Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Yaeda Ampa Mary Genda na wanafunzi wa shule hiyo wakipokea vitabu toka kwa Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule za sekondari nne za mkoa wa Manyara ambazo ni Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa chini ya mpango wake wa shule yetu halfa iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii.
Afisa Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde akikabidhi vitabu kwa Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu Mikaeli Hadu ,kwa niaba ya shule nne za sekondari zilizokabidhiwa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shuke,shule hizo ni Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa,Mkoani Manyara (katikati )ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Harry Sinjela.
Wanafunzi , walimu ,wafanyakazi wa Airtel na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya mbulu mkoani Manyara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Airtel kukabithi vitabu kwa shule 4 za sekondari zilizopo mkoani hapa, kila shule imepata vitabu vya thamani ya shilling milioni moja. Walikaa kutoka kushoto ni Afisa wa uhusiano wa Airtel Jane Matinde Akifatiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mbulu Bwana Harry Sinjela, Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu Mikaeli Hadu na diwani wa kata ya Yaeda Ampa Bw Marcel Malley.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...