Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa, Gesase Waigama akirisha moja ya vishale kwenye ubao wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) yanayofanyika katika ukumbi wa Rose Garden,Mjini Dodoma.Wengine Pichani ni baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wakishuhudia uzinduzi huo.
Mchezaji wa Timu ya Kilimanjaro,Asina Munisi akirusha vishale kwenye ubao wakati wa mchezo wake dhidi ya mpinzani wake kutoka Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni (hayupo pichani) kwenye uzinduzi wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) yanayofanyika katika ukumbi wa Rose Garden,Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa, Gesase Waigama akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) yanayofanyika katika ukumbi wa Rose Garden,Mjini Dodoma.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa,Mohamed Mitegeko na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mchezo huo,Kale Mgonja.
Washiriki wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Vishale (Darts) wakimsikiliza Mwenyekiti wao (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa mashindano ya hayo leo kwenye ukumbi wa Rose Garden,Mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...