Chris, Jestina na wadau wengine wakikusanya misaada mbalimbali
 Louisa Frisch (Bright Future TZ), Jestina George, Haruna Mbeyu (TA London) & Chris Lukosi 'Mzee wa Kazi (Serengeti Freight).

KWA MAWASILIANO ZAIDI KUHUSU MISAADA WASILIANA NA
JESTINA GEORGE 07404332910
FRANK  EYEMBE 07865594576
BARAKA NYAMA 07816981577 

KAMA UNA MCHANGO UNAWEZA KUDEPOSIT KATIKA ACCOUNT IFUATAYO:
BARCLAYS BANK
JINA: TANZANIA ASSOCIATION LONDON Account Number: 23374815 
Sort Code: 20-72-89 
ANDIKA JINA LAKO NA MAFURIKO AS REFERENCE

TUNAWASHUKURU NYOTE KWA KUJALI NDUGU ZETU
Contact us for more info;
CHRIS LUKOSI 07903828119 
SIMON LOUIS (MOHSIN) 07950689243
BRIAN (BABA NJOROGE) 07795160757
HASSAN (RICHARD) 07405159255
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Asanteni sana kwa kuonesha moyo wa Kiuzalendo na pia tunapend akutoa shukurani za pekee kwa utawala wa The Pit Stop 'Uwanja wa Nyumbani kwa kutupatia nafasi ya kufanyia shughuli yetu pale. 

MUNGU AWABARIKI,

Serengeti Freight, Miss Jestina Blog,Urban Pulse na Bright Future TZ 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. HONGERENI WAZEE WA KAZI KWA KAZI NZURI MNAYO JITOLEA KWA COMUNITY YA WATANZANIA HUKO ULAYA NA HAPA TANZANIA

    ReplyDelete
  2. ninatowa shukran za dhati kwa wazalendo wote waliochangia msaada huo , ila natowa ushauri anzeni na mapema kuwasiliana na viongozi huko tanzania ili msitozwe kodi na TRA na msije mkatozwa storage change wakati mnafanya harakati za kutowa mzigo huo ,moyo wenu mzuri utageuka kuichukia nchi yako kwani hivyo vyombo vya serikali havijuwi imani zenu
    Mungu ibariki TANZANIA MUNGU WABARIKI WA TANZANIA

    Slim Slim .Norway

    ReplyDelete
  3. Mh.Haruna Mbeyu -Meya wa London naona the konozz zimekuzidi hasa hiyo yenye njano.

    Hongereni kwa kukumbuka nyumbani.Bwana awe nanyi.

    ReplyDelete
  4. Hongereni sana. Ila hayo mabegi nimezoea kuyaona Ubungo stendi ya mkoa nikawa nafikiri ni mjasiriamali mmoja wa kiembe-mbuzi anayashona, leo ndio nimejua kumbe yanatoka kwa Mama!!

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli tunawashukuru sana kwa moyo wenu wa huruma. Hivi ndivo inavyotakiwa, na kwa Mungu thawabu zenu zinaongezeka.
    Hoja yangu hapa ni je, misaada hiyo itawafikia walengwa? Kwa uzoefu tulioshuhudia, tumeishapatwa na majanga mengi, na watu wakajitolea sana tu, mfano mabomu ya Mbagala, Mafuriko ya Kilombero, Mabomu ya G' Mboto, na sasa mafuriko Dsm. Je, huyu Mkuu wa Mkoa, na kauli zake za ajabu, utata katika utendaji wake wa kazi wakati wa majanga, kuna dalili kwamba waathirika watapata misaada hii? Kumbukeni, wakati wa mabomu ya G'Mboto, alivyokuwa akiwajibu watu wanaokwenda kwake kutaka msaada, alikuwa akijibu ndivyo sivyo, na wengi kuwakatisha tamaa. Kauli zake zina utata, na ndio maana tunasikia watu wa Lindi walimkataa. Labda wenye kutoa misaada yao wafanye kufatilia wenyewe kuhakikisha wanawafikia walengwa. Nina maana kwamba kwa wale walioko nchini, wahakikishe wenyewe wanaenda kwenye vituo husika na kuwagawia walengwa misaada husika wao wenyewe, iwe chakula, vifaa muhimu, mashuka, magodoro, nk. Wale mlioko nje, basi, wekeni utaratibu kwa kuweka wawakilishi hapa kufanya kazi hiyo kwa niaba yenu. Maana tumeshuhudia watendaji wa hapa, kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa, wanatumia ile kauli ya kufa kufaana. Akiwa anagawa yeye, basi atahakikisha ndugu yake aliyeko tarafa au mtaa mwingine anamuita aje kwenye foleni, mfano yuko Kawe, aje Vingunguti ambako yeye anasimamia, apate Godoro,sukari, blanketi, n.k. ili mradi yeye msimamiaji anahakikisha wa kwake wamepata. Hii inawakatisha tamaa wale wanaojitolea, maana dhamira yao ni kusaidia walengwa na wenye kuwa ndani ya kipindi cha maafa, lakini wanaopata ni wengine. Tumeliona hilo tangu mabomu ya Mbagala, hadi yakaja ya G'Mboto, na sasa mafuriko. Hali ni ile ile, viongozi wanaweka sana umimi, badala ya kusaidia walengwa, zikiwa fedha, hapo ndo usiseme. Mpaka leo bado wengi tu hawajalipwa, hawajapatiwa kile walichostahili na kuahidiwa, wakati misaada inatoka mingi mno ya kila aina. Leo ndo tupo na janga la mafuriko, tunashuhudia wanaopokea ni watu hata hawakuguswa na mafuriko, wakati wahanga wapo na hawajui la kufanya. Hebu watu wa habari, wajaribu kufuatilia kuhakikisha wahanga wanafikiwa jamani, hali ni mbaya kuliko inavyosomeka. Tunasoma tu wa Jangwani, lakini sehemu za Kigogo na Vingunguti Maji Machafu, watu hawana kitu, si nguo, si shuka, si chakula n.k. Nendeni mkahakikishe, halafu wafahamisheni viongozi hawa, wawe na aibu kidogo. Leo kwa hawa, huwezi jua kesho, yaweza kuwa wao,wewe, yeye ..... hili ni jinsi nilionavyo mimi. Niwashukuru tena watu wa London, msichoke jamani.

    ReplyDelete
  6. hongereni sana kwa kukumbuka nyumbani mungu yupo nanyi

    ankali nakuomba ruhusa nimsifie huyo dada hapo kati nimependa supu zake mwe!

    ok nitundikie nishamaliza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...