Na Mashaka Mhando,Korogwe.

ASKOFU wa kanisa LA Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) Askafu Davie Mulenga, alifanya maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake akiwemo Rais Jakaya Kikwete kwa kushika picha yake na ramani ya Tanzania kwa kumaliza miaka 50 baada ya uhuru bila kutokea machafuko na kwamba waliliombea ili miaka mingine 50 ijayo Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani.

Akizungumza katika maombi hayo yaliyofanyika katimamamlaka ya mji mdogo wa Mombo wilayani hapa, Askofu Mulenga aliyekuwa na makazi yake katika mji huo wa Mombo, alisema lazima Watanzani wakiwemo viongozi wa dini watii mamlaka iliyopo madarakani na kamwe wasioneshe dalili ya kuisema hadharani kutakapopelekea kuamsha hasira za waumini ambao wanaweza kuwa chachu ya kuleta migogoro na umwagaji wa damu.

"Viongozi wa serikali mmewekwa na Mungu fanyeni kazi zenu bila mashaka yoyote yale, waheshimuni waliowachagua na kamwe sisi viongozi wa dini tusiwe na choko choko zitakazofanya waumini wetu waichukie serikali yao tukifanya hivyo tunatenda dhambi kwamaana kwenye bibilia Misali mstari wa 20 unaeleza 'mioyo ya viongozi ipo mikononi mwa mungu, tunatakiwa tuamini na kuwapenda," alisema Askofu Mulenga.

Kuhusu suala la kuongezewa posho kwa wabunge linalolalamikiwa na karibu na kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, Askofu Mulenga kwa upande wake alitofautiana na jamii inayopinga suala hilo akisema ni haki yao wabunge kuongezea fedha hizo kwa vile kazi wanayoifanya ni kubwa inayotakiwa kuwa na utulivu katika kipindi chote wawapo bungeni.

"Watu wajue kuwa mbunge ni kalishika Taifa na ana dhamana kubwa ya nchi hivyo wanatakiwa wawe na utulivu na amani wanapopitisha mambo mbalimbali kule bungeni kwa maana hiyo suala la kuongezewa posho ni sawa na hata vitabu vya mungu vinasema 'mtu atakula kwa jasho lake, wabunge wana haki wapewe posho hizo, ni suala la utofauti tu kwani hata miti imetofautiana, wanyama pia wametofautiana, tofauti zipo kila mahala, watu wafanye kazi waache kulalamika," alisema Askofu Mulenga.
 
Katika mkutano huo Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu', aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujiandaa kutoa maoni yao kwa tume itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya marekebisho ya katiba baada ya muswada wa sheria kwa ajili ya kuunda tume kupitishwa bungeni mwishoni mwa mwaka jana mjini Dodoma.

Mbunge huyo alisema kuwa wananchi lazima waepuke maneno ya uzushi kwamba tayari katiba hiyo imepitishwa na rais kusaini akieleza kwamba ni maneno yanayopotoshwa na wapinzani wa serikali na kwamba wananchi wanatakiwa katika kipindi hiki kupitia katiba iliyopo kisha kusubiri kutoa maoni kwa vipendele ambavyo wanaviona vimepungua au kutaka kuongezwa baadhi ya mambo

"Ndugu zangu jiandaeni kutoa maoni yetu wakati huo tume itakayoiundwa na rais ikipita katika maeneo yenu, kilichofanyika kule Dodoma tulipitisha sheria ya kuundwa kwa tume ya kurekebisha sheria...Acheni kuwasikiliza watu wanaowapotosha, chamsingi mje mtoe maoni yenu mkitaka rais akichaguliwa akae maisha mtasema," alisema Profesa Majimarefu na kushangiliwa na umati uliofurika katika viwanja hivyo.

Akifafanua mbunge huyo alisema kuwa madhumuni ya kuundwa kwa tume hiyo ni kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi, kuanisha na kuchambua maoni yao kuhusu katiba waitakayo ikiwemo kuweka mfumo utakawezesha uchaguzi wa spika na naibu spika wa bunge la katiba na kupatikana kwa katiba hiyo na watendaji wake.

Akizungumzia suala la maendeleo, mbunge huyo aliyeongozana na viongozi wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kata hiyo waliochaguliwa Januari 7 mwaka huu kujaza nafasi zilizokuwa wazi, wakiongozwa na Mwenyekiti wa kata Bw.  Yusuph Singano, alisema wananchi wa tarafa ya Mombo hawana budi kuacha majungu na badala yake wajenge umoja utakaosaidia mji huo kupata hadhi ya Halmashauri ya mji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Njaaa mbaya saaaana.
    By Andendekisye Mbije-0718563311

    ReplyDelete
  2. Duh ninamheshimu sana Askofu lakini mbona na yeye anafikiria tu kuhusu Viongozi, angekuwa mkarimu kufikiria walioko chini wanavyo taabika na kupanda kwa maisha na posho ndogo. Degelavita

    ReplyDelete
  3. Askofu njaa huyo siasa imemjaaa kazi kwao waamini wake mwenye macho haambiwi tazama na wala mwenye masikio haambiwi sikia - hakuna dini hapo

    ReplyDelete
  4. Huyo anayejiita Askofu kazi yake kula Sadaka hajui shida za wananchi,akae kimya kabisaaa

    ReplyDelete
  5. ogopa sana hawa viongozi wa dini wakiingilia mambo ya siasa hapo ndipo utagundua kuwa viongozi kama hao wapo kwajili ya masirahi hi na sio uwajibikaji...full stop.

    ReplyDelete
  6. nadhani Askofu mjanja, anajitengeneza uji mwenyewe. maana hapo anaongelea kuhsu siasa lakini anawahasa wengine wasisem hivyo..tofauti yeye anajitengezea pazuri pa kukaa

    ReplyDelete
  7. hapo ndio unapotoa umuhimu wa dini yako,lazima ujue kuna mabadiliko ulimwenguni sababu mojawapo ya mungu kuleta dini ni kufanya watu wakaribiane na wasinynyane wala kutesana,askofu anajipendekeza bila kutoa sababu za kisayansi

    ReplyDelete
  8. ONGEZEKO LA POSHO KWA WABUNGE:

    Ongezeko la posho za Waheshimiwa Wabunge liwe la TIJA kwa kuongeza huduma zao kwa Wananchi, na sio KUWAPA UWEZO WA MATANUZI NA ULEVI!

    ReplyDelete
  9. huyo sio ascoph bali ni mwanasiasa anayejiandaa kwa uchaguzi 2015, kwa kuwaonyesha wanasiasa kwamba yuko upande wao hivyo wasimbanie 2015.

    ReplyDelete
  10. POSHO ZA NYONGEZA KWA WAHESHIMIWA WABUNGE:

    itakuwa na TIJA kama zitatumika kuboresha huduma kwa wananchi wanaowatumikia lakini sio kwa KUONGEZEA WAHESHIMIWA UWEZO WA MATANUZI NA ULEVI!

    ReplyDelete
  11. Askofu anaona mgao kanisani utaongezeka.

    ReplyDelete
  12. ALIYEWAHI KUNENA NI MWENYEZU MUNGU PEKE!!!! HIVYO ACHENI MUNGU AWE MUNGU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...