Wakazi wa mji wa Musoma wakichukua mchanga kandokando ya ziwa victoria licha ya serikali kupiga marufuku uchotaji wa mchango kando ya ziwa hilo.Hata hivyo inaoenekana wazi katazo hilo la serikali halijatiliwa mkazo kutokana na kwamba hakuna hata vyombo vya usalama ambavyo vinaweza kutembea kando ya ziwa hilo kwa lengo la kuwakamata wale wanao fanya uharibifu huo.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi aliyekuwa Musoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Baada ya kumaliza misitu, sasa Watanzania tunaingila mito na maziwa. Huu nu ukosefu wa Uzalendo na Nidhamu. Wajibu wa utunzaji wa mazingira ni wa kila mmoja katika nchi hii.

    ReplyDelete
  2. Chonde chonde mbona tubajimaliza wenyewe, nadhani hawa wananchi hawajui athari zake. Wahusika wako wapi au mpaka.......... ndio mnaanza kuunda tume?

    ReplyDelete
  3. wewe nini waalike kwako ili waje kula basi waache watu wapate riski yao polisi mbona wamelala kwa mambo muhimu kuliko huo mchanga acha zako wewe watu wanaiba mahela haswa mbona hamsemi acheni hizo noma

    ReplyDelete
  4. Ankal tumefumbia macho mambo mangapi makubwa tu, itakuwa hili?

    ReplyDelete
  5. waacheni hao wanaiga wakubwa wao. sitowalaaumu kabisa. kwanza wamekosa elimu ya kujua athari pili wana njaa. Sasa tuwashike hawa wenye matatizo yote na tuwaache wale walioshiba ila tamaa inawasumbua na wanamashahadaima ya feki au ya ukweli????Sio utakuwa uonevu?????

    ReplyDelete
  6. Anony wa tano toka juu: SADATAAAAA!!!!!

    ReplyDelete
  7. KITAALAMU WANACHOFANYA KWA WAKATI HUU NI KUPUNGUZA ULE MCHANGA ULIOLETWA NA MVUA. UKIACHWA KUINGIA ZIWANI UNAWEZA KUSABABISHA KINA CHA ZIWA KUPUNGUA. KINACHOTAKIWA NI USIMAMIZI ILI WACHOTE TU HUU WA UFUKWENI.

    PICHA YA KWANZA NIMEIPENDA, JAMAA KAACHIWA LINDO LAKINI KAUCHAPA USINGIZI SASA HIVYO VILOBA SI VITAIBIWA?!!

    ReplyDelete
  8. ACHA WATU WAPIGE KAZI BWANA, MMEKALIA MANENO TUUU.............

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...