Makamu Wa Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa na mavazi ya asili ya kabila la Kikonongo baada ya kuvishwa na kutunukiwa uchifu wa Kabila la Kikonongo na machifu wa Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mpanda wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mtemi na Chief Mkuu wa Kijiji cha Inyonga, George Mbaula (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Machief wa Inyonga, baada ya kumvisha nguo za asili ya Kabila la Kikonongo na kumkabidhi mikoba ya kuwa Chief wa Kabila hilo, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa jana.
Makamu a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Inyonga Mkoa wa Katavi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa katavi jana.
Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Inyonga, baada ya kumaliza kuwahutubia katika mkutano wa hadhara akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mkoa wa katavi ndiyo mkoa mpya au vipi? Hivi bado kuna ma chief Tanzania nilifikri waliishaga wakati wa mkoloni.

    ReplyDelete
  2. Hawa ndio Watanzania Asilia,

    Wakonongo.

    ReplyDelete
  3. Leo nimepata jipya, na umri wangu wote huu wa nusu karne sijawahi kusikia hilo kabila la Kikonongo. Hili ni kabila kweli au ni ukoo tu?

    ReplyDelete
  4. nadhani ni kabila la wakimbo(u) kwa sababu kwetu singida wakimbu pia tunawaita wakonongo. walihamia singida toka miaka mingi kutoka maeneo ya urambo na mpanda. wana utamaduni unaokaribiana na wanyamwezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...