HABARI WAPENZI WA BLOG HII SAFI YA CHAKULA BORA NA SALAMA

NASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU NA MCHANGO WA MAWAZO YENU PAMOJA NA KUA WASOMAJI WAZURI SANA WA BLOG HII.

CHANGAMOTO ZIMEKUA NI NYINGI SANA IKIWA MOJA WAPO NI MUDA WA KUKAA CHINI KUWEKA PICHA NA MAELEZO YA MAFUNZO JINSI YAKUNDAA VYAKULA.

TUOMBE UZIMA MOLA AKIPENDA NITIMIZE NDOTO YANGU YA KUANZA KUWEKA VIDEO HII HAITAKUA NA MASWALI MENGI MAANA KILA MMOJA WENU ATAONA NA MNAKIELEWA KISWAHILI KWA UFASAHA KABISA.

PIA WALE WOTE WALIOJIANDIKISHA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAPISHI TANZANIA KAENI TAYARI KABISA KWA MKUTANO MKUU WA CHAMA PIA TUWEZE KUCHAGUA VIONGOZI NA SHUGHULI ZA CHAMA KUANZA RASMI

KWA NIABA YA ACTIVE CHEF ASSOCIATION OF TANZANIA NACULINARY CHAMBER BLOG NAWATAKIA MWAKA WA MAFANIKIO NA AFYA NJEMA 2012 MOLA ATULINDE SOTE NA ATUSIKILIZE DUA ZETU SOTE AMIIN

WASALAAM

CHEF ISSA
Habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Asante na Happy New Year Chef Issa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. chef Issa wa ukweli happy new year same to youuuuu, napenda sana sponge cake ungekuwa jirani yangu acha tuu!

    ReplyDelete
  3. BIG UP CHEF CHAPA KAZI KIZALENDO NA WAZAWA WAIGE MFANO NA KUTOA USHIRIKIANO YOUR THE BEST

    MDAU HOLAND

    ReplyDelete
  4. Hii inahusu chef safi sana kwa salamu za mwaka mpya upo wapi kwasasa?

    mdau USA

    ReplyDelete
  5. Duh chef kweli unamoyo unajua watanzania hasa wa fani ya hoteli hawapendi kabisa kujielimisha we kaza buti ingawa ushirikiano ni finyu sana.

    BJ Japan

    ReplyDelete
  6. The number one chef in Tanzania big up and keep it up. Nawe pia na familia yako heri ya mwaka mpya

    Brother Sam. Sweden

    ReplyDelete
  7. Asikwambie mtu bwana mi nazimika sana na zile dengu nimeona kwenye blog yako. Je unasehemu rasmi unafundisha mapishi? wapi tukutafute mzee nataka my wife apate maujuzi ili tule mahanjumati

    ReplyDelete
  8. JUZI JUZI HAPA NIMEONA RAIS AMEFUNGUA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII NA KULIKUA NA MASHINDANO YA UPISHI JE WANAFAHAMU KAMA WEWE CHEF ISSA UPO? NIWAKATI SASA WA KUHUSISHA WATAALAMU WAZAWA WENYE UCHUNGU NA MOYO NA TALUUMA ZAO WANAOJITOLEA KAMA CHEF HUYU MZALENDO NAMFATILIA SANA HUYU KIJANA TOKA MICHUZI UMEMTAMBULISHA SIKU YA KWANZA MIAKA 2 ILIYOPITA KWELI KIJANA YUKO MAKINI NA FANI YAKE NA ANAUWEZO MKUBWA SANA HATA KUSHINDA MACHEF WENGI TU WABABAISHAJI ULAYA.

    TUJIVUNIE VYAKWETU

    SPENCER CANADA

    ReplyDelete
  9. Hahahahhaaaa mahanjumati oyeeeee poa bwana chef ok nawe pia kheri ya mwaka mpya cheers.

    DUBAi

    ReplyDelete
  10. nikweli kabisa we mchangiaji hapo juu hata mimi nimekua nikimfatilia sana huyu kijana kweli ameonyesha uzalendo wa hali ya juu maana baada ya kumalzia masomo yake aliufahamisha uma na akaahidi kutoa elimu bure katika mtandao watanzania na wanao jua kiswahili wote wamenufaika sana na taluma yake anayojitoea bure.

    Wizara ya maliasili na utalii utakuata hawafahau hata kama taifa lina kichwa kama hiki. Kila kukicha tunapata machef wageni mishahara mikubwa sana na kisha wanafaidisha nchi zao kwanini sasa usitolewe wito machef wazalendo warudi kuja kuendesha hotel zetu na pesa itabaki nyumbani nchi ifaidike.

    Chef issa ni world class chef na anauwezo mkubwa sana mi nafamilia yangu tunakuatakia pia kheri ya mwaka mpya na mafanikio katika kukiongoza chama hicho cha machef Tanzania.

    Mdau Swistzerland

    ReplyDelete
  11. Cahangamoto kwa wadau wa sekta ya utalii wataalamu wapo walipeni vizuri ili waje waendeleze fani hii adimu na adhimu kwa uzalendo.

    ni wakati wa taifa kujivunia vipaji vya wananchi wake.

    chef keep it up cheers

    Australia

    ReplyDelete
  12. YOUR LOST BWANA WEKA MAMBO MAPYA HAPPY NEW YEAR TO YOU TOO.

    ReplyDelete
  13. Chef Issa,,,,makulaji yako unayoandaa yanapatiKana wapi?

    Maana sisi wengine MANCHESTER UNITED au ARSENAL zetu ni madishi kwa kwenda mbele!!!,,,wengine sisi ni mashabiki wa sahani na bakuli zilizojaa,,,walahi mabata ushungu udenda unanindoka kwa uchu wa chakula!!!<<<hatuna ushabiki wa mipira kabisaaaa!

    Mdau

    Ustaadh Mohamed Omar
    Mbagala Mgeni nani/Mihande
    Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  14. Mimi zaidi ya kuipenda Liverpool timu yangu ya pili ni Biriani ya Ngamia,,,Super Chef Issa sahani moja tafadhali!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...