Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akifagia kwenye moja ya barabara za Mji wa Sumbawanga Mkoani humo jana katika uzinduzi wa kampeni ya kusafisha Mji huo ijulikanayo kama "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Wanaojumuika naye kwenye usafi huo ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Samwel Simwela. Mkuu huyo wa Mkoa ameanzisha Kampeni hiyo ambayo itakuwa ni ya kudumu baada ya kuona Manispaa hiyo imezorota katika usafi wa mazingira.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal akitoa uchafu kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Mji wa Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Sabas Katepa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akijumuika na wa wananchi pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali katika ufagiaji wa barabara za Manispaa ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akifanya uhamasishaji wa usafi wa mazingira katika Mji wa Sumbawanga kwa abiria wa daladala jana kwenye uzinduzi wa kampeni ya "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. I like that---Realy! Hata jamaa zetu wangekuwa wakionyesha kwa vitendo kama hivi badala ya tambo za kujitafutia umaarufu kwenye vyombo vya habari na kuandamana kila kukicha, hakika ningewaunga mkono!

    ReplyDelete
  2. Huu ndio mfano wa uongozi unaotakiwa katika karne na generation ya leo.
    Hongereza sana mama!!!!

    ReplyDelete
  3. safi, mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  4. safi sana mama umeonyesha mfano hai kwa viongozi wengine hasa wanawake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...