Dear all,

Watanzania wasomi ndio tatizo la nchi yetu.

1. Tunalalamika sana - badala ya KUTHUBUTU na kutumia fursa zilizopo kufanya mambo.

2. Tunapenda sana kuajiriwa "civil service and perdiem mentality".

3. We do not lead - tunawaachia ambao hawakusoma ndio wanajaribu kufanya biashara za kimataifa.

4. Hivi (jiulize) - Tanzania itakuwa wapi, iwapo kila msomi (with at least MSc.) angeendesha Enterprises za kimataifa - na kila mmoja akaajiri vijana 1,000+:
Kuzalisha umeme (mini-hydro; gas power plants, wood fired power plants etc),
Kutengeneza machize za kilimo (walking trcators; small motor pumps, food processing plants etc...)
Kutumia misitu yetu kutengeneza fanicha za kimataifa,
Kutumia bandari zetu na reli (Tanzania ndiyo nchi peke yake East & Central Africa yenye THREE Railway Corridors to the Ocean - Kenya is just thinking about their 2nd!!!- and we are the only country in Africa with SIX landlocked countries surrounding us!!) - je tunaitumiaje hii fursa.
La mwisho - ambalo pengine wengi hamtakubaliana nami - ni kwamba, kwa ujumla wa serekali zetu za awamu nne - serekali zetu pamoja na mapungufu yake - zimefanya kazi yake. (nasikia milunzi!!)

Kwa nini nasema hili?

Tuna kilometa ngapi za tarmac-ed Highways? - wasomi mnazitumiaje km zilizopo - kujenga biashara za kimataifa zenye tija - kabila ya kulalamika?
Je barabara ya lami toka Mwanza - Mtwara inatumikaje na wasomi?
Wengi tunaishia kwenye kununua daladala!

Wasomi tunaitumiaje KIA ku-exploit usomi wetu?

Wasomi wangapi wameanzisha miradi mikubwa kuutumia umeme wa ziada unaozalishwa Mtwara - kabla ya kulalamikia upungufu wa umeme sehemu zingine?

Bila wasomi kutumia fursa zilizopo na usomi wao kufanya mambo makubwa (zaidi ya Guest Houses) - pato la kodi la nchi litaendelea kudidimia mpaka nchi itafilisika kama Creece.

Hivyo wote - tuamke - tufanye mambo makubwa.

Let us take our Country's Economy Back - from donor advisors who are misleading us; Chinese government businesses that are giving us poor deals, etc!!! - ONLY US the "wasomi" can do it.

Amkeni

Nuhu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Nuhu amenena mwenye macho aone na mwenye masikio asikie na mwenye mikono na akili afanye jambo

    ReplyDelete
  2. ndugu umenena
    asante kwa kutukumbusha

    ReplyDelete
  3. Wazo lako ni zuri na kweli yote tunayaona ila tatizo kwangu binafsi ni kero ya kuombwa rushwa. Binafsi hapo ndio pananikatisha tamaa ya kurudi kuwekeza nyumbani. Labda mwenzangu unichangie mawazo hao wazee wa kuomba omba ndio mambo yako yaende unawafanyaje?

    ReplyDelete
  4. nipoteze muda wangu wote wa nn wakati njia rahisi ya kutoka ipo? siasa ndio mtaji rahisi wa kutoka nitadhirisha vipi usomi wangu bila kujulikana kwa wananchi?

    ReplyDelete
  5. Hoja unayo mkuu.Ila mimi sina utalaam wa masuala haya uliyoyazungumzia Elimu,uchumi na maendeleo..Kuna wadau humu huwa wanatoa hoja nzuri na mchanganuo kuhusu hili suala ulilolileta nadhani wataweka comments zao nzuri.

