Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa shambani kwake Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Shamba hilo ni la manyasi ya kulishia mifugo kwa njia ya kisasa (zero grazing), akiwa ni mmoja wa wafugaji kijijini hapo. Rais Kikwete, ambaye aghalabu hutumia muda wake wa likizo shambani kwake, pia analima pia mananasi ambayo hustawi vizuri katika wilaya hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Mwantumu Mahiza. PICHA NA IKULU
Home
Unlabelled
JK katika shamba lake la manyasi ya kulishia mifugo kijijini Msoga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tehe Tehe hehe hehe! Ndio Mzee! :D
ReplyDeleteHongera Mheshimiwa Rais Kikwete maana vijana wengi wa Kitanzania wanadhani kuwa kazi ni kufunga tai na kukaa ofisini, tunahitaji vijana kuwa wakulima wa kisasa ili Supermarket zijae bidhaa za Tanzania maana itafika wakati tunapata maziwa fresh kutoka South Africa.
ReplyDeleteumekuwa mfano mzuri muhwshimiwa rais,tunahtaj marais wanaowekeza ktk nchi zao ili kutoa fursa za ajira zaid na kukuza mitaji.
ReplyDeleteKizungu wanaita HAY haya manyasi -- yanauzika sana hapa Marekani mpaka hayo manyasi yanasafirishwa toka hata Canada na huu ukame uloikumba marekani ya kusini (Texas hasa -- roli moja lilojaa manyasi kama haya la futi 53 likitolewa Southern California mpaka katikati ya Texas (mwendo wa siku mbili - kilometa kama 2000 hivi) gharama yake inakuwa around $8,000 manyasi na usafiri ndani. Sijui bei hapo home zikoje kwa wenye idea jamani?
ReplyDeleteSafi sana!! Tunajua kufuga kafundishwa na rafiki yake Lowasa lakini je hilo shamba lina ekari ngapi? Usikute shamba lenyewe eka tatu tu (Mtu wa Pwani huyo) kwao kulima ni adhabu kuu, teh teh
ReplyDeleteHongera Mhe. Raisi JK kutuhamisisha Kilimo Kwanza halafu wewe mwenyewe ukaonyesha kwa Vitendo!
ReplyDeleteNi dalili njema pia Wakuu watatu wa Afrika ya Mashariki kushiriki Ufugaji wa ng'ombe,
-Raisi Jakaya M.Kikwete:TANZANIA
-Raisi Yoweri K.Museveni:UGANDA
-Raisi Paul Kagame:RWANDA