Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wametanda na magari yao sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo baada ya wanafunzi zaidi ya 80 kusimamishwa na wengine zaidi ya 10 kufukuzwa baada ya Uongozi wa Chuo hicho kukutana na kutoa maamuzi kutokana na mgomo na uvunjaji wa sheria uliofanywa na wanafunzi hao.
Home
Unlabelled
FFU wakiwa kwenye maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


hawa watoto wanatumiwa na nani na kwa faida ya nani?
ReplyDeleteWewe namba moja kwanza nikutakie mwaka mpya.Pili, umepita chuo kweli wewe?Kama umepita basi ww utakuwa walee......
ReplyDeleteDavid V
hawatumiki kwa mtu yeyote maana kwa namna moja ama nyingine wanaonewa hii fukuza fukuza uangalie na madai yao plz serikali tatua hili mapema
ReplyDeleteKichwani hamna kitu ni wavivu wa kusoma ndiyo maana ikifika kipindi cha mitihani basi wanashabikia migomo.
ReplyDeleteVijana jitahidini musome wacheni ibilisi huyo hatowafikisha popote. Au mulinunua mitihani ya A level?
we mdau una maana gani?
ReplyDeleteKwani hawana demokrasia ya kuzungumza au kuandamana?
Au wewe umetumwa??
MDAU WA JUU UNAULIZA NINI? HAO WANAFUNZI WANATAFUTA HAKI YAO YA MSINGI KWANI WEWE HUJUI?
ReplyDeletehawatumiwi na mtu yoyote, akili zao finyu tuu. Wao wanadhania migomo/vurugu ni kipimo cha kuelimika na pia wanadhania duniani kote hivyo ndivyo wanafunzi wa chuo kikuu wanavyofanya.
ReplyDeleteKwa nini unafikiria wanatumia. Hiyo ndio hali ya vyuo vikuu tangu enzi za mwalimu!!
ReplyDeleteKma mtu umepitia pale chuoni basi hutauliza hayo maswali ya ajabuajabu, wanatumiwa na nani?Nyinyi watanzania ndiyo mna akili finyu, wasomi wanaona mbali na wanapotaka haki zao na kuwatetea nyinyi watanzania, basi nyinyi huwa munawasema na kuwasaliti, halafu huku nyuma kimya kimya na kwa uoga mnaendelea kuilaumu serikali.waacheni wao wanajua haki yao na wana uhuru wa kuzungumza hadharani siyo kam wewe mdau no. 1 na wenzio.kalagabaho!!!!!
ReplyDeletemdau Semkiwa
Hawa wanbafunzi sio wendawazimu! wana agenda ya nguvu bali Wakuu wa chuo ndio tatizo kwao! wawasikilize then watatue tatizo na sio kuwanyamazisha kwa style hiyo!
ReplyDeleteWakumbuke kuwa siku zote UKWELI UNAUSHINDA UONGO.
MTUMIKIE KAFIRI UPATE MRADI WAKO!!!
ReplyDeleteHawa wanafunzi wangeijua busara hii yote haya yasingewafika.
Wangestahimili wasome wamalize halafu huo upinzani wao waulete wakiwa na shughuli zao wakijitegemea, kuliko hivi sasa wame haribiwa kabisa dira za maisha yao.
Angalia sasa umeshafukuzwa Chuo kilichobaki ni kuingia Mtaani Kuendesha Bodaboda, Kuwa Vinyozi katika Saluni, kufanya Umachinga na Kuchoma mahindi!
kwanini kuwahukumu kwa mazingira binafsi amabayo ni tofauti na yao? mi nadhani wangesikilizwa madai yao, afu uelewe system ya chuo ilivokaa ndio uweze kuwahukumu hawa.. si kukurupuka tu na kulaumu kwa maneno ya dharau bila kujua kipi kinawasibu.
ReplyDeletemfano, unakuta mtu anapita na gari, kamwona mtu kalala kituoni (homeless) anaanza kashfa, si angerudi kujijini kwao.. jambo jema ni kuuliza kafikaje hapo, si kuchukulia mazingira yako unayaweka kwake!! hawa wanafunzi kuna kitu kimewapelekea hapo, tukumbuke wamepita toka chekechea bila kufukuzwa, kwanini ije chuo kikuu? tena ambacho migomo ni karibu kila mwaka?
kwa sie tuliopita chuo hatuwezi kuuliza maswali hayo mnayouliza baadhi yenu hapo juu,chuo hupati haki yako kwa njia ya demokrasia. Miaka yetu sie tuligoma na kuandamana kudai stationeries na sehemu za kusomea(vembwete) viongezwe,na ada za shule za msingi zitolewe,watu walitusema hivyohivyo km hapo juu,tukafukuzwa chuo,baadae tulirudishwa kwa barua maalum,wengine wakawa wamefukuzwa kbs,tukagoma tena,wakarudishwa kwa masharti warudie mwaka,lkn walirudi. Lakini yote yalifanyiwa kazi,vimbwete viliongezwa vya kumwaga,na serikali ikatangaza kuondoa ada za shule za msingi. So mkiona wanafunzi vyuoni wanaandamana/kugoma msidhani hawana akili.