    David V

    ReplyDelete
  6. Ndugu yangu usiwalaumu wasomi wa nchiyetu hayo unayosema ni kweli lakini cirriculum za vyuo ambavyo hawa wasomi wanatoka sio relevant na labour market ndo maana wana kua wagumu kufanya critical thinking, resoning capacity ni ndogo ukiwauliza wana dai hawana mitaji wakati hela ya pombe wanayo.. Ila nafurahi kwamba wasomi hawahawa hawataki kufikiria we waache walale ili sisi tuwa waache wakiwa wengi na competition inkua kubwa hivyo bora tuwe wachache kupunguza competition

    ReplyDelete
  7. ... Ni rahisi sana kuwalaumu wasomi, ci wamesoma? Kuna mawili, kwanza mwandishi ni msomi na mfanyabiashara aliyefanikiwa. Pili, ni msomi aliyekosa ajira na anataka kuajiajiri na hivyo anachokoza mada ili apate msaada.Labda la tatu linaweza kuwa mwandishi hajasoma lakini ana biashara za kimataifa.




    Haya mambo ni rahisi kuyaongelea kama ndo umeshamaliza shule, ambapo unakuwa na matumaini ya kuhamisha milima. Kimsingi, ukweli wa mambo hauko hivyo. Biashara ni connection na connection hujengwa kwa miaka na hata kurithishwa kutoka familia moja hadi nyingine.
    Maana yangu ni kwamba, haiwezekani wewe ambaye muda wote ulikuwa shule, leo uwe na connection za biashara.


    Hauwezi kuwa sawa na mtu ambaye wakati wewe unasoma, yeye alikuwa anafanya biashara-huyu ana uzoefu na ana elimu ya biashara, wakati wewe una elimu let's say ya umeme bila uzoefu wowote.


    Ukitaka kujua ugumu wa hili, angalia jinsi wahindi wanavyofanikiwa ktk biashara. Siri ni nini? Wahindi wanajifunza biashara tangia utotoni na wanarithishana deals na hata wateja.


    Mwisho, hivi ni lazima wasomi wote wawe wafanyabiashara? Nani atakuwa mtafiti na mtaalam wa fani mbalimbali? No wonder prof UDSM walikuwa wanajifugia ngómbe, maana kuna watu wanafikiri kila mtu lazima afanye kila kitu.

    ReplyDelete
  8. msomi wewe sijui umesoma shule gani??unasema tanzania itafilisika kama Greece?Unajua kama greece inauwezo wa kuilisha tanzania??

    ReplyDelete
  9. nashukuru kwa kuwaamsha wenzio lakini wewe pia ni sehemu ya tatizo kwani unataka kuajiriwa. ulipokosa kazi ukadhani wa kulaumiwa ni wasomi wasiotaka kuanzisha kampuni ili upate kazi. Ujasiriamali ni kipaji na elimu. kuna watu ni wa kuajiriwa milele hao hawaepukiki hivyo kama wewe ni mmoja wao subiri utufanyie kazi.

    ReplyDelete
  10. Mwana Nuhu, tupe contact zako basi tukutafute. Kuwa msomi peke yake haitoshi, inahitaji mtu kama bw Nuhu wa kuweza kukusaidia ni namna gani unaweza kugenerate ideas za kuwekeza, pamoja na kupata mtaji (from zero) wa kuendesha shughuli hizo.

    ReplyDelete
  11. kaka nakuja..niko kwny last process ya kugenerate idea..i hope to launch it at the end of dis year..i hope wadau mtanipa support mtanzania mwenzenu kwa kuniungisha..naunga mkono hoja.

    ReplyDelete
  12. Kwanza kabisa napenda kumshukuru bwana nuh kwa hoja yake nzito na ya maana sana. Napenda kuwakumbusha wenzango tunaochangia huja hapo juu,issue sio about Nuh, ni about the problem. Ni afadhali usichangie hoja, kuliko to attack mtoa hoja. unayo haki ya kumpinga mtoa hoja.Naamini huyo mtoa hoja amesema maneno ambayo yapo, na yana ukweli na yako matatizo ya kufanya jambo hilo lisifanyike.Kwa mfano mimi binafsi, ni mtanzania mwenye asili ya kisomali ambaye nilikwenda nje kutafuta maisha na elimu, alhamdulilah nikafanikiwa. nikarudi nyumbani kuja ku invest niweze kusaidia nchi yangu na mimi binafsi nijiendeleze. Nilikutana na hongo, vurugu, fitna na kila aina ya mambo hata sijafakiria katika dunia hii ya 21st century yanaweza kutokea.Nina uraia wa tanzania( nimekaa nje muda mrefu sijachukua huo uraia wao), mke wangu sio mtanzania. Nimekuja kutembea nikaona investment opportunity, nikaja na familia yangu..nikafanya kila kitu kwa mujibu wa sheria. Nimesumbuliwa miezi mitatu, nimeitwa mpaka alshabab.....nimehonga kutoka polisi. Kwa kifupi, kwa sasa niko Uganda na nime invest on the same opportunity nilioina Tanzania. naishi kwa raha na starehe, alhamdulilah. Hamna hata siku moja nimetoa hongo, nimesaidia kujenga sekondari hapa. Nawajua viongozi, some of them are my friend. Vilevile nawasaidia vijana wa one of the University hapa, namna ya kujiajiri.hilo ni wazo binafsi, sisemi kwamba waliokuwa na nafasi ni wabaya. Inawezekana nimekutana na bad experiance, its possible. Lakini naamini kuna wengi wamekutana na bad experiance.Nimeandika haraka haraka samahani kwa kuchanganya lugha.

