Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) wakibadilishana hati ya mkataba baada ya kusaini na Mkandarasi kutok a kampuni ya DOTT Services Ltd kutoka Uganda  ambae ni Meneja Mkuu kwajili ya kukarabati   Mkumbara- Same (96km) utakaogharimu shilingi 128 bilioni za kitanzania, leo jijini Dar es Salaam-Picha na Mwanakombo Jumaa-MALEZO.
Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Mkandarasi kutoka  ya DOTT Services Ltd kutoka Uganda ambae ni Meneja  Mkuu Bw.G,Prudhvi Raj wakiwekeana saini mkataba wa ukarabati wa ujenzi wa barabara ya  Korogwe- Mkumbara- Same leo jijini Dar es Salaam, Mradi huo utagharimu  zaidi ya shilingi 128 bilioni. ambapo kampuni  hii itakarabati kapande  cha Mkumbara- Same (96 km) kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 65 za kitanzania.
 Makamo Mwenyekiti  wa  Kamati ya Miundombinu na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela (kulia) akishukuru katika hafla hiyo ya  mradi wa ukarabati wa barabara ya  Korogwe- Mkumbara- same (km 172) ambayo utagharimu zaidi ya shilingi 128 bilioni za kitanzania, hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dk, John Magufuli ((pichani  hayupo) na (kushoto) ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Herbert Mrango,
  Waziri Magufuli (kulia) akiteta na Mhandisi John Ndunguru (kulia) katika hafla hiyo
Baadhi ya wakandarasi wakiwa katika hafla ya kusaini mikataba ya mradi wa ukarabati wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Je Mh Waziri kalisoma hilo kabrasha? Isija akaacha "small print", maana hao watu wajanja!!

    ReplyDelete
  2. Yale yale ya barabara ya Kilwa kwenda Mbagala mwaka 2008-2009!

    Jamani Wahindi ni wacheza Sinema tu, tena sinema za mapenzi na kulia lia ,sio sinema za vita....mambo ya barabara na Ujenzi toka lini?

    ReplyDelete
  3. Linus RweikizaJanuary 26, 2012

    Nadhani kuna makosa kidogo ya kimaandishi manake kama mradi mzima wa korogwe hadi same (172km)gharama ni 12bil/= inakuwaje 96km zigharimu 65bil/=?

    ReplyDelete
  4. Huyo Mhe Mbunge hapo anaimba ngonjera nini? Hongerea Magufuli na Hongera awamu ya nne.

    ReplyDelete
  5. Mwenyekiti wa kamati Miundombinu anapeleka mradi kwao. Oyeee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...