Binti yetu Zenna Ally Mapee mwenye umri wa miaka 22 amepotea nyumbani tangu tarehe 3/2/2012 aliaga anakwenda Mbagala na kisha kuelekea Mwananyamala kwa shangazi yake. Ni kawaida huwa anaenda na kurudi nyumbani.
Alipiga simu akitujulisha kuwa atarudi usiku kwa kuwa ilikuwa usiku kama saa mbili hivi tulimwambia alale kwa Shangazi ili arudi kesho mapema. Tulikubaliana hivyo siku ya Ijumaa tarehe 3/2/2012 asubuhi kama saa tano alikuwa bado hajarudi tukapiga simu kwa Shangazi ndipo aliposhangaa kwani hata jana yake hakuwa huko.
Tumejaribu kumtafuta kwa ndugu na jamaa bila mafanikio na kutoa taarifa vituo vya police bila mafanikio. Tunaomba mtu yoyote ambaye anataarifa za Zena awasiliane na sisi kwa simu tutazitoa hapo chini au hata kwa kupitia blog hii.
Zena kama unaona tangazo hili na kwenye vyombo vya habari popote ulipo tunakuomba urudi nyumbani Familia zote za Mzee Iddi Sungura na Familia ya Mzee Mapee wote tunakupenda, tunakujali na tunakuhitaji sana.
Namba zetu za simu kwa taarifa.
0716 696858- Shangazi Mama Hadija
0713 400363 – Kaka Madaraka
0778 612613- Mama Mdogo Masha Sungura
0715 080926- Mama Mdogo Utesi Sungura
0656 369316- Mama Mdogo Shindo Sungura
tangazo hili ungelipeleka TBC bango ingekuwa rahisi zaidi watu wengi wangemuona
ReplyDeletesuali dogo tu, mumejaribu kumpigia simu? i assume ana mobile na ndiyo alopiga kusema atarudi usiku. ni wazo tu. Inshaallah ataonekana na kurudi nyumbani kwa familia yake kwa salama amin
ReplyDeletePoleni sana wazazi na watu wa karibu
ReplyDeletelakini kwa taarifa hizi msifadhaike huyo binti inaonyesha hajapotea wala kupata matatizo, ila kwakua anajiona kakua ameamua kuacha nyumbani kwao na kuenda kwake bila kufuata utaratibu rasmi.
Kifupi ameenda kwa bwana!!¨hivyo wazazi kwakua mmekwishatoa taarifa tulieni atakuja mwenyewe tu akili ikimuingia.
Angepata asingepiga simu na angekua amefika kwa shangazi yake, kosa mlilofanza bila kutegemea ni kumruhusu kulala kwa shangazi yake bila kuwasiliana nae, na sasa amenogewa.
huyo hajapotea kuna mtu kamuweka ndani kwa mda, nahisi anaona aibu kurudi ngojeni ajipange kuja kuwadanganya!
ReplyDeleteMashaallah!! Binti wa haja hasa.
ReplyDeleteJamani wanaume wenzangu, yeyote aliyepiga bao la kisigino hapo hajakosea wala kulaumika. Tuwasiliane ili niwe mshenga na tuhalalishe maisha ya huyu binti huko aliko.
Hakika ni mpini wa nguvu, hivyo tusiwasumbue Wazazi wake bure.
Abiola Jr.
Mafia kiduka cha juice
Huyo hajapotea, msichana wa umri wake huwa hapotei ila anachelewa kurudi tu. Ondoeni shaka.
ReplyDeleteAna hamu ya kupika chungu chake sasa na anaonekana dhahiri kuwa 'mapishi" anayajua.
Ignas wa Chelsea
Nadhani, atakuwa amepata mume,na sasa nahisi ni mshenga ndiye atakayejitokeza ili awaambie msimtafute binti yenu tunaye.
ReplyDeleteSura hii haiwezi kulala bus stand. Kuna malazi mazuri yameandaliwa kwa ajili yake. Wazazi wavute subira. Watajua alipo. Ana mvuto binti huyu, bwana.
ReplyDeleteTatizo mnawafungia sana nao huwa wanatakiwa kusevisi maungo.
ReplyDeleteFedheha inayofanywa hapa ni ya kusikitisha. Ni busara kuwaonyesha wazazi hawa na ndugu wenye hofu na upendo wa ndugu yao huruma wanayostahili badala ya kejeli za kipuuzi.