    ReplyDelete
  13. Mimi ni msomi na nina shahada mbili za biashara kutoka Marekani (B. Sc., na MBA (Finance).

    Tatizo ni serikali yetu, sio wasomi. Nilijiajiri mwenyewe, na kuwa na wafanyakazi 15 katika shughuli zangu. Lakini ilinibidi nifunge biashara zangu kwa kuwa kila siku, nilitembelewa na TRA kazini, wanataka document za kila kitu. kila wiki wanakuja watu tofauti, hata nilipowaripoti naambiwa wanafanya kazi zao.Kila mwaka nikipeleka makaratasi yangu, TRA inakataa kuwa revenue yangu sio ya kweli, lakini wanakubali ni ya kweli nikiwapa hongo. Muda wangu mwingi nilitumia TRA na polisi njaa wanaotaka chai kila wiki.

    Nikiagiza mali nje, hamna system ya haraka ya kutoa mali yangu bandarini na napata gharama nyingi za kipuuzi. Mzigo wa aina moja natozwa ushuru tofauti kila nikiuleta.

    Pia, nilipoenda mahakamani kuomba haki yangu (mteja alinizulumu)sijapata haki yangu mpaka leo na nikapoteza milioni 20.
    Sitaongelea matatizo kama ya umeme, maji, elimu, na tiba.

    Kama serikali itatetea haki ya mwananchi badala ya kutetea kwa mdomo tu na kuthibiti hongo, basi wasomi kama mimi tutarudi. Kwa sasa, serikali yetu ni maneno tu na siasa yetu na fikra zetu bado ni za ujamaa na kujitegemea hata kama tuna vyama vingi, kibiashara bado hatujakomaa kimawazo.

    Kwa sasa, sina nia yoyote ya kurudi nyumbani.

    ReplyDelete
  14. Nakusikia kama vile nasikia sauti ya mlevi tu ambaye hajui anachokiongea na nafikiri anaongelea nje ya Tanzania. Kama uko TZ Mr Nuhu nenda kachunguzwe akili sio timamu hata kidogo. Tafakari nilichokuambia kwa kuangalia mistari yako

    ReplyDelete
  15. Hoja bomba wasomi tuamke

    ReplyDelete
  16. We uliyeandika hii lazima ni either mtoto wa wafisadi au u have connections.
    Na i can see you have gone to school because unajaribu kutranform what exactly they taught you in Business class in reall world it does not work that way, but you have good points.
    Ni kweli watanzania we are not aggressive on maswala ya kimaendeleo, ila stage tuliyofika sasa hivi Tanzania tunawasomi weengi sana na wote wanajua what is our big problem..UONGOZI wetu .
    Either ni wa somi au sio wasomi maendeleo hayaji kirahisi sometimes hata KUMWAGA DAMU, nasema hivyo kwa sababu muda umefika kwa CCM kutoka madarakani..kwa kura au kwa DAMU, otherwise hatutafika mahali.

    utakuwa na wasomi weengi kama our GOVT is not supporting small business, technological advances..hatufiki mbali.

    Cha kwanza CCM out ...and have leaders who are 100% for the good of the country na its people.

    ReplyDelete
  17. HONGERA MDAU NUHU!

    Hapo umepiga kwenye kubwa la Maadui wa maendeleo yetu.

