Na Mary Ayo-Arusha
HATIMAYE jambazi Pokeaeli Samson Kaaya au Kaunda lilokuwa likisakwa
na Jeshi la polisi mkoani hapa ambaye alifanya tukio tarehe 03
january la kumjeruhi Afisa wa polisi ASP.Faustine Mafwele pamoja na
kumuua askari EX.F.2218D/C KIJANDA kwa kumpiga risasi shingoni
ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi usiku wa
kuamkia leo katika kijiji cha orarashi wilayani Arumeru.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Thobias Andengenye amesema kuwa polisi kwa kushirikiana na wananchi
waliendelea kumfuatilia jambazi huyo kwa karibu ambapo jana majira ya
saa nane usiku polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuzingira
nyumba ya ya Anna Roshirari.
Andengenye alieleza kuwa majira ya saa 06.45 asubuhi gafla jambazi
huyo ailchomoka ndani ya boma hilo na kuanza kukimbia ambapo askari
walimfukuza umbali wa kilometa mbili ambapo jambazi huyo ailimgeukia
gafla askari namba E.9912d/c WITO aliyekuwa karibu kumkamata na
kumvamia ambapo ailimjeruhi jichoni pamoja na kumuuma kidole gumba.
Kamanda aliendelea kudai kuwa askari wenzake walifika na kumpiga
risasi jambazi huyo kwa lengo la kumpunguza nguvu ndipo gafla
alianguka chini na kufariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini.
Hataivyo andengenye amesema kuwa jambazi Kaunda alifika kwa anna
Roshirali kwa lengo la kutibiwa kwa mganga wa kienyeji jeraha
ililokuwa amejeruhiwa mguuni siku ya tukio kwa kuhofiwa kutibiwa
hospitali kwa kuwa alikuwa ansakwa na jeshi la polisi.
Pia amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha
alizokuwa akitumia marehemu huyo kuwa ni pamoja na SMG No 1016188011
, risasi 20,Shortgun Moja yenye Model 88-12GA,risasi nne ambapo
zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa salvet na kufichwa kwenye
kichaka.
Aidha Bw Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo watu wanne
wanashikiliwa na jeshi la polisi ambapo watu hao ni pamoja na mke wwa
marehemu Agness Silas(40), Josephat Haule(33),Juma Salum(46},pamoja
na Dainess Masawe(19).
Vilevile jeshi la polisi linawasaka washiriki wa kaunda ambaye mmoja
wapo ni Augusti Shine au Baba Mzungu mkazi wa sakina juu.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru.


Jambazi :Pokeaeli Samsoni Kaaya-Kaunda, ni sawa kwa kupigwa risasi bora atangulie aende kuzimu na hata kama angekamatwa akiwa hai ingefaa afungwe Maisha afie Gerezani!
ReplyDeletePana umuhimu kutoa Semina Elekezi kwa Majambazi na Wahalifu nchini kuendesha maisha kwa mipango mingine kwa kuwa sasa Jamii imeamka na inatoa ushirikiano kwa Mamlaka ni vile UHALIFU HAUKUBALIKI KABISA!
Kamanda aliendelea kudai kuwa askari wenzake walifika na kumpiga risasi jambazi huyo kwa lengo la kumpunguza nguvu ndipo gafla alianguka chini na kufariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini.
ReplyDeleteJambazi alikuwa amejeruhiwa mguuni, lakini walikimbizana na polisi kilometer mbili??????
ReplyDeleteAngekuwa Hans jeraha sidhani kamalla wangemshika!
Deletemtu anayeibiwa kwa jeraha la mguuni anaweza kukimbia kweli? e
ReplyDeleteYote hii ni style ya kuieleza jamii kuwa hawakuwa na dhamira ya kuua, ila ukweli ni kuwa kuwa ilikuwa lazima wamuue tu.
