wataweza?

    ReplyDelete
  7. akina Ras Makunja poleni sana kwa msiba huu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...