    Kwa maoni yangu kitu kikubwa ambacho kimetuathiri Watanzania ni kuwa na kiwango cha chini cha Muamko wa Ujasiriamali kutokana na aina ya Siasa tuliyowahi kupitia ''SIASA YA UJAMAA'' ingawa kila kitu kina uzuri na ubaya wake Ujamaa ulitupa faida upande mmoja na upande wa pili ulituletea balaa kitu kama hiki ulichotoa ktk Mada hii ,kushindwa kujiamini, kwa kujiendesha kibiashara na Kiuchumi kwa tija, yaani (Mwamko wa uwezo wa Kiujasiriamali) kinacho sababisha watu wengi kupendelea Kuajiriwa na badala ya Kujiajiri.

    Sasa kwa Mlengo huo ndio unazalisha aina ya Viongozi na Jamii ambayo haithamini uwezeshaji wa Wajasiriamali, na mara nyingi mtu ukiwa na mtazamo wa Ujasiriamali unaonekana kama Raia kutokea Sayari nyingine na wakati wote watu hukukatisha tamaa na mtazamo wako au wanakuwa hawaamini kama mambo yanaweza yakawa.

    ReplyDelete
  18. WEWE MSOMI ULIYETOA HOJA, EMBU TUELEZE WEWE UMEFANYANINI CHA MSINGI HADI UNALAUMU WENZIO! BIASHARA NI MIPANGO NA MIPANGO HUANDALIWA KWA KUJENGA MISINGI OTHERWISE KWA NAMNA UNAVYOSHAURI WASOME KUINGIA KWENYE BIASHARA TUTAJENGA KIZAZI ZA FAILURES AS A RESULT WASOMI WATAGEUKA KUWA MATAPELI NA WATU WASIO NA MWELEKEO

    ReplyDelete
  19. Ni rahisi sana kuzungumza hayo uliyoyazungumza. Sijajua msingi wa wazolako. Inawezekana unachokoza Mada ili upate hali halisi ilivyo. Kwa ufupi tu, mwanzo wa Biashara ni Mgumu, unahitaji uwekezaji kabla hujapata faida. Shuleni hatutafuti fedha, tunatafuta elimu. Ukishapata elimu unaingia mtaani, kama ni mtaji unakuwa nao mdogo, katika mazingira hayo unahitaji uwanja rafiki...... Baba, hapo ndo mambo yanapoanzia kuharibika, Kwanza Competitors wako hawalipi Kodi,washajua mashimo yote ya kukwepa kodi, Tender wanazipata kabla hazijatangazwa, Viongozi wetu ni Miungu watu, anaweza kupindisha sheria anavyojisikia yeye, vyombo vya dola havisimamii tena haki za raia wake, Pesa imekuwa kila kitu. Kwa ufupi ni Mazingira yanayokutaka Umkane Mungu kwanza, Ujanja ujanja umekuwa mwingi mno..... Inawezekana unazungumza haya ukiwa kwenye nchi ambayo mifumo yake iko wazi na ni ya kuwajibishana. Hebu jaribu kwanza kufanya hicho unachokisema halafu baadaye naamini utakuja na mada nzuri zaidi ya hii, na sitashangaa kuona unazungumza Kinyume kabisa na hii Mada!

    ReplyDelete
  20. Badala ya kulaumu tuchukue yale yatakayosaidia nchi kuendelea tuyafanyie kazi.
    Ni kweli wote hatuwezi kuwa waajiriwa au wote hatuwezi kuwa wajasiriamali wazo la Bwana Nuhu ni kuwa tutumie fursa zinazopatikana kwa kutumia elimu tuliyoipata kwa manufaa yetu na Taifa letu badala ya kubaki tunalaumu kwamba huyu kasababisha kile au hiki wakati hatutumii kikabilifu fulsa zilizopo pamoja na rasilimali zilizopo kwa manufaa yetu na Taifa letu.badala yake tunatamani mana kama tupo jangwani enzi za Musa.
    We have to toil to get whatever we are dreaming of achieving. Let's think in an entrepreneurial way to succeed in Life.

    Nuhu hana maana wote tuwe wajasiriamali lakini kwa kiasi fulani hilo linawezekana kwa sababu ukitegemea mshahara tu kila siku bila hata kuanzisha ka business kadogo ka ku subsidize huo mshahara utakwama ndugu yangu maana kila siku tunalia mshahara hautoshi.

