Na Mwandishi Wetu.

Wapiga kura wa jimbo la Kigoma Kusini, ambalo mbunge wake ni David Kafulila wamefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu, Dar es Salaam wakipinga kifungu kwenye Katiba kinachotamka mbunge anapovuliwa uanachama anakoma kuwa mbunge.

Watu hao watatu walifungua kesi hiyo leo na kupewa namba 1/2012 wanakilalamikia matumi ya Ibara ya 71 (1) (f) kinachosema Mbunge atakoma kuwa mbunge iwapo ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge .

Aidha wanaiomba mahakama hiyo iamuru Bunge litunge sheria inayoruhusu mbunge aliyefukuzwa uanachama katika chama chake awe huru aruhusiwe kuhamia chama chochote atakacho bila kuvuliwa ubunge.

Kesi hiyo imefunguliwa zikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kuvuliwa uanachama katika chama NCCR-Mageuzi na hivyo kupoteza ubunge wake.

Kafulia alivuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 20, mwaka jana, lakini amefungua kesi mahakamani hapo kupinga hatua hiyo ya kuvuliwa uanachama.

Kesi hiyo ya kikatiba imefunguliwa leo na wapiga kura watatu wa jimbo ambao ni wanachama wa tofauti kwa niaba ya wananchi wengine wa jimbo hilo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walalamikaji wanaowakilishwa na Kampuni ya uwakili ya Mpoki & Associates, ni Juma Shaban Nzengula (CCM), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kigoma kata ya Nguruka, Patrick Haruna Rubilo (NCCR-Mageuzi), mjumbe wa Kata ya Itebula na Mwenyekiti wa Kijiji cha Bweru na Fanueli Misigalo Bihole ambaye ni mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) ni Katibu wa wazazi wa Kata ya Mtegowanoti.

Wanalalamikia kifungu hicho kinakiuka haki za msingi katika Ibara ya 21 ya Katiba inayotoa uhuru wa kushiriki katika shughuli za umma kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa mujibu wa sheria.

Aidha Ibara hiyo inakiuka Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu ambao Tanzania imeuridhia na kuusaini.

Mbali na hayo inakiuka Ibara ya 201 (1) ya Katiba ya Nchi inayotoa uhuru kwa wananchi kushiriki na kutoa maoni yao kwa uwazi. Nje ya mahakama walidai kuwa kesi hiyo wamefungua kwa niaba ya wapiga kura wa jimbo la Kigoma Kusini baada ya kuona wimbi la kufukuzwa uanachama wabunge lililoingia sasahivi baada ya mbunge wao, Kafulila kufukuzwa NCCR na sasa mbunge wa Wawi Zanzibar (CUF), Hamad Rashid kufukuzwa.

Wakizungumza baada ya kufungua kesi hiyo, walalamikaji hao walisema kwamba wameamua kufungua kesi hiyo liocha ya kwamba wanatoka vyama tofauti kwa kuwa mbunge huo hakuchaguliwa na wanachama wa NCCR-Mageuzi tu bali na wa vyama vingine pia.

Walisema mbunge anakuwa ametoa ahadi nyingi baada ya kuchaguliwa, na sasa ni kipindi cha kutekeleza ikiwa ni pamoja na shunguli mbalimbali za maendeleo na hivyo ni kurudisha maendeleo nyuma.

Kwa upande wake Rubilo alisema kuwa mbunge anafunga mkataba na wananchi na kwamba huwa wanatoa ahadi nyingi katika kutekeleza mkataba huo kama vile kusomesha watoto na shughuli nyingine za maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. CCM ITABAKI MADARAKANI KWA MUDA MREFU KWA MTENDO HUUU WA CUF NA NCCR.POLE KAFULILA HUKUJUA UMEMKIMBIA MBOWE KUMBE HUKO UNAKUTANA NA MBATIA MBELE YA SAFARI WOTE KILIMANJARO.

    ReplyDelete
  2. Tuache kutunga sheria kwa manufaa ya baada ya tukio! Hiyo itatufanya kuwa tunatengua sheria kila kukicha. Tuache sheria zifanye kazi yake, na ikiwa hazina manufaa, tuziondoe kwa manufaa ya Umma, sio kwa manufaa ya kafulila au Rashid! Just imagine angefukuzwa vijisent huko chama cha Magamba, halafu sheria ikasema hawezi kutoka, patatosha kweli?!

    ReplyDelete
  3. Ndio maana mpaka leo hatuna maendeleo na umasikini umetujaa na yote haya yametokea kwasababu ya kuoneana muhali.Viongozi lazima waangaliwe na kuadhibiwa pale wanapokosea.Hakuna kuwekana madarakani kama mtu hajatimiza kile alichotumwa na huku anachafua hali ya hewa na pengine ufisadi.

    ReplyDelete
  4. Hawa wapiga kura nao hovyo. Tatizo hapa ni ukabila na huyu ni wa nyumbani. Kafulila ni limbukeni ingawa hata Mbatia si safi. Alichofanya Kafulila alistahiki kufukuzwa. Kinachofanyika hapa ni kutapatapa. Haiwezekani mbunge au mtu binafsi akawa maarufu kuliko chama. Kama Kafulila anaamini alionewa ni kwanini alilia na kuomba msamaha zaidi ya kutapatapa baada ya kupata waajinga wa kumtimizia matakwa yake ya kutaka kurudi bungeni achume siyo kuwatetea?
    Gwiji

    ReplyDelete
  5. wananchi pia wawe na uwezo wa kuwaondoa madarakani wabunge wasiofanyakazi sio kuwalinda wanaofukuzwa tu.

    ReplyDelete
  6. Ukiwa kisiki utakuwa ADUI wa wengi!

    ReplyDelete
  7. Watu wana sera ya Utajirisho kupitia Wizi na Ufisadi, sasa ukiwa unawazibia watakukata chembe!

    ReplyDelete
  8. huyu ni kimeo...inajulikana hvyo. ni mpenda madaraka asiye na subira...na hiyo ni tabia ya watu wa kigoma kuanzia kwa kaka yao kabourou. hana hata mda mrefu toka aingie nccr tayari kaanza chokochoko za kumtoa mwenyekiti...ili best yake zitto ahamie huko na apate nafasi ya uongozi ili aweze kujirahisishia kugombea uraisi.

    ReplyDelete
  9. Mbona rosstam hawkusema hivyo au kwa kuwa muislamu?

    ReplyDelete
  10. Wewe mtoa maoni wa Sat Jan 07, 07:35:00 PM 2012, 'issue' ya Rostam ni tofauti na ya Rashidi pamoja na Kafulila. Rostam hakufukuzwa wala kuacha uanachama wa CCM. Bado ni mwanachama wa CCM, bali tu alijivua nyadhifa zote alizokuwa nazo. Sasa hawa wengine wanapoteza nyadhifa walizokuwa nazo kwa sababu ya kuvuliwa uanachama. 'Think deeply before you post your comments'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...