Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Joachim Nyambo akipokea zawadi ya katoni ya Bia aina ya Ndovu kutoka kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi baada ya kuibuka mshindi wa kubaini ladha halisi ya aina ya vileo vinavyotengenezwa na kampuni ya Bia ya TBL.Mashindano hayo yaliyohusisha wannahabari wa mkoa huo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akizungumza na Baadhi ya Waandishi wa habari wa Jijini Mbeya wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya uzalishaji vileo ya TBL wakati wa kubaini ladha halisi ya vileo vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
Mshindi wa kwanza wa uonjaji ladha halisi za Bia zinazotengenezwa na Kampuni ya TBL Mbeya ambaye ni mwandishi wa habari wa Chanel Ten Saada Matiku akipokea katoni za Bia kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Bia mkoani Mbeya Calvin Martin, Matiku alizawadiwa katoni tatu za Bia.
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakitembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Iyunga jijini humo mwishoni mwa wiki.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Christopher Nyenyembe (kushoto) na mwandishi wa habari wa gazeti la Raha Tele George Chanda (katikati) wakionja Bia zinazotengenezwa na kampuni ya Bia Tanzania TBL katika shindano la kumtafuta muonjaji mahiri wa Bia za kampuni anayeangalia kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Edith Mushi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...