    Big up Nuhu kwa kuleta hii mada.
    nimekupenda!

    ReplyDelete
  21. Nuhu umelalamika tu bila kusema wewe umefanya nini.

    ReplyDelete
  22. Mheshimiw mdau umenena sawiya kabisa!! Kuhusu wasomi ni kweli wapo. Na kuhusu mbinu tofauti za kutafuta biashara kwa ajili ya kunufaisha taifa kwa ujumla pia wanazo. Tatizo ni kwa walioshika mpini, hao wasomi wameshika kwenye makali!!

    Nasema hivi kwa maana ya kwamba, asilimia kubwa ya wasomi wa nchini wakitaka kufanya biashara inawawia vigumu maradufu, raia unaanza kulipa kodi kabla hata biashara haijaanza, huko uendako kuna kufika kweli!?

    Wazee wanang'ang'ania uongozi utafikiri hakuna kufa, na juu ya hio kumekuwa na utaratibu wa kupeana nyadhifa kwa kuhofia ukweli wa mauchafu yanayofanyika kuibuka. Hivyo madudu yanaendelea kuzalisha madudu zaidi. GIGO = Garbage In Garbage Out!!

    Na tatizo lingine kubwa ambalo wengi tumekuwa tunalijua lakini sijui ni woga ama tunguri, limekuwa likufumbiwa macho tu. Hili ni tatizo la kuwapa viongozi wenye kuhodhi biashara kadhaa na kubwa nchini, nyadhifa katika vyombo vya kuendesha biashara za taifa. Lazima kutakuwa na CONFLICT OF INTEREST. Lazima aanze kujipendelea mwenyewe halafu ndio amwangalie huyo msomi (ambae kwa yeye anamuona kama KIHEREHERE) aliyekuja na maombi ya kufanya/kuanzisha biashara ama kuwakilisha wazo la biashara.

    Kwa ufupi wasomi tunaonekana kama ndio wachawi wakati nchi za wenzetu wanawathamini wasomi na kujua kwamba wao ndio tunu la taifa. Ingekuwa nchi yetu inathamini wasomi, tatizo la BRAIN DRAIN lisingekuwepo kama ilivyo sasa. Madaktari, walimu, mameneja, n.k. wote wanakimbilia nchi wanazoona zitawapatia ufumbuzi kujikwamua kimaisha.

    Tukiacha sera za kupeana na kubebana tutaweza na ndio itakuwa sehemu muafaka ya kuanzia, vinginevyo tutaendelea kupeana maumivu na wachache tu ndio watakoendelea kufaidika.

    ReplyDelete
  23. Mi naona porojo tu, yaani mtoto wa mkulima anapata wapi hio connection na mtaji hadi afanikiwe kama mdau unavyoshauri? Capital ndo issue. connection, etc.

    ReplyDelete
  24. sawa Nuhu, lakini labda ungelitonyesha kwa vitendo. Sasa basi tuambie wewe umefanya lip katika haya uliyoyaleza? au nawe ni domo kaya kama viongozi wetu wengi nchini?

    Tuambie unafanya nini, ofisi zako ziko wapi, uko tayari kiasi gani kwa watu wenye ideas kukufata uwape muangaza zaidi ili kufanikiwa na haya uliyoyasema?

    Nasubiri majibu, na nategemea michuzi itaweka maneno haya.

    ReplyDelete
  25. Nuhu umeongea hata kama hatuupendi ukweli. Wote mnaotoa sababu ndiyo mila yenu.. Nawapenda watu Kama Nuhu ambao hutoa hoja za Nguvu za kutukumbusha kwamba uchumi lazima kwa asilimia 70 umilikiwe na Watanzania na si vinginevyo. Kukabidhi biashara yote kwa wageni na kuendelea na visingizio mbalimbali hakutaemdeleza nchi. Tuamke tuthubutu, tujiamini na tuwekeze hata Kama ni kwa ubia mwishoni tutafanikiwa. Doing nothing is not an option! Excuses is even more shameful.

