Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea na kutoa wito kwa madaktari hao kurejea kazini  na kuendelea kutoa huduma za utabibu wakati serikali ikiendelea na juhudi za kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya nchini.
 Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Lucya Nkya (kulia) akimweleza jambo waziri wa Afya na Ustawi wa jamii mara baada kumaliza mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakitekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jamii wakati wa mkutano kati yao na viongozi wa Wizara ya afya uliojadili hatma ya mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
========  ======  =======  =======
SERIKALI YASISITIZA,MADAKTARI WALIO KWENYE MGOMO KUREJEA KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO
26/1/2012.
Serikali imewataka madaktari wote nchini walio kwenye mgomo kurejea katika vituo vyao vya kazi na kufanya kazi za utabibu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda amesema  serikali inatambua mchango walio nao wataalam wa afya katika utoaji wa huduma za afya nchini na inaendelea kuboresha maslahi yao.
Amesema serikali kwa kutambua mchango huo imekuwa ikiboresha maslahi yao na kuongeza nafasi za ajira kila mwaka kwa wataalam wenye sifa kutoka  nafasi 1,677 za mwaka 2005/2006 hadi kufikia 9,391 katika  mwaka huu wa fedha 2011/2012.
“Serikali inatambua mchango wa watumishi wa kada za afya nchini na ndio maana nafasi za ajira zimekuwa zikiongezeka kila mwaka hasa katika mwaka huu wa fedha 2011/2012”
Amefafanu kuwa madaktari kupitia Chama chao (MAT) wamewasilisha madai mbalimbali serikalini yakiwemo nyongeza ya posho ya kuitwa kazini baada ya kazi na madaktari kupewa nyumba za kuishi karibu na hospitali amesema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha maslahi hayo ili kuwawezesha wataalam hao kutekeleza majukumu yao ikiwemo ujenzi wa nyumba 8 za madaktari kwa wilaya 18 pamoja na kufanya maboresho ya posho.
“Serikali imepata fedha kutoka Mfuko wa Dunia(Global Fund) kwa ajili ya kujenga nyumba za madaktari na kwa kuanzia wilaya 18 zilizo pembezoni zimechaguliwa kujengewa nyumba 8 kila wilaya kama hatua ya kuboresha upatikanaji wa nyumba”
Kuhusu malipo ya udhamini kwa madaktari wanaochukua mafunzo ya uzamili,Kuhamisha madaktari bingwa wenye mikataba ya Ajira na Hospitali ya Taifa Muhimbili, Posho ya mazingira hatarishi na ajira za madaktari amesema kuwa baada ya serikali kupandisha hadhi ya hospitali za mikoa kuwa hospitali za Rufaa za mikoa kumekuwa na umuhimu wa madaktari hao kwenda kufanya kazi katika hospitali hizo na kuongeza kuwa idadi ya udhamini wa madaktari katika mafunzo ya uzamili imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Aidha kuhusu madai  ya kutaka nyongeza za mishahara ya shilingi milioni 3.5 kwa mwezi Dkt. Mponda ameeleza kuwa mishahara ya watumishi serikalini hufuata miundo ya utumishi (Scheme of Service)iliyopo huku akibainisha kuwa muundo wa malipo ya watumishi wa umma katika sekta ya afya umeboreshwa.
“Lazima tukubali kuwa baada ya kuboreshwa kwa miundo ya utumishi wa umma wafanyakazi wa sekta ya afya hivi sasa wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi wengine serikalini” amesisitiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Jamani hawaviongozi wetu wamekuaje sikuhizi ? Tumelogwa ama kuna nini ?

    imeshindikana nini kukutana na uongozi wa hawa madactar na kuwaeleza haya ? ili na wao wamwambie kero zao?

    je watakua wanabishana kwenye vyombo vya habari mapakalini wakati watu tunaendelea kuumia?

    walahi ningekua na uwezo ningemchapa viboko waziri . kwani kunagaramagini zakuzungumza nao?

    ReplyDelete
  2. Mhe. Waziri suala ni dooogo sana!

    Kabla ya kuwasihi Madakitari wenzako kurudi kazini,

    Hebu jiulize wewe ni mwenyewe ni Daktari na pia ni Mbunge kila kazi unaijua hapo uzito wake.

    Sasa fikiria ni kigezo gani kinampatia posho MBUNGE ya Shs. 200,000/= kwa siku, wakati DAKITARI akipata posho ya Shs.10,000/= kwa siku?

    ReplyDelete
  3. Jamani tazameni na utru na uzalendo,tuue kaka zetu,dada zetu,wadogo zetu,watoto wetu,wajukuu zetu kwa kudai maslahi tu.Hatuna viongozi ambao waendelee kuongea na serikali huku sisi tukiendelea kufanya kazi?

    Tuache ubinafsi ndugu zangu.Tumesoma kwa gharama ya wananchi haohao tuwaowatelekeza wakiwa hoi.Kuna watumishi wengi sana wa umma nao wnakazi ngumu sana lakini mishahara yao iko chini sana ukilinganisha na madaktari na wote bidhaa ni kariokoo.

