Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa pole kwa wafiwa wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji wa BBC marehemu, John Ngahyoma wakati wa mazishi yake yalioyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Kaka wa Marehemu, Ngalimecha Ngahyoma akizungumza kwa niaba ya familia baada ya mazishi.
Faidh Ngahyoma ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la BBC, marehemu John Ngahyoma akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Sport FM cha Dodoma, Abdallah Majura akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu John Ngahyoma wakati wa mazishi yake leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. RIP NGAHYOMA! TASNIA YA HABARI NA UTANGAZAJI IMEPOTEZA MTU MUHIMU SANA. MUNGU AKUREHEMU MILELE, UMETANGULIA WENGINE TUNAKUJA BAADA YA WEWE. POLE KWA FAMILIA YA NGAHYOMA KWA KIPINDI KIGUMU MLICHONACHO; TUPO PAMOJA KIROHO. AMEN

    ReplyDelete
  2. jamani! jamani! mavazi hayo misibani ay!mama ametinga kimino matokeo si mazuru waungwana!

    ReplyDelete
  3. Kwakweli mke wa marehemu hana nidhamu kweli mwanamke wa kitanzania kwenye msiba wa mumeo unakaa mipaja nje na miguu yote nje! Mama hujafurahisha kabisa!!!

    ReplyDelete
  4. kimini gani hicho cha kukikomentia, watu wengine mawazo yao machafu kweli hata jeneza hujaliona unatafuta vimini.Chunga tamaa mbaya mdau.

    RIP John

    ReplyDelete
  5. mdau si kwamba tuna mawazo machafu au tuchunge tamaa mbaya isipokuwa mama hakujitendea haki kuvaa nguo fupi kama hiyo haswa kwenye msiba wa mumewe kama hivyo!kwa kweli si heshima kabisaaaa!angavaa walau na kanga jamani kujistiri!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...