Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed G. Bilal amefungua rasmi tawi la NMB Mkuranga Alhamisi, tarehe2 Februari 2012. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Makamu wa Rais aliipongeza NMB kwa kufungua tawi na kusaidia sekta ya kilimo, hususani zao kuu la biashara la wilaya ya Mkuranga ambalo ni korosho.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing akizungumza kwenye ufunguzi huo alisema " NMB inayofuraha kuwa benki ya kwanza kwenda Mkuranga na kutoa huduma, pia kuwa benki yenye kuhudumua asilimia 40 ya watanzania wenye akaunti. Hadi sasa NMB ina matawi zaidi ya 142 na ATM zaidi ya 450 ambazo ni nyingi kuliko benki nyingine yeyote Tanzania".
NMB ndiyo ilikuwa benki ya kwanza kuanzisha huduma ya benki kwa kutumia simu kupitia huduma yake ya NMB mobile ambayo hadi sasa jumla ya wateja 550,000 wanaitumia kupata huduma za kibenki kama kuangalia salio,kutuma fedha kwenye akaunti nyingine, kumtumia fedha asiye na akaunti, kununua muda wa hewani, LUKU au kulipia DSTV, DAWASCO au TRA.
Ufunguzi huo ulihudhuliwa na wakazi wengi wa mkuranga wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mbunge wa Mkuranga Mhe Adam Mallima.


Ufunguzi huo ulihudhuliwa na wakazi wengi wa mkuranga wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mbunge wa Mkuranga Mhe Adam Mallima.
Habari zenu jamani,poleni kwa kazi.
ReplyDeleteNdugu yangu Michuzi mimi ninaswali la husu matumizi ya maneno haya:-
MAKAMU AU MAKAMO.
Naomba tupewe msimamo wa matumizi yake.Lipi ni sahihi au yote ni sahihi.Maana napata mkanganyiko kuwa mara naona makamo au makamu.
Kwa kukusaidia mdau ni kuwa Makamu ni cheo cha pili cha madaraka fulani mfano Makamu mwenyekiti, makamu mkuu wa chuo au makamu wa Rais. na neno makamo ni kadirio la mtu au umri mfano unaweza kusema makamo yake ni kama miaka 30 au makamo yake bado ni kijana mdogo. kwa hiyo hayo ni maneno tofauti. lakini naona ankal yeye kaja na neno jipya ukitazama kichwa cha habari ameandika Makakamu naona hilo halipo hata kwenye msamiati wa kijaluo hahahaha.
ReplyDeletemdau Zee la kiswahili
Zee la kiswahili,nashukuru sana kwa ufafanuzi wako.
ReplyDeleteKwa mtazamo huo na maana hiyo tuko pamoja na hata mimi nilikuwa naelewa hivyo.
Utata wangu ulikuja pale mtandaoni mara nyingi,na has wakiandika tukio likiwa Zanzibar utaona wansema MAKAMO wa Rais,au MAKAMO wa pili wa Rais Zanzibar lakini waandishi blog hiihii.