ReplyDeleteTatizo tulilonalo ni kuwa jeshi letu linawafahamu wahalifu wote, ila kwa kuwa kuna wenzao wanashirikiana nao ndio inakuwa ngumu kuwaangamiza, ila wakiguswa wenyewe ndio utawajua, ila ingekuwa raia kauwawa ingesikia bado tunachunguza. Tubadilike ndugu zangu.
Maelezo hayajitoshelezi,jeraha mguuni mbio kilomita mbili???????????????????
ReplyDeleteHongera sana jeshi la polisi Arusha na wananchi mlioshiriki kikamilifu kulisaka jambazi hilo sugu ambalo tayari lilimuua kijana wa watu Kijanda! Binafsi sijali amekufa kwa staili gani, muhimu kwangu amedhibitiwa kabla hajaua wengine wasio na hatia! Moto huu wa polisi inabidi uimarishwe zaidi badala ya kutafuta legal technicalities za kifo cha jambazi hilo!!! Kamanda umejitahidi kueleza. Inatosha hata kwa kuweza ku-recover silaha.
ReplyDeleteUtata Mtupu! Hata hivyo Hongera kwa kummaliza huyo jambazi. Heri hii kuliko askari wetu kuuwawa kwa uzembe wa jinsi ya tukio lile la kwanza.
ReplyDeleteKatika dole la mguu kisha simba atokee uone kama atakukamatia hapo alipokukuta
ReplyDeleteHivi jeshi la polisi lina kikosi maalum cha kukabiliana na kudhibiti ujambazi? Nawapa hongera sana, ila kwa upande wa kudhibiti ajali wananichisha kabisa! Said Mwema, kazi nzuri ila sawazisha kote kote!
ReplyDeleteWe hii mijambazi huijui uwa inatumia na madawa unakuta linatoka midamu kila sehemu na bado lina nguvu za kukimbia. Haitaki kufa ili iendelee kuua wengine. Wakipunguzwa hivi afadhali hata kama alikuwa hakimbii hawezi kuamka kujitolea ushahidi, alale tu.
ReplyDeleteEti...mjomba jambazi kauwawa?!
ReplyDeleteHizo bunduki walizozikamata ndiyo moja ilitumika kumuua yule Polisi? Na kama ni hizo mbona ni kubwa na zinaonekana. Mtu ana silaha halafu bado unataka kumkamata. Haya ni maajabu. Mhalifu akishakuwa na silaha siyo wa kuweka majadiliano naye ni kumnyang'anya uhai (kumuua) tu. Nilitegemea wangekamata na bastola ambayo ni ndogo na haionekani kwa urahisi. Hapa ninakuwa na mashaka na kwamba yule polisi aliuawa na jambazi bali ni wale wenzake walipoona jambazi linawaacha wakaamua kulipiga risasi bahati mbaya ikampata mwenzao. Ili wasionekane wazembe wakatoa maelezo kuwa jambazi lilimpiga risasi shingoni alipotaka kulikamata. Walipoona mwenzao wamempiga risasi walipatwa na butwaa hata hawakuendelea tena kulifukuza lile jambazi. Mbona wamechukua muda mfupi tu kulipata mafichoni mwake? Halafu risasi ya kumpunguza mhalifu ambaye hana silaha ili asikimbie inapigwa kwenye viungo vinavyomfanya akimbie spidi (miguu). Sasa wao walipiga wapi? Nataka kuamini kuwa angetoa siri za kuuawa yule polisi na jinsi ambavyo amekuwa akiwapa mgao polisi kwani Polisi wanayajua majambazi na mitaa wanayoishi. Insp Said Mwema angalia watendaji wako watatumaliza.
ReplyDeleteSioni sababu ya mtu kuwa na taarifa nyingi za Ujambazi halafu asiuwawe!.
ReplyDeletePOLISI IMEFANYA KAZI NZURI HAKUNA SABABU YA KUIELEZA JAMII MENGI KAMA HUYU MTU ANA REKODI YA MATUKIO YA UJAMBAZI NI HAKI YAKE KUPIGWA RISASI NA KUUWAWA!