ReplyDeletepoleni wazazi wenzangu, hawa watoto wa kike wanamatatizo yao. kama alipga cmu nipo kwa shangazi hali ya kuwa hayupo, basi kwa imani yangu yupo kwenye mikono salama ya dhambi, ninachomuomba binti rudi home halafu uondoke kweupe na siyo kututesa ss wazazi tuje kupata pressure hali ya kuwa wadogo zako ni wadogo.
ReplyDeleteHawa ndio watoa maoni wanaohitaji Taifa liendelee na ndio tunaowategemea kwenye maoni ya katiba mpya, inakuwaje kuanza kumtolea binti wa watu maneno makali kiasi hicho na hakuna lolote mlilothibitisha.Tuna ndugu zetu, jamaa au marafiki wangapi waliopotea kwenye mazingira ya kutatanisha?, Je ni wangapi tulioletewa taarifa kupatikana maiti zao baada ya kupotea?. Sidhani kama hapa panatembelewa na watoto wa shule za msingi na hata kama wapo wa sekondari ni wachache sana, naomba tujitahidi kuandika maoni kutokana na umri na upeo tulionao na si kukurupuka na hoja zisizo na uthibitisho.. Siwatakii mabaya ila yatakapowakuta kwa watoto, wazazi au ndugu zenu ndio mtaelimika zaidi na kujifunza kuongea mbele ya jamii linapotokea tatizo.. Mungu amuongoze na amuepushe na madhara yote yaliyo na yanayo msibu huko alipo.
ReplyDeleteKijana Mdogo
Poleni Wazazi kwa kuzidiwa akili na Kachala!
ReplyDeleteInaonekana mchezo huo aliuanza kipindi na sasa amenogewa kama Wadau walivyo tutaarifu kwa Maoni hapo juu.
Mara nyingi kwa Taratibu za Malezi haifai mtoto wa Kike au Binti aliye ktk umri kama huo au Mtoto aliye chini ya Mamlaka kutoka safari bila kushindikizwa!
Inatakiwa wawepo zaidi ya angalau wawili na lazima ijulikane watapita wapi na watarudi muda gani.
Zaidi ya hapo Wazazi au Walezi mlitakiwa KABLA msome nyendo zake Binti na kama mngebaini ameshajitambua amekuwa mtu mzima ni bora mngembana amlete huyo Kachala muwape Mamlaka wa kuwa Mume na Mke kwa njia Halali!
Muharibifu Kachala ametumia mwanya huo wa upungufu wa Usimamizi na sasa amepiga Bao ametulia na mwanamke wa bure kwake Mbagala!
Hajapotea,,,kwa umri wake ni kuwa ameshapata 'Mume' kwa njia isiyo halali!
ReplyDeleteHivyo msiwe na presha yu bukheri wa afya pika pakua kwa Mumewe wa Hiari!
ANA MIAKA 22 MTU MZIMA HUYO LABDA KAMA ANA TATIZO LA AFYA YA AKILI. ALIZOEA KUJIIBA NA MLIPO MRUHUSU TU KULALA NDIO MMEFANYA KOSA KESHANOGEWA. KESHO HAITAFIKA NA IKIFIKA ATARUDI HUKU ANALAMBA NDIMU.
ReplyDeleteInawezekana kudhani kuwa hajapotea kafichwa kumbe kuna baya lililompata. Ulimwengu huu una mengi!
ReplyDeleteZena kama unaona tangazo hili ni bora ukawataarifu ndugu zako kuwatoa wasiwasi.
Yuko kwa bwana amenogewa baada ya kulala siku moja. ishallah atarudi salama, kama si yeye basi mshenga
ReplyDeleteakirudi mkampime hiv. Nadhani mabinti wa staili hii wakiwekwa ndani huwa hawana maamuzi ya kulazimisha kinga.
ReplyDeleteInaelekea familia hizi kuna jambo mmemkosea huyu binti kwa jinsi nilivyolielewa hili tangazo.
ReplyDeleteHUYU SISTER ANAONEKANA KAJIGEMUA KULE KWETU KIGOMA TUNASEMA HIVYO,
ReplyDeleteBADO KIJANA HUYO ANAHITAJI KUWEKWA KIDOGO AKITOSHEKA ATARUDI NYUMBANI
mzuri hivi huyu kweli kapotea ama kahama au kahamishwa???
