Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu' akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa dini ulioandaliwa na kanisa la FPCT kwa ajili ya kuliombea Taifa ambapo mbunge huyo aliwataka wananchi wajiandae kutoa maoni yao kwa tume itakayoundwa na rais jakaya kikwete ya marekebisho ya katiba.
Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly Of God (TAG) Mch. Yohana Tindika wa kanisa hilo la Mazinde (Kushoto), akimuombea Rais Jakaya Kikwete kupitia picha waliyoishika kwenye mkutano wa kuliombea Taifa uliofanyika mjini Mombo. wengine ni Askofu wa kanisa la FPCT Askofu Davie Mulenga na anayemfuata ni Mchungaji John Mitindo.
| Askofu wa kanisa la FPCT askofu Davie Mulenga (kulia) akiwa ameshika bendera ya Tanzania kuliombea Taifa baada ya kumalizika miaka 50 ya Uhuru na nchi kuwa na amani hivyo walitumia mkutano huo kuliombea taifa ili miaka mingine 50 ya uhuru taifa lisiingie matatizoni, wengine walioshika bendera hiyo ni viongozi wa kata ya Mombo wa Chama Cha mapinduzi akiwemo Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu'. |


MTSCHEEEEEEEEEWWW!!!!!
ReplyDeleteUNAIJERIA MTUPU....
Fanyeni kazi ya kuliombea taifa. Nchi yetu inaelekea pabaya sana sababu ya wachache wenye tamaa ya madaraka kwa manufaa yao binafsi, marafiki zangu.
ReplyDeleteWanamwonyesha Mungu vitu anavyoona kuzidi wao. Hawaamini uoni wa Mungu, wao waseme tuu ee Mungu ibariki tz naye anajuwa kila kitu kuhusu ukweli na uongo wa tz ikiwemo ufisadi unaolelewa ukuwe zaidi.
ReplyDeleteMAKUBWA PROFESA MAJI MAREFU KWENYE MADHABAHU YA WOLOKOLE HAOGOPI AU HAWAOGOPI HIZO SALA ZILIELEKEA KWA MUNGU WA PROFESA MAJI MAREFU AU WA WALOKOLE?
ReplyDeletedah sisi wa Afrika tuna Imani kali sana,lakini huwa najiulizagaa,dini hizi hizi zililetwa na hawa jamaa waliotutawala na kufanya biashara ya Utumwa zaidi ya karne nzima,mbona bwana aliwaachia tu hawa jamaa, au ndo kusema alitaka nasie twende Ulaya??
ReplyDeleteNakumbuka mara ya mwisho tulikesha pale Taifa kuomba mvua,na sasa?
hivi jama,imefikia wakati wakuamini sayansi,uwajibikaji na nguvu kazi au tuendelee kumtegemea sir God?inategemea nchi zilizoendelea zile omba kweli kweli sasa nasie twafata mfano.
Mkiomba kwa Imani kwa kutumia jina la Mungu mtapata/mtapokea.
ReplyDeleteHawa wamepagawa period!
ReplyDeletenina wasiwasi haya maombi yanaweza kuwatia viongozi wetu wakuu wendawazimu
ReplyDeletena huyo maji marefu eti ni mbunge namkumbuka alipokuwa akidandia magari yanayoenda mnadani na badae akajihusisha na uganga na leo hii amegeuka kuwa mbunge ama kweli kuwa kiongozi tanzania huhitaji elimu ni umaarufu tu
hapo ndipo utakapoona kuwa tanzania ni kama gari linaloendeshwa na kipofu.
mkoa wangu kaeni mkao wa kula nakuja huko mnipe kura zenu niwajibike bungeni.
grow up people
ReplyDeletemipango mibovu haina uhusiano na maombi ya kanisani au msikitini
ReplyDeleteHI KWANZA NINGEPENDA KUTOA PONGENZI KWA HAO WANO JIITA WAZEE WA KAZI HALAFU NA MHESHIMIWA NAIBU BALOZI KWA KUENDELEZA MFANO MZURI ULIOANZISWA NA WATANZANIA WA UHAIBUNI WA KUKUSANYA MISAADA KWA AJILI YA WATU WALIO ASIRIKA NA MAFURIKO, HAO WATU WANAO ONGEA VIBAYA NINA UHAKIKA HATA NDALA HAWAJAJITOLEA ATI KWA SABABU WAO MAFURIKO HAYAWAHUSU KWA SABABU WANALISHWA NA KWINI.
ReplyDelete