    Tunakubali madaktari wanabeba roho za watu na ndo maana wanagoma kwa tishio hilo kuwa wakigoma watu watakufa.Lakini basi tuende taratibu.Kila mtu akiguswa kidogo na serikali basi hatma ni mgomo.

    Wameanza madaktari,wakimaliza waalimu wako ,mlangoni kaiti foleni ya mgomo,wakimaliza wananza askari n.k,n.k.Tutafika?Tunataka umeme,tunataka barabara,tunataka elimu ya vyuo vikuu.Ehe jamani acheni roho mbaya hizo tuende polepole.Kuna watu hadi leo mshahara wao laki mbili.

    ReplyDelete
  4. Yaani mimtu ambayo haitibu wagonjwa utasikia tu majibu yake. Napata tabu na elimu ya waziri. Hivi ni daktari wa PHD au Real medica doctor aliye sota 5 years of intense and hard training? Naombeni jibu jamani.
    Halafu wewe Mama Nkya (Spsychiatrist) hivi unamaanisha au unatania! Yaani kwavile mwenzetu sikuhizi upo kwenye VXGX umesahau shida za hospitali! Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa.

    ReplyDelete
  5. I am so much disappointed with these words, they do nothing everyday and wait till when people are dying and come up these politics on life of the people.
    I have been long enough a Tanzanian to know how well this is all deception.
    Let the the doctors stands on what's right till we see actions being done and for those who suffers from this I wish we could build a memorial monument engraved with their names for they are true heroes of this Nation

    ReplyDelete
  6. Ni miujiza ya Nabii Mussa!

    Mtu unakopokuwa Msomi ukafikia kuitwa DAKITARI inasemekana utakuwa ni mtu mwenye akili za kupitiliza!

    Lakini pamoja na Usomi wako ukiingia katika Siasa hizo akili za Kupitiliza zinayeyuka kabisaaaaaa,,,,ndio kama Mhe. hapa akiwasihi Madakitari wenzake warudi kazini!

    ReplyDelete
  7. Naibu Waziri Mhe. Mama kitaaluma /fani yake yeye ni (PSYCHIATRIST),,,Yaani Mtaalamu wa Tiba ya Akili.

    Sasa, kwa msimamo wake tunapata maswali mengi kuliko majibu, inawezekana ameanza kuumwa na inabidi yeye ,mwenyewe apelekwe WODINI LADBA AMEPATA MATATIZO YA UGONJWA WA AKILI!

    ReplyDelete
  8. badala ya kukutana nao wanakimbilia kwenye vyombo vya habari. KUTANA NAO.

    WAZRIRI MKUU NAO BADALA YA KUWAITA VIONGOZI ANASEMA KWENYE VYOMBO VYA HABARI YOKO TAYARI KUKUTANA NAO. KWA NINI ASIWAAGIZE WASAIDIZI WAKE WAKUTANE NAO?

    SUBIRINI SIKU WATU WA SEKTA YA FEDHA TUTAKAPOANGUSHA MGOMO WETU. TUTAONA KAMA MWALIMU AU DAKTARI AU SISI NANI ZAIDI. SISI HATUTATANGAZA ILI MCHUKUE FEDHA ILA MTAAMKA ASUBUHI MKUTE HAKUNA BENK WALA DIRISHA LOLOTE LA FEDHA LINALOTOA FEDHA. NYIE SUBIRINI TU KUJIFANYA FANI ZENU ZAIDI.

    ReplyDelete
  9. Ndo maana naipenda CCM na serikali yake. Mambo si ndo hayo bwana. CCM Oyeee, wapiga kura oyee. Mwaka 2015 lazima CCM itashinda kwa kishindo. si ounaona uteekelezaji wa sera zetu jamani?

    ReplyDelete
  10. Mie maskini sina uwezo wa kutibiwa india wala private ila nawaunga mkono madaktari washikilie uzi wao mpaka kieleweke kama tukifa tufe tu ila haki yao itendeke, siwalaumu kwa sababu hata mie ugumu wa maisha naujua lawaza zote ni juu ya serikali ya Rais wetu KIKWETE na washauri wake wabovu kuanzia huyo Mh. Waziri, Naibu Waziri na Mkuu Wetu Pinda ameshapoteza mwelekeo sio tena mtoto wa mkulima kesha onja asali kajua utamu wake si mtetezi tena wa wanyonge.

    ReplyDelete
  11. Madaktari wetu wanatumia wagonjwa kama kinga kwenye vita yao na serikali ila waelewe yafuatayo.
    1. kisheria chama chao hakina mamlaka ya kuitisha mgomo. hiyo ni kazi ya chama cha wafanyakazi wa sekta ya Afya. Waziri wa kazi mwenye dhamana ya usimamizi wa haya kakaa kimya.Vipi? Pia msajili wa vyama vya hiari alipaswa kuwaita viongozi wao ka kuona kama haya wanayofanya yamo kwenye madhumuni ya kuazishwa na kusajiliwa kwa chama hiki. seria zifuatwe.
    2. Hao wagonjwa wanaooteza maisha sasa kwa kukosa huduma ni sababu tosha ya kuwashtaki madaktari hawa kwa mauaji ya halaiki. kwani kina uhuru Kenyata waliua mtu kwa mikono yao? Ni matendo kama haya yanaleta mauaji ya kimbari. Je wakipata haki zao watarejeshaje maisha ya marehemu wetu?
    3. Kwa nini waziri wa fedha, Afya, utumishi na wa Kazi wasikutane chini ya waziri mkuu na kutoa majibu?
    4. Wabunge wote wamekaa kimya!!! Au wanajua waiongea wataibua mjadala wa posho zao? sasa utetezi wa wananchi upo wapi? wapiga kura ndo wanakufa waheshimiwa wabunge, madiwani nk.

