Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Jeshi la Polisi Zanzibar limeagizwa kuimarisha doria kwenye maeneo ya fukwe za Bahari ili kuyafanya maeneo hayo ambayo ni vivutio vya watalii kuwa salama wakati wote.

Taarifa ya Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa agizo hilo limetolewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati akizindua nyumba na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba nyingine za Askari Polisi eneo la Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Wakati wa hafla hiyo, Balozi Idi, amesema kuwa maeneo ya fukwe za Bahari visiwani humo ni moja ya mambo yanayowavutia watalii na kuingia kwa wingi visiwani humo na kuchangia pato la uchumi wa Zanzibar.

Amesema kutokana na ukweli huo, Serikali imeona kuwa ipo haja ya maeneo hayo kuwekewa mikakati ya kutosha ya kiusalama ili yaendelea kuwa kivutio kwa watalii wanaoitembelea Zanzibar.

Amesema kama maeneo hayo yatagubikwa na vitendo vya kihalifu vinaweza kuwa chanzo cha kuwafukuza watalii na kupeleka sifa mbaya warudipo makwao na hivyo kukosa mapato yatokanayo na utalii.

Balozi Idi amesema Serikali itafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanaendelea kubaki salama na kuwa vivutio vikubwa kwa wageni wanaoitembelea Zanzibar.

“Usalama wa maeneo hayo ndiyo chanzo cha kuvuta watalii na bila ya kuwepo kwa usalama wa kutosha haitakuwa rahisi kwa wageni kuendelea kuja kwa kuhofia maisha yao”. Alisema Balozi Idi.

Balozi Idi amesema kujengwa kwa nyumba za askari katika maeneo ya fukwe hizo, kutasaiidia kuimarishwa kwa maeneo hayo ya fukwe kwa vile askari hao sasa watakuwa wakiishi huko kwa wakati wote.

Pamoja na ujenzi wa nyumba hizo zilizochangiwa na wawekezaji, Balozi Idi, amesema Serikali bado inaendelea na juhudi zake za kuboresha makazi ya Askari wake ili waishi kwa pamoja makambini ikiwa ni hatua ya kuimarisha nidhamu na kuwapata kwa urahisi askari hao kila wanapohitajika kwa kazi hasa wakati wa dharura.

Awali Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa jengo lililomalizika linauwezo wa kuhifadhi askari 24 na lingine linaloendelea kujengwa litakuwa na uwezo wa kuchukua askari 18 na hivyo kuyafanya majengo yote kuwa na uwezo wa kuwahifadhi askari 42 kwa pamoja.

Amesema ujenzi wa nyumba hizo umechangiwa sana na wawekezaji wa mahoteli ya kitalii yaliyopo katika fukwe za Pwani ya Paje mkoa wa Kaskazini Zanzibar.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazi Unguja Bw. Mustafa Mohammed Ibrahim, amesema mkoa wake umetenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa chuo kipya cha Polisi na vituo vya Polisi na nyumba za kuishi Askari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hello Bro Misupu,
    Kuna hili jina huwa linani udhi sana kila nilionalo na nadhani sio mimi pekee.

    Ni jina ambalo Tanzania visiwani wanependa kulitumia na kusahau oficial name lao.Jina lenyewe ni Zanzibar.Maadamu Zanzibar na Tanganyika tumeungana na kuunda jina moja Tanzania basi sioni ni kwanini hawatumii jina Jipya ambalo ndo jina halali kisheria.Au na Watanzania Bara tutumie Tanganyika?.Basi nasi wa Tz Bara tutumie Tanganyika.
    Au muungano hakuna tena kilichobaki ni historia?.
    Tunaomba Serikali zi heshimu Muungano na kutunza Jina Lililo pendekezwa na litumike.

    ReplyDelete
  2. mdau hapo juu kwani hujuwi kama Zanzibar wana serikali na rais wao?sioni sababu ya kupiga kelele

    ReplyDelete
  3. Taarifa kama hii ni vizuri ukaweka picha ya tukio. Inapendeza zaidi na pia utapunguza bla bla.

    ReplyDelete
  4. mdau wa mwanzo hivi kweli wewe mtanzania? Umesoma historia ya muungano? umesoma kanuni na sheria za muungano? ni nani alokwambia kuwa jina halali kisheria ni Tanzania pekee?

    Ama kwa wazo lako la kutaka tanzania bara mtumie jina la Tanganyika, ingelikuwa vizuri kama wapo wengi kama wewe, tatizo ni kuwa wengi wenu hamupendi tuwaite watanganyika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...