Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.



Safi sana, ni bora mambo ambayo yamekwishatokea yakasahaulika maana hata yakiendelezwa hayawezi kubadilika mbali ya kununiana na kutafutana ubaya mpya. Hata vitabu vya dini vimeandika hivyo.
ReplyDeleteHii habari imefanya jioni yangu iwe nzuri
ReplyDeleteWagombanao ndio wapatanao, ole wao wale waliokuwa wachonganishi, watajibebaje!!!!!!!!!!!,
ReplyDeleteHongera Sugu na Ruge kwa hatua ya busara mliyofanya, hata malaika wa Mungu wanashangilia, maisha ni mafupi huitaji kugambana na mtu, kwani hatuijui kesho ikoje, kabla ya giza yatupasa kusamehena, ili ulalapo uwe msafi katika roho.
Good, ila muwe wakweli mbele ya Mungu kwanza.
ReplyDeletehongereni sana. Nimefurahi sana kusikia hivyo............. hiki ni kitendo cha kiungwana sana
ReplyDeleteI would not care less! naenda kunywa togwa.
ReplyDeleteruge kasalimu amri kisa uheshimiwa asingekua mheshimiwa asingekubali...hapo kamwomba sana nchimbi amuombee msamaha kwa mbunge ila ingekua ni msanii tu kamwe asingekubali inaonyesha jinsi gani anavyonyanyasa wasanii wadog
ReplyDeletekubali yaishe!!
ReplyDeletesugu snichter,najitoa chadema
ReplyDeleteRuge karudisha majeshi nyuma! Hai seheee Sugu ni kiboko,yaani lile bifu lenu limekupatia ubunge! mwe! mwe! mwe!
ReplyDeleteSASA HII IMEKAAJE NANI ALIYE KUWA MCHOKOZI NANI MWENYE HAKI YA KUMSAMEE MWENZAKE TUELEZE CHANZO CHA UGOMVI
ReplyDeleteHUO NDO UBINADAMU, KAMA MUNGU ANASAMEHE KWANINI BINADAMU WASISAMHEANE!!!
ReplyDeletevinega kalimeni sasa.......au hamjui kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake?????? mnalo!!!!!
ReplyDeletesugu vp msimamo wako kuhusu kupinga vazi la taifa umekubaliana nn na nchimbi?
ReplyDeletekama wamepatana safi kabisa ,,kwani mabifu siku zote hayasaidii ,,hongereni na iwe kweli kutoka moyoni.
ReplyDeleteSugu waaambie moja ya condition zako kwenye huo upatanishi ni lazima wapige nyimbo zako clouds fm including Ant virus lazima tuisikie hewani maana wamekubania sana nyimbo zako zenye ujumbe
ReplyDeleteIna maana Anti Virus ndiyo basi tena?????
ReplyDeleteDunia ya sasa ni vizuri ukawa na BUSARA zaidi kuliko JAZBA na UBABE.
ReplyDelete