ReplyDeletenyie mnaongea tuu hamjui serikali jinsi imeoza unafikiri wao niwajinga kugoma,we mdau kichwa chako kimejaa maji wewe,chuo chenyewe hujasoma paka wewe unajiropokea,nimesoma pale shida tupu mpaka nimemaliza nilishukuru maana hakuna haki hata kidogooooooooo we hujui uozo uliopo pale nyamaza tuu kuku mgeni wewe
ReplyDeleteHawatumiwi na mtu yeyote ile ni kuiga ya waliopita ya kuwa lazima kuwe na migomo. Mimi nimesoma hapo wapo wanafunzi ambao lengo lao sio kusoma bali ni kutafuta chokochoko kama mlisoma kuanzia nursery, std 1-V11 english media na o'level ampaka A'Level shule za international mnachodai nini hao wazazi waliokuwa wanalipa hizo ada miaka yote walikuwa wanazipata wapi? Iweje wasizilipe sasa. ACHENI HIZOOOOO SOMENI NDIO MAANA MAJORITY YA GRADUATES HAMPATI KAZI VICHWANI HAMNA KITU TUNAONA MKIJA KWENYE INTERVIEW HATA LUGHA HAIPANDI SWALI LA KIZUSHI MNASHINDWA. KILICHOWAPELEKA NI ELIMU NASIO MIGOMO. MKIKASIRIKA JUU YENU NA UKWELI UNAUMA.
ReplyDeleteby
mdau wa elimu
Hao ni wale walionunuliwa mitihani ya A'level kabisaaaaaaaaaaaa aliesugua msuli huwezi kumkuta anaandamana komeni kabisa.
ReplyDeleteSerikali iwatatulie na kusikiliza matatizo yao fukuzafukuza sio dawa kabisa hawa ni vijana wetu tukae nao chini tuongee; serikali itakuja ona hasara ya hii fukuza badae kwani taifa la Tanzania litakuwa la vijana wengi na mbumbumbu. Elimu ni hitaji la msingi kwa kila mtu.
ReplyDeleteOmbi langu kwa Mheshiwa Rais hebu mtoe huyu bwana Prof Mukangara tuone chuo kitakavyo kaa sawa maana ameshindwa kazi kabisa.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa ndio maana weng wenu mnalaumu msichokijua kaz mnafuata upepo wa viongoz wa serikali wanaodhan kila ukigoma eti sabab za kisiasa au oo wametumwa na chama fulan.Achen mawazo yenu finyu kama wenye akili timamu
ReplyDeleteKwa nini wagome? Wanadai haki zao. Bodi ya mikopo inatoa fedha lakini kupewa wanafunzi inakuwa tabu. Kwa nini wawape pesa mpaka waandamane. Serikali isiangalie upande wa wanafunzi tu iangalie na uongozi kwa nini kuwe na migomo mara kwa mara? Sababu watu wamezoea ufisadi wanataka kufisidi mpaka hela za wanafunzi. Timizeni mambo wanyostahili muone kama watagoma. Kama baba anapata hela na anaishia kulewa na vimada tu watoto wanahangaika tu. Siku wakimkuta na vimada wake wakamcharaza bakora mtawalaumu? Serikali itafute chanzo cha migomo isibaki kusingizia kwamba wanatumiwa.
ReplyDeletematatizo ya migomo yanasababishwa na watawala yaani serikali au wakuu wa vyuo. Kwa nini wanashindwa kukaa na kuongea na hao vijana, wanaogopa nini kama wao wako sawa. Kwa sasa Tanzania inanuka kwa migomo kila mahali mpaka watoto wa chekechea na wao watagoma ni aibu. Halafu wakigoma kidogo jeshi la polisi liko kuwatwanga mabomu hivi huko nyumbani hao ma FFU hawana kazi nyingine ya kufanya ya maendeleo.Serikali na watawala mjifunze jinsi ya kuongea na hao watoto wenu kuwafukuza vyuo sio tija ni kuongeza matatizo katika nchi.
ReplyDeleteJAMANI EBU TULIZENI MIGOMO HAPO UDSM KWANI INA HARIBU REPITATION YA CHUO KABISAAAA....
ReplyDeleteSIKU HIZI AKIJA MWANAFUNZI WA UD KUOMBA KAZI SIWEZI KUMPA SABABU NA MOTIVATE MIGOMO MPAKA MAOFISINI MFANO MZURI ANGALIENEI CBE.. WALIO LECTURES WENGI NI GRADUATES WA UDSM NA NDO MAANA KILA KUKICHA MARA WALIMU WAMEGOMA... please ata zuieni media isi report migomo yenu.. shauri yenu
Urasimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umezidi. siwezi semea vingine manake sijavisoma ila UDSM kama hujapapita ndio unaweza ukawalaumu vijana.
ReplyDeleteKWAKWELI ANNOUN JAN 11,03:28: PM 2012 Ninakuunga mkono kabisa CBE haikuwa hivyo yote yanatokana na walimu waliotoka UDSM, niligraduate pale CBE ADA 2004 tangu nilipoingia chuoni hapo hapakuwahi kutokea migomo mambo yote tulikuwa tunayamaliza COBESO wote tulijua kilichotupeleka pale ni Elimu tu. Lakini siku hizi eti lecture anagoma what is this uliposain mkataba ulisemaje au kwakuwa ulikuwa na njaa ya ajira? Kwa ufupi mimi ni Chief accountant mara panapotokea vacancy huwa ninaondoa wote waliotoka UDSM, mara nyingi huwa tunawachukuwa wale waliomaliza TIA,Mzumbe,na wa CBE most of them are intelligent.
ReplyDeleteUSISHANGAE UMEMALIZA UDSM NA UNAENDELEA KUTESEKA HATUWATAKI KWA TABIA ZENU MNAZIAMBUKIZA MPAKA MAOFISINI.