aslam-alaikum
kaka michuzi sisi wazanzibari tunaoishi canada tunaomba uturushie kwenye mtandao wako wa michuzi salaam za rambirambi kwa wazee wetu waliopoteza maisha yao katika january 12 ,1964 katika mapinduzi ya zanzibar na leo imefikia miaka 48 tokea kuondoka kwao tunamuomba Allah awalaze pema peponi ameen hakika sote tupo pamoja nao na hatutowasahau milele ahsante.
mdau canada

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Nilifikiri Zanzibar wa Canada ni katika Makomredi. Kumbe mnayatambua mapinduzi!!

    ReplyDelete
  2. Mimi si mtaalamu wa historia. Lakini nilisoma kuwa zanzibar ilipata uhuru baada ya uchaguzi huru tarehe 12 desemba 1963. Sasa mbona tena walifanya mapinduzi januari 1964? naomba nielimishwe.

    ReplyDelete
  3. Inna Lillah wa Inayhi Rajiuuunnn!

    ReplyDelete
  4. ndugu unamaanisha nini rambirambi zako,waliouliwa katika machafuzi ya january 1964.
    Imechukuwa miaka 48 kuichafuwa nchi jee kuijenga itachukuwa miaka mingapi ?

    ReplyDelete
  5. mdau wa pili kinachokutatiza ni nini hasa hapo? Hujui maana ya mapinduzi au ni vipi?

    Kwani nchi ikishapata uhuru huwa haiwezekani kutokea mapinduzi baadae katika nchi hiyo hiyo?

    Kama unataka kweli jawabu basi hili ndio jibu. Zanzibar kama nchi tele za afrika na kwengineko kulitokea mapinduzi januari 12 1964 kupindua serikali iliyokuwa madarakani wakati huo. Serikali iliyokuwepo madarakani kabla ya hapo ni hiyo ambayo iliipatia zanzibar uhuru.

    Kwa ufupi Zanzibar ilipata uhuru 1963 na kulifanyika mapinduzi mwaka 1964.

    Kwa taarifa yako tu kuna tafauti baina ya mapinduzi na uhuru na ndio maana Tanzania bara husherehekea uhuru wakati zanzibar husherehekea mapinduzi. Zanzibar inasherehekea mapinduzi kwa sababu walipindua serikali iliyoipatia uhuru zanzibar.

    ReplyDelete
  6. waZanzibari tunaoishi huku Scandinavian country tulifanya sherehe mwezi uliopita za Zanzibar independence 12 Dec 1963.

    God Bless Zanzibar and his Peoples

    ReplyDelete
  7. mbona mwanamapinduzi mwenyewe hatajwi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwanamapinduzi ni John Gideon Okello

      Delete
  8. http://www.youtube.com/watch?v=IE24qenucRY
    angalia hii link utafahamu alichomaanisha

    ReplyDelete
  9. sema ni wewe tu uliyeandika kutoka Canada ndie unayoyatakia Mapinduzi ya Zanzibar kheri....Mimi sitobadilika kuwa mpinzani wa serikali ya Mapinduzi hadi viongozi wetu watakapo punguza ulafi wa mali ya umma.Simchuki mtu kwani tumekatazwa kuchukiana ila nachukia mwenendo na tabia ya wapenda uongozi na ukubwa bila ya kuutumia ipasavyo ktk jamii. Wazanzibar wenzangu hili tuliangalie kwa macho tuliyojaaliwa na Allah.Tatizo si Muungano tatizo ni sura mbili sisi tunazo Wazanzibar kwa manufaa ya matumbo yetu au watu fulani..Watabaruk.

    ReplyDelete
  10. Mtake msitake MAPINDUZI DAIMA!!!

    Aliyepindua:
    Ni John Godeon Okello akishirikiana na WASWAHILI wenzake wa UNGUJA, yaani KARUME NA WENZAKE!

    Aliyepinduliwa:
    Ni WAARABU wote wa UNGUJA wakiwa na majambia yao mikononi huku wakisimamiwa na SULTANI WA OMANI!

    ReplyDelete
  11. Mtake msitake Mwarabu alipinduliwa na kuumbuliwa Unguja baada ya miongo kadhaa ya Utawala wake dhalimu na wakiunyanyasaji!

    Ilifikia watu weusi wakawa wanabaguliwa kama nchi sio yao!

    Hongera Mapinduzi yaliyomjengea Mswahili heshima kufikia kuweza kumuoa mwanamke wa Kiarabu bila taabu chini ya Utawala wa Mwanamapinduzi (Mswahili) ABEID AMANI KARUME!

    ReplyDelete
  12. Nyundo inapotua hakuna kinachobaki matunda ya CCM ni kuanzia Mapinduzi Unguja!

    ReplyDelete
  13. Watu weusi wanabaguliwa hata sasa angalia maendeleo gani yamepatika miaka 48 ya mapinduzi nchi imerudi nyuma mika 58,hao hao mliowapinduwa na kuwabaguwa na bado mnashikilia kuwaowa kwanza mliwakamata kwa nguvu na kutaka kuzaa nao watoto wenye nywele za singa na rangi nyeupe.baniani mbaya kiatu chake dawa.wacheni kasumba zenu hizo za kijinga.

    ReplyDelete
  14. Anonymlous wa Sat Jan 14, 08:50:00 PM 2012

    Watu weusi wanabaguliwa...kuwaowa Wanawake Weupe,

    Asalalee wewe Mdau usisikie Mwanamke Mweupe licha ya nywele laini,ngozi laini na rangi, suala ni manjonjo na joto tu wananoga sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...