Marehemu Aziz Sheween (Kushoto) akiwa kwenye mazungumzo ya kikazi na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia wakati wa uhai wake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Aziz Sheween, Afisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, kilichotokea huko Riyadh, Saudi Arabia.
Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nyumbani kwa mazishi zinaendelea na pindi zitakapokamilika taarifa rasmi itatolewa. Tunawapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, watumishi wa Wizara na wote walioguswa na msiba huu mzito.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
S.L.P 9000
Dar es salaam, Tanzania
www.foreign.go.tz
Kiukweli nimesikitishwa sana na kifo chake ila ndo ahadi ya Mungu ikifika hatuna cha kufanya. Rest in peace bro.. Nawapa pole wanafamilia na nawaombea moyo wa subira poleni sana
ReplyDeleteNi pigo kubwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na familia kwa kuondokewa na mfanyakazi hodari ambaye alikuwa ni hazina kubwa sana. Tunaomba roho yake ipumzike mahali pema peponi, AMEEN.
ReplyDeleteAm out of words.... Ntakukumbuka daima ndugu yangu. Bwana ametoa na bwana ametwa.... R.I.P Aziz.
ReplyDeleteMungu amuweke mahali pema, ndio mapenzi ya mola. Mwenyenzi mungu awafariji familia ya marehemu.
ReplyDeleteLeo umetutoka lakini ndio amri ya mola.Amina!
Jamani Bro Sheween! Alinisaidia sana nikiwa Foreign. Kaka nenda kwa amani. Ee Mungu ipe familia yake nguvu ya kulipokea na kulikubali pigo hili kubwa. Poleni sana wana-foreign! R.I.P Brother Aziz Sheween!
ReplyDeleteRIP Auncle Aziz! kifo chako ni cha ghafla umetuacha kwenye majonzi mazito, daima ucheshi,upendo wako tutavikumbuka daima, Mwenyezi Mungu akuweke mahala pema peponi Amina!
ReplyDeletePole sana Sophia Kawawa na watoto, Mungu awape subira kwenye wakati huu mgumu, Inalillah Wainalillah Rajun
ReplyDeletekaka uende kwa amani, ila sitasahau wema na upendo wako kaka. ulimsaidia mtu wangu wa karibu alipokwama kwa kupoteza pasipoti yake. At that mtu wangu hakuweza kuthibitisha kama alikuwa Mtanzania, na hakuna mtu ubalozini (not in Saudi) aliyekuwa tayari kumsaidia pa kumhifadhi. Ila wewe ukajitolea kumhifadhi na ukamsaidia mpaka akaweza kuondoka salama. Ahsante sana kaka kwa msaada, sikuweza kukuona uso kwa uso kukupa ahsante yangu. Nashukuru sana. Mola aipe nguvu na amani familia yako katika kipindi hiki kigumu kwao. Once again, thank u! thank u! for being there for us at that difficult time for us. RIP bro Aziz
ReplyDeletePOLENI SANA NDUGU,MARAFIKI NA WAFANYAKAZI WOTE WA WIZARA YA MAMBO YA NJE.MWENYEZI MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI -AAMIN.HE WAS A NICE YOUNG DIPLOMAT NA ALIKUWA RAFIKI WA KADA ZOTE BILA KUJALI YEYE NI NANI.SI WOTE WANAJALIWA KARAMA KAMA YA AZIZ.RIP BRO AZIZ.-ADAM
ReplyDeleteRest in Peace, I do not know you but from the comments above you seemed to be a good person "mtu wa watu" Mwenyezi Mungu akufunulie nuru yake upumzike kwa amani, pole na wapate nguvu familia walio bakia. bll
ReplyDeleteNi Kweli Bwana Azizi ni Mtu wa watu, mtu mzuri mtu mwenye ushirikiano na watu, habagui mkubwa na mdogo wa kihceo wala umri, nawapa pole wanafamilia ndugu jamaa na marafiki na hasa watumishi wa Ubalozi wa Tnzania Mjini Riyadh, kazi ya Mungu haina makosa yeye ndio mwenyekupanga na kuamua kile alichokipanga.. Innaa Lillah wa Innaa Ilaihi Raji3un..
ReplyDeleteAbu Bintain
R.I.P Aziz. You will always be remembered for your kindness and charm.
ReplyDeleterest in pace Aziz
ReplyDeleteR.I.P uncle Aziz. We will miss you.
ReplyDeleteMungu amrehemu brother Aziz.
ReplyDeleteAlikuwa ni binaadamu ambaye alikuwa hapendi kuona mtanzania anapata tabu ugenini. Sura yake ya ucheshi na uamuzi wake wa busara, tumeikosa...
Watanzania tuliopo Riyadh tutam-miss sana Aziz.
Mungu amrehemu na awape subra na imani family yake. Amin