    ReplyDelete
  26. Mdau ameongea, nakubaliana naye ila si kwa yote!! Ukiongelea wasomi, halafu ukawa unawamaanisha wale wa UDSM, sijui nisemeje.. pale watu wana vyeti ilimradi vyeti, reasoning and thinking capacity hazilingani na vyeti vyao. Wengi wao wamefaulu kwa kudesa.. Nalisema hili wazi nimeona, nilkuwa mwanafunzi UDSM, Bachelor of Commerce mwaka 2006-07. Course moja e.g Accounting, wanafunzi walikuwa wanafika mpaka 800, mwalimu mmoja anaefundisha ubaoni, sio kwa kutumia projecta au powerpoints (Except Mr. Assad, at the same time Microfons hazifanyi kazi na kipindi ni mchana wa nyuzi joto 28-10 C . Umeme hamna kwa hiyo hata ventilation ndo hivo tena. Sema baada ya miaka 3 ya kusoma hivi utamuita huyu mtu msomi?.. Baada ya mwaka uzalendo ukanishinda nikaenda kusoma nje, Netherlands.. lkn je ni wangapi wenye bahati hiyo? si wengi.
    On the other hand sidhani kama wasomi wote wanatakiwa kuwa wafanya biashara, utakuwa unasema kama wazungu walivyokuja na Microfinancng wakadhani hili litatatua tatizo la umaskini, ikiwa wakiwapa watu mitaji kwa bei rahisi, wakishindwa kufikiria kwamba si kila mtu mjasilia mali. Matokeo yake? sihitaji kusema, riba za Microfinancing institutions kubwa kuliko kwenye benki. Je imeondoa umaskini? ...still to be discussed...

    Cha msingi kila mtu awajibike kwenye kazi yake, let us be honest and ethical, tufanye kazi kwa bidii na tuzipende kazi zetu, haijalishi ni kazi gani na tufanye kwa ufanisi, kwa kujituma na si kwa sababu bosi amekutuma na akiondoka wewe porojo! Mambo ya rushwa na kitu kidogo haitusaidii wala kutufikisha popote, na inawakatish awatu tamaa, ambao walikuwa na nia njema ya kuwakomboa wengine kwa kuanzisha miradi midogo midogo itakayoajiri vijana wengi.

    ReplyDelete
  27. kaka mina kushukulu kwa mawazo yako nimazuli sana,tatizo watanzania wengi tunapenda kuajiliwa tukiofia kuanguka kimaisha lakini mda umefika watanzania kuamka,tuna weza wenzetu wameweza wananini?,asante kwa mawazo yako nathani yatafanyiwa kazi.

    ReplyDelete
  28. Mambo makubwa matatu hapa chini:

    Hili suala limekuwa ni tatizo kwetu kutokana na

    1.Aina ya Siasa 'Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea' ambayo ndiyo imejenga msingi wetu wa kimwenendo, Siasa hii kama Wadau walivyoeleza juu imetusaidia upande mmoja (Ushirikishwaji wa Watu na Kuthaminiana N.K) na imetuathiri upande wa pili (Muako wa Kiujasiriamali).

    2.Aina ya Mfumo wetu wa Elimu hauendani na mwenendo na mabadiliko ya mahitaji yetu hasa Kiuchumi na kasi ya Kimaendeleo.
    (Mfumo wa Elimu hauwaandai wahitimu kujiajiri,,,sababu iliyopelekea Taasisi kama VETA-Ufundi, NIIT-Usafirishaji ,SIDO-Viwanda vidogo vodogo, na CBE-Chuo cha Biashara,UCC-Chuo Kikuu Komputa kubadili Mitaala kwa kubadili Kozi zake na malengo ziende na Wakati na kasi ya Mabadiliko.

    3.Utawala wetu Umedumaa kulingana na (Msingi wetu wa Itikadi No.1 juu 'Ujamaa') na Mfumo wetu wa Elimu No.2 juu), ni kuwa Mamlaka hazitoi uzito juu ya Uwezeshaji na Watu hasa Wahitimu kujiajiri.

    Kitu ambacho Mashirikisho ya Maendeleo kama WB-Benki ya Dunia, IMF-Shirika la Fedha la Kimataifa na IFC-Shirikisho la Kifedha la Kimataifa,yanasisitiza zaidi kuelekeza maendeleo kwenye Sekta Binafsi,SME-Biashara ndogo ndogo na Kujiajiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...