Katika jitihada za kuunga serikali mkono kwenye kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata huduma za afya salama kwa ukaribu na ya salama, Dr. Ole Lengine, Mtaalamu Daktari wa Binadamu aliyebobea kwenye afya ya viungo Muhimu, yaani Pua, Macho na Kinywa , amepanua dispensary yake ya Ekenywa iliyopo maeneo ya Mwembechai -Magomeni, jijini Dar es salaam,  kwa kufungua kikwangua anga cha ghorofa Tatu. 

Kwa sasa Hospitali hii ina uwezo wa kulaza wagonjwa zaidi ya 50. Pamoja na huduma ya utaalamu nguli ya macho , pua na kinywa, pia huduma zingine za afya zinatolewa kwenye hospitali hii. 

Hospitali hii ipo mbele kidogo ya kituo cha daladala  cha mwembe chai, ukikata kulia kabla ya kufika kwenye makutano ya mataa ya Morocco road na Kawawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kama ni Mtaalamu wa ENT ambayo ni Ears Nose and Throat kiswahili ni Masikio, Pua na Koo na si Macho Pua na Kinywa, E stands for Ears not Eyes Mtaalamu wa macho ni Ophthalmologists au opticians

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni wapi wameandika ENT? Nisahihishe kama nimekosea kusoma kwani sioni hoja inapotokea

      Delete
  2. Ku-'ekenywa' ndio kufanywa nini??? Jina ni sehemu muhimu ya any kind of business undertaking. Mwezi huu mta'ekenya' wangapi?

    ReplyDelete
  3. Enkenywa ni neno la kimasai lenye maana ya kumekucha au kumepambazuka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...