Kampuni inayokua kwa kasi ya DARLET inayomilikiwa na Vijana wa Kitanzania mwishoni mwa wiki iliyopita iliandaa mafunzo yanalolenga zaidi sekta ya kibenki yahusuyo PAYMENT CARD INDUSTRY DATA SECURITY STANDARD (PCI DSS). Vigezo hivi vya PCI DSS vitakuja kuwa muhimu kwa watendaji wa mabenki kuvitumia katika mifumo ya malipo ndani ya benki katika siku za usoni. Benki zilizohudhuria ni pamoja na EXIM, DTB, NMB, FBME na CRDB. Bila shaka muitikio haukua mkubwa sababu bado ni mahitaji mapya ndani ya soko/sekta ya kibenki na ni mafunzo ambayo ndio kwanza yamefanyika kwa mara ya tatu ndani ya Bara la Afrika ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania. Mafunzo haya ya siku Mbili (2) yalifanyika Dar es Salaam International Conference Center (DICC). Karibu utembelee www.darletgroup.com uone jinsi gani tunaweza tatua changamoto zako katika Ulimwengu wa Teknolojia.
Dr. Abiola Abimbola (Phd & QSA)
Mkufunzi na Mmiliki wa Kampuni ya NetHost Legislation (UK) Ltd iliyojikita nchini Uingereza na ambayo iliingia ubia na Kampuni ya Nyumbani ya DARLET kutoa mafunzo haya ya PCI DSS Nchini Tanzania.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DARLET Bw. Gilbert Kapya katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni kutoka Uingereza ya NetHost Legislation (UK) Ltd Dr. Abiola Abimbola.
Washiriki wa Mafunzo ya PCI DSS na Wafanyakazi wa Kampuni ya DARLET katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Bw. Baraka Magayo (Mshiriki kutoka FBME), Bw. Glen Kapya (Mmoja kati ya Wakurugenzi wa DARLET), Bw. Abdulrabih Nyoka (Mshiriki kutoka NMB), Bw. Geofrey Odero (Mshiriki kutoka DTB), Bi. Kabula Mashala (Mshiriki kutoka CRDB), Bw. Gilbert Kapya (Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DARLET), Dr. Abiola Abimbola (Mkufunzi na Mmiliki wa Kampuni ya Nethost Legislation), Bw. Manfredy Kayala (Mshiriki kutoka EXIM) na Bw. James Njiu kutoka DARLET.
Mafunzo Yakiendelea katika moja ya kumbi za DICC
Mafunzo na majadiliano yakiendelea kwa njia ya vitendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. kuna yeyote mwenye kuijua official website ya kampuni hii ya nethost legislation? nime google bila mafanikio. mwenye details naomba anipatie kupitia email hii iammwale@gmail.com

    ahsanteni sana

    ReplyDelete
  2. Wana address ya 42 Adolphus Road, Finsbury Park, London N4 2AY. Google map wanasema barabara hiyo iko Hackney. Line of business ni Miscellaneous Computer Services. Hawana website ambacho ni kitu cha ajabu kwa UK businesses. Trainer jina lake ni Dr. Abiola!!!

    ReplyDelete
  3. http://www.nethostlegislation.co.uk/

    ReplyDelete
  4. Visit the following links:
    www.nethostlegislation.co.uk

    PCI Approved Companies: Learn more here!
    www.pcisecuritystandards.org

    Go to 'Approved Companies & Providers' tab, then chech on QSA link

    ReplyDelete
  5. This is such constructive development in IT security for Banking services.Keep this up Darlet!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...