Kwa mara nyingine tena tunashukuru sana kwa msaada wenu.
Update za mipango ya misa ya kumuaga marehemu na mazishi ni kama ifuatavyo.

Misa ya kumuaga marehemu itafanyika Jumapili Februari 19, asubuhi (10 am) katika kanisa la Takoma Park Seventh Day Adventist Church, lililoko 6951 Carroll Avenue, Takoma Park, MD 20912. 10am mpaka 11am ni muda wa kumuaga marehemu. 11am asubuhi mpaka 12 noon misa itaendeshwa. 

Baada ya hapo tutakuwa na chakula cha mchana katika ukumbi wa hapo kanisani. Mume wa marehemu ameomba watu wote wajulishwe kwamba hairuhusiwi kupiga picha mwili wa marehemu. Tafadhali tulizingatie hili.

Mazishi yatafanyika 10.30am Jumatatu Februari 20 katika makaburi ya Gate of Heaven yaliyoko 13801 Georgia Avenue Aspen Hill (wakati mwingine GPS itaonyesha Silver Spring), MD, 20906. Tutakutana 8.30am J.B Jenkins Funeral Home iliyoko 7474 Landover Rd, Landover, MD 20785. Msafara wa mazishi utaondoka J.B Jenkins Funeral Home 9 am kuelekea Gate of Heaven.

Kwa mara nyingine asanteni sana na tunamtakia mpendwa wetu Christavina, tumziko jema. Shukrani Magoma

Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Teddy (301.254.4169); Makaya (202.460.1044); 

******R.I.P Christavina******

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...