Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli akihutubia leo wakati wa hafla ya utiliaji wa saini wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unatarajiwa kuanza siku yeyote kuanzia hivi sasa leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkataba huo umesainiwa baina ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wakandarasi kutoka nchini China ambao ni CHINA RAILWAY JIANGCHANG ENGINEERING CO. (T) LTD na MAJOR BRIDGE ENGINEERING CO. LTD.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla hiyo leo ambapo ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuomba kazi za ujenzi huo wa mradi wa daraja la Kigamboni.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akihutubia katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo wakati wa kutoa hotuba yake juu ya mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambao utagharimu kiasi cha sh. Bilioni 214.6 na utachukua muda wa miezi 36.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ukijua kucheza karata bwana........Kila kitu kwako ni kama unaria! Ngoja tuone.

    ReplyDelete
  2. Magufuli,Dau na msechu(NHC) ni mifano ya watu wa vitendo zaidi kuliko maneno hapa nchini kwetu.Tunahitaji watu kama hawa ili mambo yaende.Daraja hili litabadilisha kabisa maisha ya kigamboni,mama Tibaijuka tunataka new kigamboni city mama.

    ReplyDelete
  3. NSSF Kwa hili mnazidi kutisha mnaonesha ni jinsi gani mmejipanga katika kuibalilisha TZ kwa ujumla,live longer DR RAMADHANI DAU.

    ReplyDelete
  4. Nampenda sana Dr. Dau kwa utendaji kazi wake pamoja na kijana Mchechu, ni wakati wa Dau kupelekwa TRA akarekebishe na pale liwe shirika lenye tija, angalia udom, miradi ya umeme kama mashirika yote ya kijamii yangekuwa kama nssf hatuhitaji misaada ya masharti toka nje, mungu ibariki TZ, mpe afya na siha njema Mh Rais JK, baada ya kumaliza wengi ndio watakuelewa daima mbele mh

    ReplyDelete
  5. Magufuli hahusiki na Mradi huu.

    kwani Mradi huu uko kwenye Ilani ya CCM ya 2010 wakati huo waziri alikuwa Dr.Kawambwa na ndiye aliyeshiriki kuandaa Ilani ya Chama kwenye eneo la miundombinu.

    Mchechu uwezo wake bado mdogo kama ilivyo shule yake ndogo.tumpe muda kwanza tumuone kwani maneno ni mbali na vitendo.

    Mradi huu wa daraja ulianza chini ya waziri Basil Mramba akiwa waziri wa kwanza wa miundombinu kwa serikali ya awamu ya Nne.na waliona haja ya kuanzisha Mradi huo ni Nssf si Magufuli.

    ReplyDelete
  6. Nadhani imefika sasa watu wanaotenda kazi kupewa nafasi katika taasisi mnyeti kama Uwaziri mkuu, TRA na Tanesco... hivi vichwa vitatu angalau tuna cha kujivunia Tanzania, Siasa za nini wakati mambo hayaendi? Big up guys

    ReplyDelete
  7. Sawa Magufuli, tunahitaji Utekelezaji na sio Siasa,

    Pia kwa gharama kubwa za ujenzi isiwe kisingizio, Kivuko cha Feri kwenda Kigamboni hapana gharama zozote za Ujenzi pamekuwepo kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu labda ni hizo Pantoni na ni juzi tu umeamrisha TOZO la Shs. 200/=kuvuka...SEMBUSE DARAJA LA KIGAMBONI?,,,,USIJE RUKA KIMANGA OHHH KUVUKA Shs. 2,000/= asiyetaka AOGELEE!!!

    ReplyDelete
  8. MRADI WA DARAJA LA KIGAMBONI CHINI YA MRAMBA:

    Wewe Anonymous wa Tue Jan 10,03:23:00 AM 2012

    Ahhh Mramba nafanya nini hapo tena?

    Sasa unaona afadhali Mungu ametuepusha na kuchakachuliwa na Mchagga!,

    Angalia katika miradi ya ajabu Mchagga huyu aliyoshiki lazima alikuwa na chochote kitu katikati (kwa panga lololo jamaa hafai!!!)

    Hebu angalia suala la ndege ya Raisi isiyo na ubora wa kiwango jamaa alidai ''HATA WATU WALE NYASI LAZIMA NDEGE INUNULIWE''

    Kama Mradi wa Daraja la Kigamboni ungekuwa chini ya Mramba nadhani nchi INGEFILISIKA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...