Afisa Habari na Mahusiano Mkoa wa Rukwa, Hamza Temba (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Magereza wa Mkoa Rukwa George James Kiria zawadi za mwaka mpya kwa niaba ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya (MB). Msaada huo ni kilo 40 za nyama, debe moja la vitunguu, kilo 5 za nyanya, na sabuni za mche box 5. Zawadi hizo zitatumiwa na wafungwa wa gereza la mahabusu la Manispaa ya Sumbawanga.
Sehemu ya msaada uliotolewa na Mkuu wa Mkoa huo zikipokelewa na Maofisa wa Magereza Mkoa wa Rukwa. Kulia ni Mwandishi wa habari wa Star TV na RFA Samy Jumaa Kisika.
Picha ya pamoja kati ya Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Hamza Temba (wa pili kulia) na Ofisa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa George James Kiria wa pili kushoto. Kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa Job Philipo na Mwandishi wa Habari Samy Jumaa Kisika (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Chonde chonde baba mkuu wa gereza,tunakuomba uhakikishe msaada huo unawafikia walengwa usije ukakata kona na kuingia njia za panya ukatokezea kwenye kota za vijana wako.Pia hakikisha wanyapara hawajimegei wao peke yao tu maana sina uhakika kama msaada wenyewe utawatosha wafungwa wote kutokana na kiasi kilichotolewa.Big up Mama Manyanya umetuonyesha njia.

    ReplyDelete
  2. Hii sielewi kabisa. Hawa watu wamefungwa,kufungwa maana yake ni kunyimwa raha kwa muda unaotumikiakifungo sasa zawadi ya nini? Sana sana hakikisheni kuwa hamuwatesi na mnafuata sheria zote za haki za ninaadamu,hii ya zawadi mpya.

    ReplyDelete
  3. nice sasa mwakilishi eeeeh...am single tooo...nitupie email at neemajay13@yahoo.co.uk lol

    ReplyDelete
  4. Sio kama nnachuki na wat, lkn kwanini wapewe zawadi watu wanaovunja sheria? watoto yatima na maskini wamejaa kila pembe ya TZ na hawavunji sheria, hao ndo wanaostahili zawadi sio wafungwa!!!

    ReplyDelete
  5. Watu wengine wana roho ya ukatili sana hawafai kabisa katika jamii na ni hatari sana.
    Wafungwa wanahitaji haki zao pia kama binadamu wengine, Ile kufungwa tu yaani kunyimwa uhuru ni adhabu tosha, sasa iweje nyie wadau hapo juu eti mnasema wasipewe hata zawadi??
    Hivi mnaelewa maana ya kunyimwa uhuru binafsi hata kwa siku moja maana yake ni nini?? Au mnabwabwaja tu?
    Ngoja siku moja mtiwe sero hususani hapo bongo ndio mtajua ni mateso makali kiasi gani kisaikolojia licha ya physical
    Kuweni binadamu, na wenye huruma, si ukatili!

    ReplyDelete
  6. Jamani mahabusu hata wewe siku moja unaweza ukajikuta umetua, ni kiasi cha jirani yako kukuzushia tu na kwenda kukufungulia kesi. Mpaka ujitetee utoke unakuwa umeshapapitia. Mbaya zaidi ukutwe muda mbaya wawikiendi au afande anaekukamata akuchukie.

    ReplyDelete
  7. sasa hizo ndio zawadi za machungwa na machenza kwani hawali huko jela matunda?

    ReplyDelete
  8. ni gereza la mahabusu! hao sio wafungwa! Someni kwanza!

    ReplyDelete
  9. wewe ulesema kuwa wanafungwa ili wateswe na sio kupewa raha au zawadi unaonekana una roho mbovu na katili sana nani aliesema mfungwa hana haki?

    mtu akifungwa jela haimaanishi anatakiwa ateswe au apewe adhabu ndani ya jela sheria ya jela ni kufungiwa na kukosa free unayoipata ukiwa nje ili ujifunze na kujirekebisha ili hata ukitoka nje ubadilike tabia na haina maana kuna haja ya kuteswa zaidi

    wafungwa wa nchi zilizoendelea kwa mfano mimi nilifungwa huku ughaibuni lakini jela zake ni zaidi ya hotel za maana za huko bongo maana unapatiwa huduma zote na mpaka sehemu za michezo mazoezi na bado kwa mwezi unalipwa

    sasa usichukulie kuwa wafungwa hawana haki na badili yake wapewe mateso kumbuka unaweza kujikuta kwenye kesi labda unaendesha gari uagonga mtu sheria ikakuangukia ukafungwa


    mfungwa wa zamani.ughaibuni

    ReplyDelete
  10. Bro mfungwa wa ughaibuni.
    Nimependa comment yako,na hujakosea kabisa.Kufungwa sio kuteswa kama wanavyojuwa wenzetu Bongo,lakini upande mwengine sio makosa yao kufikiria hivyo, hawajuwi ni makosa ya serekali na uongozi kutoelimisha watu.Unafungwa ukose uhuru wa kujiamulia mambo yako,hiyo ni adhabu tosha,kama mtu habadiliki mueke maisha jela lakini usimtese.
    Marikani jela ziliitwa "college of correction"Zanzibar ziliitwa Vyuo vya mafunzo,kwa maana yake.Na jamani jamani leo chakula ishakuwa zawadi sio haki ya mtu.Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  11. Wewe uliyefungwa Ughaibuni mbona hujaeleza ulifungwa kwa muda gani na hizo pesa ulizokwa unalipwa kwa kufungwa zilitoka wapi na kiasi gani kwa mwezi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...