Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu' akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa dini ulioandaliwa na kanisa la FPCT kwa ajili ya kuliombea Taifa ambapo mbunge huyo aliwataka wananchi wajiandae kutoa maoni yao kwa tume itakayoundwa na rais jakaya kikwete ya marekebisho ya katiba.



 Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly Of God (TAG) Mch. Yohana Tindika wa kanisa hilo la Mazinde (Kushoto), akimuombea Rais Jakaya Kikwete kupitia picha waliyoishika kwenye mkutano wa kuliombea Taifa uliofanyika mjini Mombo. wengine ni Askofu wa kanisa la FPCT Askofu Davie Mulenga na anayemfuata ni Mchungaji John Mitindo.
Askofu wa kanisa la FPCT askofu Davie Mulenga (kulia) akiwa ameshika bendera ya Tanzania kuliombea Taifa baada ya kumalizika miaka 50 ya Uhuru na nchi kuwa na amani hivyo walitumia mkutano huo kuliombea taifa ili miaka mingine 50 ya uhuru taifa lisiingie matatizoni, wengine walioshika bendera hiyo ni viongozi wa kata ya Mombo wa Chama Cha mapinduzi akiwemo Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu'. 

Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Assembly of God (PAG) la mjini Mombo Mch. Peter Mgonja (Kushoto) akiombea viongozi wote wa Tanzania kwa kutumia ramani ya nchi yetu kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya benki katika mji mdogo wa Mombo. wengine kulia ni Askofu wa kanisa la Free Pentecostal Of Tanzania, askofu Davie Mulenga ambaye ndiye mratibu wa mkutano huo wa kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake baada ya kumalizika miaka 50 ya Uhuru.Picha zote na Mashaka Mhando wa Globu ya Jamii




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. MTSCHEEEEEEEEEWWW!!!!!
    UNAIJERIA MTUPU....

    ReplyDelete
  2. Fanyeni kazi ya kuliombea taifa. Nchi yetu inaelekea pabaya sana sababu ya wachache wenye tamaa ya madaraka kwa manufaa yao binafsi, marafiki zangu.

    ReplyDelete
  3. Wanamwonyesha Mungu vitu anavyoona kuzidi wao. Hawaamini uoni wa Mungu, wao waseme tuu ee Mungu ibariki tz naye anajuwa kila kitu kuhusu ukweli na uongo wa tz ikiwemo ufisadi unaolelewa ukuwe zaidi.

    ReplyDelete
  4. MAKUBWA PROFESA MAJI MAREFU KWENYE MADHABAHU YA WOLOKOLE HAOGOPI AU HAWAOGOPI HIZO SALA ZILIELEKEA KWA MUNGU WA PROFESA MAJI MAREFU AU WA WALOKOLE?

    ReplyDelete
  5. dah sisi wa Afrika tuna Imani kali sana,lakini huwa najiulizagaa,dini hizi hizi zililetwa na hawa jamaa waliotutawala na kufanya biashara ya Utumwa zaidi ya karne nzima,mbona bwana aliwaachia tu hawa jamaa, au ndo kusema alitaka nasie twende Ulaya??
    Nakumbuka mara ya mwisho tulikesha pale Taifa kuomba mvua,na sasa?
    hivi jama,imefikia wakati wakuamini sayansi,uwajibikaji na nguvu kazi au tuendelee kumtegemea sir God?inategemea nchi zilizoendelea zile omba kweli kweli sasa nasie twafata mfano.

    ReplyDelete
  6. Mkiomba kwa Imani kwa kutumia jina la Mungu mtapata/mtapokea.

    ReplyDelete
  7. Hawa wamepagawa period!

    ReplyDelete
  8. nina wasiwasi haya maombi yanaweza kuwatia viongozi wetu wakuu wendawazimu

    na huyo maji marefu eti ni mbunge namkumbuka alipokuwa akidandia magari yanayoenda mnadani na badae akajihusisha na uganga na leo hii amegeuka kuwa mbunge ama kweli kuwa kiongozi tanzania huhitaji elimu ni umaarufu tu

    hapo ndipo utakapoona kuwa tanzania ni kama gari linaloendeshwa na kipofu.

    mkoa wangu kaeni mkao wa kula nakuja huko mnipe kura zenu niwajibike bungeni.

    ReplyDelete
  9. grow up people

    ReplyDelete
  10. mipango mibovu haina uhusiano na maombi ya kanisani au msikitini

    ReplyDelete
  11. HI KWANZA NINGEPENDA KUTOA PONGENZI KWA HAO WANO JIITA WAZEE WA KAZI HALAFU NA MHESHIMIWA NAIBU BALOZI KWA KUENDELEZA MFANO MZURI ULIOANZISWA NA WATANZANIA WA UHAIBUNI WA KUKUSANYA MISAADA KWA AJILI YA WATU WALIO ASIRIKA NA MAFURIKO, HAO WATU WANAO ONGEA VIBAYA NINA UHAKIKA HATA NDALA HAWAJAJITOLEA ATI KWA SABABU WAO MAFURIKO HAYAWAHUSU KWA SABABU WANALISHWA NA KWINI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...