Rais Dkt. Jakaya kikwete akiwa na Waziri wa Uvuvi, Maliasili na Bunge wa Gambia na Mjumbe Maalumu wa Rais Yahya Jammeh, Mh Lamin Kaba, ambaye kamletea ujumbe toka kwa Rais huyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya kikwete akipitia ujumbe kutoka kwa Rais wa Gambia,Mh. Yahya Jammeh alioletewa na Waziri wa Uvuvi, Maliasili na Bunge wa Gambia Ikulu jijini Dar es salaam leo.Picha na IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Jumatatu, Januari 9, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais wa Gambia, Mheshimiwa Yahya A. Jammeh.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, mjumbe huyo maalum, Mheshimiwa Lamin Kaba ambaye pia ni Waziri wa Uvuvi, Maliasili na Masuala ya Bunge amemkabidhi Rais Kikwete ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jammeh.

Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete na Mheshimiwa Kaba wamezungumzia masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Gambia na pia masuala ya Afrika na ya kimataifa.

Mjumbe huyo maalum anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Nairobi,
Kenya ambako anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais
Ikulu,
DAR ES SALAAM
Januari , 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mbona amefanana na Muheshimiwa LIKWELILE!?!

    ReplyDelete
  2. Waziri wa Uvuvi, Maliasili na BUNGE??? Hawa watu wa Afrika magharibi hawa, JK kuwa macho, usikute hapo leo umeokotwa peupee.

    ReplyDelete
  3. Jk Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kukupa busara za subira.wangekuwa wengine ndio wameshika nchi tungekuwa tumekwisha chinjana.

    ReplyDelete
  4. Natumaini Rais wangu umemweleza wazi akamwambie bosi wake aache mauzauza na pia aruhusu demokrasia ya kweli. Kama hujamweleza hayo kwangu mim chochote kingine mlichoongea ni BATILI!!

    ReplyDelete
  5. Namkumbuka babu yangu JK Nyerere alivyokuwa anasema IKULU SI PAHALA PA KUKIMBILIA sasa nimeamini Jakaya alikuwa bonge la HB lakini sasa hivi kwishnee kweli urais kazi bora angebakia kwenye uwaziri wake!

    ReplyDelete
  6. jakaya waangalie hao watu wa west..kwanza wachawi hao hasa wagambia.

    ReplyDelete
  7. Hatutaki hao matapeli wa afrika magharibi watauza mpaka IKULU, shauri zenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...