Msimamizi wa zamu wa Idara ya kuendesha mitambo ya kufua umeme katika mgodi wa Kidatu kwa kutumia kompyuta , Joseph Mwansasu ( wapili kutoka kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ( wa kwanza kulia) mfumo wa Teknolojia ya Kompyuta za kuwasha mashine nne za kufua umeme kwenye mgodi wa Kidatu kilingana na mahitaji ya Umeme nchini , Naibu Waziri huyo aliutembelea Mgodi huo Januari 8, mwaka huu, ili kuona hali halisi ya uzalishaji wa umeme na kiwango cha maji kwenye  Bwawa la Kidatu.
 Kaimu Maneja wa Mgodi wa Kidatu , Joseph Lyaruu , ( mwenye tochi) akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ( wa kwanza kulia) kifaa kilichobadirishwa baada ya kufanya kazi muda mrefu na kufanya sehemu nyingi kusagika na maji  wakati wa kuzungusha  mtambo wa kufua umeme ndani ya mgodi wa Kidatu, Naibu Waziri huyo aliutembelea Mgodi huo Januari 8, mwaka huu ,  ili kuona hali halisi ya uzalishaji wa

umeme na kiwango cha maji kwenye  Bwawa la Kidatu.

Bwawa la Kidatu likoonekana kuanza kujaa maji ya mvua baada ya kunyesha mvua za kutoka katika Mikoa ya Iringa, Mbeya, Singida na Morogoro , ambapo hadi kufikia Januari 8, mwaka huu ujazo ulifikia mita 690.5 kutoka 680 ambalo ni ongozeko la mita 10.5 kwa muda wa miezi mitatu ya mvua zilizonyesha. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. maji yanaongezeka na ikiwezekana na yale ya bonde la msimbazi yaelekezwe huko ili mgao upungue tumechoka na kelele za majenereta mitaani utasema tunasaga mawe.

    ReplyDelete
  2. Hayo maji kupungua pengine yanatumika ktk mashamba.Na kama watu wanatumia ktk mashamba,kwanini hawakatazwi na wawekewe walinzi kuhakikisha kwamba hayatoki nje.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...