Rais wa Zazibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kwenye  Uzinduzi wa Barabara ya Chanjamjawiri-Tundauwa,kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi na Shirika la misaada la Norway (NORAD),ikiwa ni katika shamara shamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,( kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Barabara ya Chanjamjawiri-Tundauwa Pemba,kwa  mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi na Shirika la misaada la Norway (NORAD),ikiwa ni katika shamara shamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa iundombinu na Mawasiliano hamad Masoud Hamad,(kutoka kulia) Katibu mkuu wa Miundombinu na Mawasiliamo,Dk Lila Vuai Lila,Naibu Waziri wa Wizra ya Miundimbinu,Issa Haji Ussi na
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Igun Klepsvik.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akitembea katika barabara ya Chanjamjawiri-Tundauwa,,akifuatana na Waziri wa Miundombinu ,Mawasiliano,Hamad Masoud Hamad,(wapilimkushoto) na Balozi wa Norway Nchini Bibi Igun Klepsvik, watatu kulia) baada ya kuifungua rasmi,barabara hiyo iliyojengwa kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi na Shirika la misaada la Norway (NORAD),ikiwa ni katika shamara shamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais wa Zazibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono wananchi katika sherehe za Uzinduzi wa Barabara ya Chanjamjawiri-Tundauwa,iliyojengwa kwa mashirikiano kati ya Serikali a Mapinduzi na Shirika la misaada la Norway (NORAD),katika uwanja wa Faya chanjamjawiri Pemba,ikiwa  katika shamara shamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Pemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Norway ndio nchi za kuishi,nchi tajiri kinoma.Ukifumania bingo hapo Norway,maisha yanakuwa poa kabisa!

    ReplyDelete
  2. Wewe Mdau wa kwanza Norway ndio mahala pa kuishi!.

    Usisikie ndugu yangu hizi nchi ni vile Mabunge yao yanaongea kwa lugha zao kama ungejua wanachojadili na kutumia muda mwingi ni juu ya Agenda ya kuwabana Wageni kuingia na waliokwisha ingia nchini kwao!

    ReplyDelete
  3. mdau unasema tu, lakini kumbuka gharama za maisha ziko juu sana Norway hivyo watakulipa pesa nzuri ila zote zinarudi kwenye mzunguko, tax, kodi ya nyumba nk.
    sio rahisi kama unavovikiri, ila bora kuliko bongo anyway ambako mpaka uibe.

    ReplyDelete
  4. Mungetuonyesha hiyo barabara tukaiyona vizuri, na kama ndio hiyo anayopita Mh Rais basi nitasema ni ulimi wa nyoka

    ReplyDelete
  5. Maisha sio rahisi kiivyo mdau. Kwanza kuna ile iferiority ya ugeni, pili hali ya hewa ni mbaya kwa ujumla na tatu, kipato kinatosha tu kuishi, maana fedha unayopata inaishia kwenye nyumba, kodi na mazagazaga kibao! Ila mazuri pia yapo...utii wa sheria, huduma nzuri za jamii kama afya, nishati nk

    ReplyDelete
  6. Nadhani badala ya kuishi Norway au kuugundua uzuri wa kufanya hivyo, ni vyema tukajifunza kuwa wao walifanya nini kufikia hapa mahali walipo? Miaka 50 iliyopita hawakuwa hata na harufu ya mafuta lakini walipoyapata walichangamka na kuwatoa wataalamu wa kimarekani ki ujanja na wazawa kudaka nafasi za ujuzi wa uchimbaji mafuta. Leo mambo ndiyo hayo...watu chini ya million 5 wanatoa misaada karibu dunia nzima...nchi isiyo na deni lolote duniani-Norway.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...