    ReplyDelete
  12. Sasa hao wanaosema kwamba madaktari wamesomeshwa kwa pesa ya walipa kodi mbona wanachekesha sana! Waliosoma kwa pesa za walipa kodi ni hao madaktari wastaafu na viongozi waliomadarakani!
    Mimi binafsi ninasoma kwa pesa ya wazazi wangu, ambao wamelipa kodi ili watu wanaosomea tourism huku Ulaya wasomeshwe na serikali, niliomba MKOPO ili niweze kuwapunguzia makali wazazi wangu, lakini bodi ilininyima, na wanawapa watu wanaosomea tourism na kozi nyingine zinazofanana na hizo(Arts), tuliongea na mheshimiwa balozi wa huku na akasema mwenyewe atasimamia, lakini sasa yupo kimya, najua wamemnyamazisha tu, kwa sababu yeye alitaka watu wa Engineering na madaktari tu ndio aletewe! Lakini kila mwaka wanakuja watu wa Arts.
    Sasa mnataka uzalendo gani wakati viongozi wenu hawawajali?
    Ili yapatikane maendeleo ni lazima kuna watu waumie, na sasa serikali imeamua kuwatoa kafara wananchi wake!
    Mdau Urusi

    ReplyDelete
  13. Huyu Waziri anashangaza sana. Nyoka kaingia ndani ya nyumba unamtangazia kwa spika kuwa "Nyoka toka ndani". Pambana naye. Waziri alipaswa kwenda kuongea na madaktari na siyo waandishi wa habari. Tatizo ambalo limeota mizizi sasa Tanzania ni viongozi kutumia vyombo vya habari kama vitendea kazi. Waziri nenda kazungumze na wataalamu wenzako. Unapotutangazia kuwa mko kwenye mkakati wa kujenga nyumba 8 katika wilaya 18 ndiyo umesuluhisha tatizo. Jamani msiwafanye madaktari hawana akili na wala hawajui kuchanganua mambo.

    ReplyDelete
  14. Hoja zingine zinaongezea tu mjadala wa kibinafsi.Unawaunga mkono madaktari kugoma kwa sababu ulinyimwa mkopo!

    Unawaaunga mkono kwa sabau ulisomeshwa na baba yako!Na baba yako kama si wewe kasomeshwa na nani!Dhambi ya asili unaijua wewe kuwa tunarithi kosa alifanya Adama na Hawa.

    Ukinyimwa mkopo ndo unaunga mkono maovu.Kama hutasaidia serikali si umesoma kafanye kazi sehemu nyingine ambako hutasaidia serikali.

    Tumekubali kuwa madaktari wnamadai yao halali kwani waliahidiwa.Tunacho laumu nis madai kwa shinikizo la mgomo.Hii ni tabia mbaya.Watumie vikao,waache kujiona kuwa wao nibora kuliko watumishi wengine.

    Kila mtumishi mshahara hautoshi,tena wengine hata madaktari ni afadhali sana sana.Serikali ina mzigo mkubwa tugawane kilichopo kwa haki na usawa na kwa upendo si ubinafsi.

    Kumbukeni kipindi cha nyuma mlipendelewa sana wenzenu hawakulalamika wala kugoma.Dokta anaanza kazi kwa zaidi ya laki nane wakati watumishi wengine wanaanza na laki mbili.Mlikopeshwa magari mlipewa nyumba wengiwenu.

    Haya ndo ya Marijani Rajab " umepewa mia moja unataka mia mbili,umepewa mia tano unataka mia nane".

    Hatulaumu kudai haki zenu lakini taratibu jamani.Hamjaona wenye njaa kweli.Dunia nzima sas hivi inataabu na watu wake.Kuna shida ya fedha.

    ReplyDelete
  15. Ni kwelimaisha nimagumusana,lakini kunawenzetu hata hiyokazi bado hawajapata baada ya kusoma.

    Seeikali bado haina uwezo huo wa kiasi hicho ntakachojamani.Nendeni bwana tuacheni tufe.Kafanye kwenye hospitali zenu si mnazo!

    Kila siku mgomo mgomo mfumogani wa maisha mnauleta kwa watanzania wastaarabu!Daini kwa utaratibu wa busara.Kututishia kuua ndo nini sasa.

    Kweli mko busy sna lakini ni kama tui wafanyakazi wengine.Nanyi mnazo shift ndo maana mnapata muda wa kufanya katika hospitali zenu na za watu binafsi wa muda wa off duty.Tufuate ustraabu wa TZ tuache kuiga waarabu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...