ReplyDeleteDuh...watoto wa siku hizi SIKU ZENU ZINAHESABIKA.....yakishamshinda atarudi kisanii kwa kisingizio "eti alichukuliwa MSUKULE"......kaaz kwel kwel!
ReplyDeletePoleni sana Wazazi na wana ndugu kwa fedheha mliyofanyiwa.
ReplyDeleteBi. Zenna Inshallah inawezekana yu bukheri wa afya kwa Mumewe mtarajiwa!
La muhimu, ni dalili suala lipo nje ya taratibu za kuyafikia mahusiano halali ya Mke na Mume,,,hala hala fanyeni haraka muwatimizie taratibu sahihi zikamilike Msela asije mjaza mimba mwanenu nje ya ndoa!
Yu buheri wa afya na bwanake wanakula asali kwa maziwa!
ReplyDeleteMmemchelewesha Binti ilitakiwa mumpe nafasi aende kwa Mumewe tokea kitambo tu, kosa lenu hamku mchunguza mwenendo wake,
Inaokenana alisha choka MAISHA YA NYUMBANI na sasa ameona amekua na alazimishe mwenyewe kuyaelekea MAISHA YA UNYUMBA!
Hapa ndio kinafika kipindi Baiolojia ya Maumbile na Kujitambua inapo zungumza!
ReplyDeleteWajameni, kipindi hiki ukiwa na ulezi au uzazi wa watoto wa Kike pia wa Kiume,,,inabidi uwe makini sana, na busara na utulivu wa hali ya juu,,,(utagombana sana),,,Asalaleee jazba, hasira na ghadhabu zinaweza kukufikisha Polisi,Jela hadi Mahakamani!
Huyo Galacha au Kachala ,Msela aliyemweka Binti mafichoni, kama ni Chinga atasimamisha safari za Misele Kiwanjani sasa anashinda Nyumbani, kama ni Mwajiriwa atadanganya kuumwa au ataomba mapumziko mafupi anashinda nyumbani!
ReplyDeleteGalacha ,Kachala au Msela ana kandamiza, anashinda na Msuli au Taulo kiuonini, yupo chumbani ndani ya 'mabunduki' kwa kwenda mbele!!!!
inaonyesha Msela alishaanza kumbemenda Zenna muda mrefu tu! ila wazazi na ndugu wa Binti hawakujua hilo.
ReplyDeleteSafari hii alipokwenda kwa Msela ilikuwa wamalize saa 12 jioni, wakanogewa mara 0hhh ikafika saa 2 usiku, ohhh mara saa 3 usiku,,,ohhh mara saa 4 usiku, Msela akamshawishi binti apige simu nyumbani adanganye ili walale wote,,,wakawa wamenogewa!!!
Huyu wala hajapotea ni shauri ya nondo tu.
ReplyDeleteJamani hii ni dunia ya siku hizi naomba tusiwe na wazo moja tu la kusema kapata mume.Yawezekana kweli kapata matatizo,pamoja taarifa imetolewa Polisi lakini huenda Polisi bado hawajajua au hawaja pata uhakika wa wapi yupo huyu binti.
ReplyDeletePoleni wazazi wenzangu,endeleeni kufanya juhudi msizubaishwe na maneno ya watu.Hata kama yupo kwa mwanaume ndo hamjui eti!Hivyo hamwezi kubweteka.Shida yenu kubwa ni kujua mtoto yu salama kabla ya kuja ya mume.Kama kweli yu kwa mume basi hata huyo mume ni mjinga.
Ashaolewa huyo... subirini atarudi na mjukuu!!!
ReplyDeleteWala msihangaike!
ReplyDeleteKama muelekeo wenyewe ni Mbagala, fanyeni kama mnasitukiza nendeni mtamkuta Msela kampakata miguuni Zenna wanakula bata kwa mrija 'wanasasambua maisha mapya matamu' pale Kiota kipya cha maraha DAR LIVE...!
Duhh bibie ameyashitukia maisha matamu ya unyumba!
ReplyDeleteZenna amekwisha onja tamu ya asali,,,akiwa angali mdogo hajui kuwa asali hiyo huwa inageuka kuwa chungu kama shubiri!
ReplyDeleteKudadadadeki,
ReplyDeleteMsela atakuwa anashinda mchana kutwa usiku kucha na bukta au pensi anababua!