Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,inaeleza kwamba aliyekua mbunge wa Jimbo la Kalenga,Iringa, miaka ya nyuma Mh Stephen Galinoma (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi mjini Iringa wakati akiwa garini akipelekwa hospitalini kutoka kijijini kwake Kalenga alikokuwa anaishi.

Mheshimiwa Galinoma alikuwa mtumishi wa serikali mstaafu aliyeshika nyadhifa mbali mbali katika uhai wake zikiwa ni pamoja na Katibu mkuu idara ya ulinzi na jeshi la jenga taifa, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mbuga za wanyama pori, Mwenyekiti wa bodi ya mashirika ya Umma(SCOPO),Katibu wa tume ya uchunguzi wa viongozi, pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga ,Iringa.

Marehemu Mhe. Galinoma aliyekuwa anaugua kwa muda mrefu pia aliwahi kuenda India kwa matibabu kwa takriban wiki 6 kutibiwa tatizo la ugonjwa wa kansa ya kibofu cha mkojo .na alipata nafuu kwa kiasi fulani lakini baadae alizidiwa tena.

Marehemu ameacha wajukuu na watoto ,miongoni mwa watoto wa wake ni wanamuziki Innocent na Buti Jiwe aka Enry Galinoma. Taaritibu za mazishi zitatolewa si muda mrefu.

Mungu amlaze mahala pema peponi - AMINA.

Kwa habari zaidi za msiba wasiliana na Joseph Galinoma kwa namba hii 00255716492048 begin_of_the_skype_highlighting            00255716492048      end_of_the_skype_highlighting
au Denis Galinoma namba hii 00255784769945 begin_of_the_skype_highlighting            00255784769945      end_of_the_skype_highlighting

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. poleni wanyalukolo poleni sana. Nilisoma na Joseph Mzizima High school.

    ReplyDelete
  2. Jana Mchana saa 8 nilikuwa na Galinoma akiwa ameshikwa mkono na mama ambaye nadhani ni wa karibu sana naye ktk Restaurant ya Dolphy.Nilisalimiana naye na kasema kwa utani "muda ndio umeisha kijana"!
    Nimesikitika sana kusikia huu msiba wa Mzee wetu Galinoma.May God Rest his Soul in Eternal PeaceJames LS Urasa

    ReplyDelete
  3. RIP MZEE WETU WA UPANGA JUU

    ReplyDelete
  4. Hawa ndiyo wazee wetu wa Upanga jamani nadhani watoto wote tuliosoma Muhimbili Primary hili jina si geni kwetu, RIP baba upumzike salama. Poleni nyote familia ya Galinoma.

    ReplyDelete
  5. Familia ya Galinoma poleni sana. RIP baba yetu wa Upanga(Mindu ST).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...