KAKA MICHUZI HABARI ZA KAZI ...NAOMBA UNIWEKEE HAKA KAHABARI CHANGU KAZURI NA KA CHAKUFURAHISHA KWA WAPENZI WA ARSENAL  NA CHA KUCHUKIZA KWA WALE WAZEE WA BWAWA LA MAINI NA MASHETANI WEKUNDU.

BRO WETU KACHOGO AMERUDI NA VITU VYAKE NADHAN KILA MTU AMEPATA KUVIONA AKIWA NDO KWANZA MECH YAKE YA KWANZA TANGU AREJEE JANA USIKU AMBAPO KAMPIGA LEEDS BAO MOJA
KATIKA FA CUP.

BIG UP SANA BRO THIERRY HENRY...TUNAKUKUBALI SANA WASHABIKI WA ARSENAL. ULIVYOONDOKA ARSENAL PIA TULIKUA TUNA KUHESHIMU NA SASA BADO PIA TUNAKUHESHIMU NA BADO TUTAKUHESHIMU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. MashaAllah na ndevu za Sunna kafuga

    ReplyDelete
  2. Sasa Uchogo huyooo,,,bado Fernando Torres kurudi kundini!!!

    ReplyDelete
  3. Vijana wa arsenal jifunzeni toka kwa kaka yenu ili starehe iendelee!!!

    ReplyDelete
  4. Naona Henry kaacha kutumia vinyoleo vile anavyovitangaza, teh teh teh. Hongera zake

    ReplyDelete
  5. Kwa kurudi kundini, Assalam Alaykum zako Ustaadh Thiery Henry!

    ReplyDelete
  6. Pure magic it was
    If Henry had written the script himself with help of Hollywood, it would not have been as dramatic.And scoring a goal when he did, the icing on the cake.Its now 227+1 and counting

    ReplyDelete
  7. Hii midevu ilikuwa ni fesheni kwa wanasoka miaka ya 70. Nakumbuka wachezaji kama Gerd Muller, Paul Breitner, Socrates na wengine wengi maarufu walikuwa na midevu.

    ReplyDelete
  8. Mujuni aka Mpoki upo? naona mzee kichogo kakuiga kufuga midevu! badala kufuga ng'ombe akiwaudhi hata mkimchinja mnapata faida,nyie mmekazana tuu na midevu yenu!

    ReplyDelete
  9. Siku zote nasema kucheza mpira sawa na kundesha baskeli tu,mtu huwezi kusahau,hawa wa kwetu hapa matatizo yamewajaa na wala sio hawana ujuzi ebu fikiria leo hii mtu kama Annuar Awadhi eti nae veteran!

    ReplyDelete
  10. kuna wakati nilisoma kuwa Hendry amekuwa muslim hebu tugoogle labda ni kweli na ndo sababu ya hizo ndevu.

    ReplyDelete
  11. Henry,kanute,Anelka,Frenk reberry walıkubalı uislam kaka na nimaustadhii..we kaa 2 na kukandia midevu vijana ulaya na marekani wanakubali sanaa uislam..mtazame loon wa bad boyz..

    ReplyDelete
  12. Henry ni muislam kama alivyo Van persie,Frank Libery,Anelka.etc.

    ReplyDelete
  13. Nicholas Anelka ndiye muslim. Hii ya Thierry kuwa muslim sijawahi kuisikia.

    ReplyDelete
  14. Goli la "offside"!!

    ReplyDelete
  15. Thieny mimi ni kati ya forward ambao sipati wa kumfananisha na ukiondoa kina PELE, MARADONA na EUSEBIO,hongera sana kaka wafundishe vijana kazi,Wenger mchukue jamaa awafundishe maforward wako butu (Shamakh na Geovinho)

    ReplyDelete
  16. Henry ni Muislam jaribu ku google utaona hilo halina shaka kama alivyo Van Persie, bacary Sagna etc.

    ReplyDelete
  17. Van Persie siyo muislamu na amewahi kukataa "live" kwenye TV kwamba yeye siyo muislamu. Mke wake ni muholanzi mwenye asili ya morocco, na ndiyo kisa cha watu kudhania kwamba yeye ni muislamu. Amewahi kusema kwamba yeye si muislamu na wala si mkiristo.

    Fredy Kanoute baba yake anatoka Mali. Mali ndipo ilipo Timbuktu. Kwa hiyo Kanoute kuwa muislamu ni sawa na kusema Mutayoba au Rugambwa kuwa mkiristo.

    Nicholas Anelka na Franck Ribery ni kweli walisilimu na kuwa waislamu.

    Thierry Henrry sijasikia.

    Huu ni ushahidi tosha kwamba america propaganda machine against islam isn't working so good.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...